Nani analihujumu Taifa? Tusipozinduka sasa...

Tusipozinduka sasa, tutakuja kuamka na kukuta majirani wako dunia nyingine, Pamoja na hali ya siasa za ndani Uganda kuwa ni za kidikteta, Lakini taifa hilo linazidi kupiga hatua kubwa, Kupitia kiwanda chake cha Magari cha Kiira Motors LTD, Mwaka 2018 ilianza rasmi kuzalisha mabasi yanayotumia umeme jua.

Mradi huu sasa umekuwa mkubwa na kama unavyoona katika picha mabasi ya kiraia sasa yanazalishwa katika kiwanda hicho kwa wingi sana.

Ikumbukwe kwamba Tanganyika ilikuwa na kiwanda kikubwa cha kuzalisha magari kabla ya uhuru pale Keko Chang'ombe kiwanda hicho kilikuwa maalumu kuzalisha magari aina ya Land Rover, na baada ya Uhuru sera za ujamaa zilikiondoa kiwands hicho na waingereza wakarudi nacho kwao,

Baada ya Ujamaa kukolea Tanzania tulijengewa kiwanda kingine kule Kibaha kinachoitwa Nyumbu, (Lokomotiv), kwakutumia teknolojia ya Moscow tukafua vyuma na kuunda magari, lakini sera zetu za undumilakuwili yaani leo unakula soseji Moscow, kesho unakula siagi Washington, zilisababisha kiwanda kufa. Japo juzi kimerudi kianiaina.

Niliwahi kueleza katika Kitabu cha Ujasusi kwamba kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii linatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya makataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badi ingekusanya gawio toka kwa chombo kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake. Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai.

Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha iliutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa.

Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi kusitisha, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5, hii ni Bandari inayotajwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania la kutaka kujenga vinu vya kuchenjulia madini sasa imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Unaweza kufikiria, juzi tu kampuni kubwa dunia ya Microsoft imefungua kituo chake Nairobi Kenya kwa Afrika, Hiki ni kituo muhimu ambacho tungekipata kingesaidia sana ulinzi wa nchi kimtandao, kingetoa ajira kubwa kwa watu wetu, na kingelipa kodi kubwa na kusaidia uchumi wetu. Lakini masikini Tanzania, tuko na watu akina Kingai, Siro, Mahita, Urio nk wakufanana nao ambao ni mabingwa wa kubambika kesi za kigaidi wapinzani. Ilimradi wawafurahishe watawala.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Nimejitahidi kueleza Katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kwamba, Ujasusi wa Kiuchumi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo kwa Tanzania basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za Ujasusi wa Kiuchumi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive Navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya Navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker Junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa kifikra na Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers".

Ujasusi kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa ya sasa ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado "unaiserve CCM kwanza" kisha ndio Taifa linatafsiriwa liko salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm.

Kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Ujasusi wa kidola wa kulinda serikali na chama tawala limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, hii haikubaliki.

Tunahitaji mabadiliko makubwa ya lazima na ya haraka sana, mfumo wa Idara ya Usalama wa Taifa na Mfumo mzima wa Ulinzi na Usalama, Dunia haijasimama inasonga mbele, taifahaliwezi kushinda na majirani zetu ikiwa mfumo wa Usalama wa taifa bado uko kwenye usingizi wa Ujamaa, Mfumo ambao roho yake iko kwenye siasa za vyama hauwezi kulisaidia taifa kushindana kiuchumi.

View attachment 2167722View attachment 2167723View attachment 2167724View attachment 2167725
Hii story yako Wala sijaielewa,unapigia kampeni kitabu chako Cha "ujasusi"au unaeleza tatizo la kiuchumi la TZ na sababu zake?wewe hujawahi kuwa jasusi,hata ufahamu wako na masimulizi are like any normal next guy,ni yakawaida sana,sie tunaosoma novel za ujasusi kutoka kwa waandishi mahili duniani,wewe Bado ni bwana mdogo,
 
Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.
Wako busy na kesi za 'michongo' muda wa kuwaza vitu vyenye maslahi mapana kwa Taifa hawana!
 
Tupigane tutengane ili tuje tuungane kwa masharti. Naona Tanzania ni kubwa.

Hakuna katiba inayounganisha mchaga na mpare, mnyakyusa na msafa , mnyiramba na mnyaturu wala mkurya na mjita.

Tukitengana tutaelewana.

Wataalam wetu hawapewi nafasi badala yake wanapeana kwa kujuana.

Wataalamu wengine wanaamua kuwa chawa ili wateuliwe.

Wakiteuliwa ni kusifia tu hata kibaya.

