Nani anambeba Profesa Kapuya?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Nani anambeba Profesa Kapuya?



Na Ezekiel Kamwaga



Kuna watu wanazaliwa na bahati. Wengine wanakutana na bahati
wakati fulani katika kipindi cha maisha yao. Wengine
wanaitafuta na kupigana kwa ajili ya bahati - Malcolm X

WAKATI aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Omar Ali Juma,
alipofariki dunia mwaka 2002, magazeti ya Tanzania
yalionyesha picha ya Profesa Juma Athumani Kapuya, akilia kwa
uchungu kuomboleza msiba huo.

Kapuya alilia kwa uchungu katika namna ambayo sijawahi kuona
kiongozi wa kitaifa akifanya hivyo hadharani. Ilibidi ndugu,
jamaa na marafiki wa marehemu, wakiwamo baadhi ya mawaziri
wenzake, waende kumshika ili kumtuliza.

Mara ya mwisho kupata taarifa za kiongozi wa kitaifa kulia
hadharani ilikuwa ni wakati wa msiba wa aliyekuwa Rais wa
Ufaransa, Charles De Gaulle, katika miaka ya sabini, pale
aliyekuwa mtawala wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jean Bedel
Bokassa.

Alibubujikwa na machozi mbele ya jeneza la Gaulle uyo na
kuishia kusema, “Baba….Baba… Baba.”

Baada ya kuona picha za Kapuya akilia, wakati ule ghafla sura
ya Bokassa ikanijia kichwani (na hawafanani hata kidogo).

Nikajiuliza: Kwa nini Profesa alie vile? Dk. Omar alikuwa
nani kwake? Au ndiye Godfather wake?

Hii ni kwa sababu, kwa maoni yangu, Profesa Juma Athumani
Kapuya, hastahili kuwa waziri wa wizara yoyote hapa nchini
kwa sababu ya rekodi yake ya utendaji tangu apewe fursa.

Kwa mambo ambayo ameyafanya katika miaka ya nyuma, Kapuya
hakukuwa na sababu ya kubaki naye serikalini.

Labda kama anayemteua pekee ndiye anayeujua uzuri wake.
Nikiwa mwanafunzi wa kidato cha nne mwaka 1998, Kapuya
alikuwa waziri wa Elimu.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, mitihani ya
taifa ilivuja kiasi kwamba baadhi ya mitihani ilionekana
ikiwa imebandikwa kwenye vituo vya daladala kabla
haijafanyika.

Mtihani ule ule uliokutana nao kwenye kituo cha daladala
kabla hujafika shuleni, ndiyo ule ule uliokuja kukutana nao
kwenye chumba cha mtihani.

Hatimaye serikali ikaamua kuifuta mitihani hiyo. Hasara
iliyopatikana wakati huo haijapata kuelezwa hata leo. Na
tangu wakati huo, ‘ugonjwa’ wa kuvuja kwa mitihani umekuwa
‘donda ndugu’ kwa serikali.

Pamoja na kashfa hiyo kubwa kwa serikali, Kapuya akaendelea
kudunda tu kama kawaida. Akaendelea kuwa waziri na akasema
hatajiuzulu kwa vile eti “hahusiki.”

Katika nchi ambazo waziri anajua wajibu wake, na serikali
inafahamu maana ya uwajibikaji, Kapuya alikuwa ama ajiuzulu
au aliyemteua alipaswa kumtema katika baraza lake la
mawaziri.

Hilo halikufanyika. Na matokeo ya yeye kutochukuliwa hatua
yoyote ni kwamba tatizo la wizi wa mitihani limeendelea.

Kama aliyemteua Kapuya hakumchukulia hatua, yeye angekuwa na
nguvu gani ya kuwachukulia hatua wa chini yake?

Na nakumbuka ni katika kipindi hicho ndipo alipokuwa
akifanya maamuzi ya ajabu ajabu kwenye masuala ya michezo.
Nakumbuka zaidi tukio la kushusha au kupandisha daraja tisiyostahili.

Kwa sababu ambazo ni serikali yetu pekee inazifahamu, Kapuya
akaendelea tu kupeta na kuwa waziri.

Alipopelekwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
kama kawaida yake, Kapuya akafanya jambo ambalo lilizua
mjadala katika vyombo vya habari.

Alitumia ndege ya jeshi kufanya ziara binafsi katika jimbo
lake la uchaguzi. Kimsingi, kwa wadhifa wake, alikuwa
anaruhusiwa kutumia ndege hiyo. Lakini tatizo akawa anatoa
lifti kwa watu. Kiutaratibu, hili ni jambo ambalo watu
hawakuwa wakilielewa.

Haya yalikuwa matumizi mabaya ya mali ya umma. Katika nchi za
wenzetu, hili lingechunguzwa na kufanyiwa kazi. Na
ingethibitika kwamba mheshimiwa alitoa lifti kushoto,kulia na
katikati, ni lazima rungu lingemwangukia.