Ovyo sana
 
Niwaombeni linapokuja suala la utaifa na maendelelo Basi tuwe wamoja na tunakuwaje wamoja?

Tunaezapingana kwa hoja na bado tukawa kitu kimoja sababu wazo lako tofauti na langu ndio yatakayoonesha uimara wa Jambo letu Ila sehemu moja sana tunakosea pale tunapoleta Mambo ya serikali ya ccm au waulize chadema hapo ndipo tunajitoa kwenye reli yetu ya maendelelo sisi wenyewe.

Wote tunajua jinsi CCM na chadema walivyo hodari hvyo havinahaja yakuongea au kuviunganisha kwa lolote lile kwenye Mambo ya kujenga hapo n dhahiri hoja zetu zitakuwa hazina maana kabisa.

Nchi hii haitajengwa na CCM wala chadema hata chama chochote Cha siasa Bali Ni watanzania wenyewe wenye uthubuti
 
Aliyepita alidai soon tutakuwa Dona kantri..

Hii nchi mfumo wake ulivo ni Werevu wanaongozwa na wajinga....

Hata hvyo tunaowaona warevu huku uraiani, wakipata madaraka automatically wanakuwa wajinga fulani hvi eg, Maprofesa wa Majalalani.

Hii nchi inatakiwa reform kubwa sana,, Viongozi 24/7 wao wanawaza madaraka tu na siasa,,mipango ya maendeleo sio kipaumbele kabisa.
 
Nakushukuru kwa uandishi yakinifu YERICKO NYERERE tatizo ni mazingira kwa siasa zetu mwanachadema kamwe hawezi kukubali mwanaccm kama yuko sahihi; Sera za nchi yetu hasahasa kuhusu uchumi zilishapitwa na wakati; watu walishaacha kufanya mambo yaende kwa sababu ya mwanasiasa bali kuna bodi za kichumi zinazong'amua mambo na kufanya nchi ziwe imara. UPINZANI Uko kupondea mambo yote ya serikali na kufikia kuchukiwa na wananchi tofauti na miaka ya 2010s wananchi waliwaamini sana upinzani. Kujuana na kupeana nyadhifa kindugu bila kuangalia uwezo nayo ni sababu inayoididimiza nchi yetu
 
Rais Samia anapambana kufufua mradi wa Bagamoyo na LPG ya Lindi lakini unajifanya hujui kwamba Chadomo kwa kushirikiana na Sukuma gang wanafanya kila mbinu Ili kukwamisha kwa visingizio vya kijinga lakini ukweli ni kwamba hawataki mama amfunike yule shujaa wao wa Afrika..

Mchawi mbongo mwenyewe.
wafuasi was shujaa,Wana nongwa Sana [emoji56]yaani hawapendi kufunikwa,,kipindi kile Mtu ukija juu tu iwe ki Mali,kisiasa ilikua lazima utulizwe,walitakiwakuinuka matajiri was lake zone TU,akina mYanga,,kina manji wakanyooshwa,,
saa hii tena hawataki Mtu yeyote amzidi sif shujaa,,
 
Kweli sikio la kufa halisikii dawa.Tulikuwa na Mangula Mechanical Tools (MMT)ilikuwa karakana kubwa kuliko zote kusini mwa jangwa la Sahara iliojengwa na China ya Mao.Ilikuwa na uwezo wa kuunda hata kifaru cha jeshi tokea kwenye udongo wa chuma hadi finishing.
Kwa ujinga wetu tuliuza na hakuna kitu tena pale.
Si hiyo tu karakana kubwa zilizokuwa UFI,TAZARA,URAFIKI,zimetekezwa.
Nchi yetu iliokuwa na nyenzo za kukuza uchumi wa viwanda imebakia kuwa nchi ya wafokaji wa musiki kizazi kipya.
R.I.P Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Baba wa Taifa.
impossible,kifaru kina components nyingi Dana hatuwezi unda,
enzi hizo unakuta wilaya nzima,Ina magari matano,,hii katakana ilikuwa inaunda Nini?
nchi nzima unakuta Ina mabasi 15[emoji23]
 
Viwanda vingine kama mwatex, mutex, Tanganyika packers, bora shoes, kiwanda cha magunia Moro , machine tools, general tyres, sunguratex, doublecola, minjingu stamico, to mention the few kweli R.I.P Mwalimu !
mwatex walikia wanatengeneza kanga mashuka na vitambaa Vya suruali,,
havikutengeza finishing products kama,magauni,jeans,chupi,t-shirt etc,,,(poor management)
 
Huyo Yericko Nyerere ni kada mkubwa wa Chadema.
Wewe uko nyuma na hujui ya kule mbele kwenye Dash board ya gari letu.