Lakini hiyo ni nchi nyingine, si Tanzania. Hapa kwetu, hilo
likapita kama lilivyokuja. Juma Athumani Kapuya akaendelea
kuwa waziri hadi aliyemteua alipoamua kumrejesha kwenye
Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.

Lengo la aliyemteua kumpeleka katika wizara hiyo nyeti
silijui. Wizara hii ni nyeti kwa vile inagusa kundi lenye
watu wengi hapa nchini.

Sensa zote zilizowahi kufanyika nchini zimethibitisha pasipo
shaka kwamba nchi yetu ni ya vijana. Kwamba karibu robo tatu
ya watanzania ni vijana. Kwa hiyo waziri wa wizara hii
anashughulika na walau nusu ya watanzania.

Anatakiwa kutazama maendeleo ya kundi hilo kubwa la watu.
Katika dunia ya sasa ambayo ina tatizo kubwa la anguko la
uchumi. Ni wizara ambayo, kwa maoni yangu, inahitaji mtu
makini kwelikweli.

Cha ajabu akapelekwa Kapuya ! Na kama kawaida yake, tayari
kashaharibu na ninaweza kukuhakikishia kwamba ataendelea kuwa
waziri katika serikali hii.

Kama Kapuya angekuwa aina ya waziri anayestahili kuongoza
wizara hiyo, huu mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kufanyika

Mei 5 mwaka huu, usingefikia katika hatua ya sasa.
Yeye angekuwa amekutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama
vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kabla hawajafikia hatua
waliyofikia sasa.

Angekuwa tayari amempa rais taarifa kuhusu matatizo ya
wafanyakazi. Rais angepanga kukutana na wawakilishi wa TUCTA
kuweka mambo sawa. Kama serikali ingeona ina uwezo wa kutatua
tatizo hilo, ingelitatua mapema au ingewaeleza wafanyakazi
ukweli kuhusu hali halisi.

Lakini Kapuya hana muda wa kufanya haya. Kwake yeye, ni
afadhali aende Uwanja wa Taifa kwenda kukabidhi Kombe la
Ubingwa wa Ligi Kuu kwa klabu kipenzi chake ya Simba !

Waziri wa Kazi anapata wapi muda wa kwenda kuangalia mpira na
kukabidhi makombe wakati mgomo wa wafanyakazi ukiwa unanukia?

Hivi, kama mgomo huu utafanyika, yeye atakwepa vipi lawama za
kuhusika?

Halafu sikiliza taarifa zake kwa wana habari tangu mgomo wa
wafanyakazi ulipotangazwa. Wakati wafanyakazi wa serikali kuu
ndio hasa wanaodai kuumizwa na mishahara yao kiduchu, yeye
anakwenda kuzungumzia mishahara ya watu wa sekta binafsi
ambayo serikali haihusiki.

Mwalimu anahusika vipi na mshahara wa wachimbaji madini na
mahausigeli? Kwa nini alifanya mkutano kutangaza mishahara ya
watu ambayo serikali si inayolipa? Inachekesha. Sana tu.

Kama mgomo wa wafanyakazi utafanyika, uchumi wa nchi yetu,
ambao tayari uko taabani, utaathirika sana. Na najua hakuna
anayejali katika serikali yetu.

Na Kapuya ataendelea kuwa waziri katika serikali hii. Kwanza,
yeye si aliyegoma. Watakaogoma ndiyo wenye matatizo. Yeye
ataendelea kupeta.

Sina hakika kama ni bahati pekee ndiyo inayombakisha Kapuya
madarakani. Lakini kama ni bahati, basi pengine mwenzetu ana
bahati ya kuzaliwa.

Vinginevyo nina imani kwamba yupo anayemlinda Kapuya ndani ya
serikali yetu. Swali pekee ninalojiuliza kichwani ni kwamba;
ni nani huyo Godfather wa Kapuya?

Maoni haya binafsi yamechapishwa katika Mwanahalisi Toleo Na.

187.
 
Nadhani mdogo wake na Mama Salma ni mke wa Kapuya! sina uhakika san a
 
Nasikia huyu ni profesa wa Botany! Wapi na wapi katika kuendesha siasa?
 
KAPUYA KWELI NI MOJA YA TEUZI ZA HOVYO KATIKA NAFASI ZA JUU ZA SIASA ZA KWETU TANZANIA, huyu Kapuya anaungana na wanasiasa wa kariba ya Sophia Simba, Karamagi, Kingunge, Adam Malima, wamefail kabisa kabisa, ni teuzi za hovyo kabisa.
 
Katika historia hii hakuna waziri wa elimu aliyefanya madudu katika wizara hiyo kama yeye. Kwa kuwa hakuchukuliwa hatua yoyote wakati wa uvujaji wa mitihani, tatizo hilo la aibu linaendelea hadi leo!
 
Katika historia hii hakuna waziri wa elimu aliyefanya madudu katika wizara hiyo kama yeye. Kwa kuwa hakuchukuliwa hatua yoyote wakati wa uvujaji wa mitihani, tatizo hilo la aibu linaendelea hadi leo!

Sidhani kama anamzidi Mungai kwa kuharibu!
 
Si mnakumbuka wanamtandao walikuwa na kikosi kamili ,yaani first eleven na hawa wanaoitwa reserve,chini ya kepten wao mkuu Kikwete.Sasa kwa taarifa yako Kapuya alikuwa ndani ya first eleven hivyo ni lazima Kikwete alinde mkataba hata aboronge vipi Kikwete anabanwa na mkataba labda itokee watu kama wale wa kamati ya Richmond anaweza kuvunja mkataba kama alivyo lazimika kufanya kwa Lowasa.
 
Nimesikia kwamba aliweza kum-convince JK kwamba yeye ndiyo ilikuwa nguzo yake mkoani Tabora katika uhamasishaji wa wananchi kumpa kura mwaka 2005. Awali hii kazi ilikuwa ya Aden Rage alipewa na JK tangu 1995, lakini Kapouya ailijiingiza baadaye baada ya kutiwa gerezani Rage kulikochangiwa na fitina za Kapuya.
 
Inasemekana pia kule Mlingotini ndyo maskani kwake kila wikiendi.
 
...Kapuya bila aibu wala uzalendo yeye ndio aliyepigilia msumari wa mwisho juhudi za wafanyakazi wa Tanesco wakati walipojidhatiti kuikataa network solution. Walipotaka kumwaga ugali...akawajia na hotuba yake ya vitisho (nahisi Kikwete ameiga kwake) na wafanyakazi wale wakalegea.
Kilichofanywa na network solution, ni madudu matupu. Lakini Profesa Athuman Juma Kapuya bado anaendelea kutesa tu...
 
Nimesikia kwamba aliweza kum-convince JK kwamba yeye ndiyo ilikuwa nguzo yake mkoani Tabora katika uhamasishaji wa wananchi kumpa kura mwaka 2005. Awali hii kazi ilikuwa ya Aden Rage alipewa na JK tangu 1995, lakini Kapouya ailijiingiza baadaye baada ya kutiwa gerezani Rage kulikochangiwa na fitina za Kapuya.
Tushike lipi?mara kaoa nyumba moja na JK.MARA ALILIA SANA WAKATI WA MSIBA WA DR.OMAR ina maana alilia kuwa refarii wake kafariki,hapo hapo unauliza nani anambeba Professor Kapuya?mara anaonekana sana Mlingotini,jee huko Mlingotini ndio kuna mbeba?

nadhani nyinyi na huyu Mwandishi aliyeandika huko Mwanahalisi wote mnazua tu.Mara alimconvince JK kwenye Kampeni,mara Uprofessor na dini yake.vyote mnaongea ni pumba tupu.
 
kapuya kweli ni moja ya teuzi za hovyo katika nafasi za juu za siasa za kwetu tanzania, huyu kapuya anaungana na wanasiasa wa kariba ya sophia simba, karamagi, kingunge, adam malima, wamefail kabisa kabisa, ni teuzi za hovyo kabisa.

dada haitwi kapuya ni professor kapuya.mwandishi mzima unashindwa kuweka hiyo title?

simba,professor kapuya na malima hawajafeli.nenda jimboni kwa professor watu wake ndio watakwambia kama amefeli au laa,hizi hapa ni propaganda na uchaguzi.mwandishi mwenzio aliyeandika ameshindwa kufikisha ujumbe,

mara anamtaja dr.omar na kilio cha kapuya ina maana dr.omar ndio alikuwa refarii wake?kama alilia sana kwa refarii wake kufariki mbona anapeta?refarii wake ni elimu yake.nawe kasome uwe professional,vinginevyo utaendelea kuwa kanjanja tu.


 
dada haitwi kapuya ni professor kapuya.mwandishi mzima unashindwa kuweka hiyo title?

simba,professor kapuya na malima hawajafeli.nenda jimboni kwa professor watu wake ndio watakwambia kama amefeli au laa,hizi hapa ni propaganda na uchaguzi.mwandishi mwenzio aliyeandika ameshindwa kufikisha ujumbe,

mara anamtaja dr.omar na kilio cha kapuya ina maana dr.omar ndio alikuwa refarii wake?kama alilia sana kwa refarii wake kufariki mbona anapeta?refarii wake ni elimu yake.nawe kasome uwe professional,vinginevyo utaendelea kuwa kanjanja tu.



Soma vizuri rafiki yangu - hakuna mahala wachangiaji wamesema Prof Kapuya kafel ubunge. Kinachosemwa hapa ni kwamba kafeli uwaziri. Inawezekana kafanya vizuri jimboni mwake, lakini nahisi hiyo ni kutokana na kuwa waziri, tena katika wizara nono -- kama vile hii ya usitawi wa jamii ambayo mifuko yote ya hifadhi za jamiui (pension funds) iko chini yake. Tusisahau kwamba ile kashfa ya magodown ya Ubungo ilifanyika wakati yeye ndiyo waziri wa wizara hiyo.

Mimi nafikiri angekuwa ni mbunge tu bila ya uwaziri, asingeweza kufanya chochote jimboni kwake.
 
Back
Top Bottom