Ni kawaida ya Chadema kusema angalieni majirani....

Kwani uongo???
Kwani ni Uongo kwamba majirani zetu wanatupita?!!
 
Ukimkuta mwandishi huyu anaipamba Urusi na kufurahia mauwaji ya innocent people ndio utaujuwa undumilakuwili wa Watanzania.
Huyu mwandishi ni bonge la jasusi aise

Ova
 
Nilidhani watu watajikita kujadili, kupinga au kukubaliana na hoja kwa mantiki

Tatizo la vijana wetu mijadala ni kama 'sumu' , kwa maana hiyo wakikuatana na vijana wa nchi za jirani wakwetu wanasubiri '' kutetewa ajira na serikali''. Vijana wabadilke, jibu hoja , jenga hoja

Yericko Nyerere ana hoja nzuri sana, kwamba, sisi kama Taifa tumekosa dira na hatuwezi ushindani katika dunia ya 'uchumi' na si ya maderaya na makombora.

Miaka 20 iliyopita, tulikuwa na 'maisha bora kwa kila Mtanzania''.
Tukawa na 'elimu kwanza ' halafu 'kilimo kwanza' , ghafla tukawa na ''Viwanda''.

Nani anaweza kutueleza tathmini ya sera hizo, zimefaulu wapi na zimeshindwa wapi?

Pili, tukiwa na 'arable land' tumezungukwa na maji na mito, kwanini Tanzania isiwe kituo kikubwa cha ''FAO' na Mazao ya biashara kama Kahawa, Chai, Tangawizi, Dengu , Mbaazi n.k.

Kwanini hatuwezi kuwawezesha watu wetu kulima Dengu na Mbaazi tukilenga soko la watu Bilioni 1 India? Kwanini hatuwezi kutumia bahari na maziwa kuuza samaki nchi za 'EAC na SADCC'

Kwanini kiwanda cha TANELEC au Sahara vilivyozalisha bidhaa bora sana vilikufa na sasa tunaagiza bidhaa hizo hizo hafifu kutoka China.

Kwanini Gneral Tyre iliyokuwa na matairi bora viwango vya dunia ilikufa sasa tunaagiza mitumba !

Orodha inaendelea, lakini ukitaka kujua tatizo lipo wapi angalia hili

Rais JK alisaini Mradi wa Bagamayo . JK ni mwana CCM , katika baraza lake alikuwepo JPM.

Mwezi mmoja tu baada ya JPM kuingia madarakani, mradi wa Bagamoyo ukafutwa kwasababu 'eti hatutakusanya kodi''. Anayetuambia hayo ni rAIS JPM Waziri wa Rais JK

Katika mazingira ya kawaida wawili hawa wangekutana na tungekuwa na kauli moja.

Hivi Bagamoyo kama sera ya CCM na Marais ni wa CCM mkanganyiko unatoka wapi?

Watu wanadhani tatizo ni CCM, la hasha! Chadema wakichukua madaraka yatatokea haya haya.

Tatizo letu ni mfumo usioruhusu kufikiri sawa sawa, mfumo usioruhusu fikra mbadala , mfumo wenye taasisi zisizojua majukumu, mfumo usiozawadia ubunifu bali siasa.

Tuandike utaratibu utakaotuwajibisha na kujenga mifumo sawa sawa , KATIBA

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Uchama ni kama udini tu, hautatupeleka popote...inabidi tuwe na katiba inayoweka uchama pembeni na badala yake inasimamia maslahi mapana ya nchi...bila ya hivo hatutatoboa...
Mtu akiongea kitu kuhusu maendeleo ya nchi watu wanaingizia Uchadema Uccm hatar sana hii tabia sijui itaachwa lini
 
Yericko Nyerere.

Kazi yenu kubwa chadema ni kusifia nchi jirani bila Tafakuri.
Mkiamini katika nyinyi pekee kuyaona maono hayo.

Na kudharau wasio upamde wenu ki itikadi.

Umeisifia sana Msumbiji ya Philipo Nyusi iliyojaza majasusi Dunia nzima ila imeshindwa kupigana na kundi la Islamic state walioivamia na kulikalia jimbo la Cabo Delgado.

Nchi yenye majasusi Duniani kote ila imeshindwa kulinda uwekezaji mkubwa wa uchimbaji gesi uliowekezwa nchini kwake.

Nchi yenye majasusi kote duniani lakini imepigwa na magaidi hadi ikaomba msaada wa nchi ndogo ya Rwanda ili kujiokoa.

Umeisifia Rwanda kwa kujenga kiwanda cha uchenjuaji madini wakati haina madini yoyote ardhini kwake.

Ila hukutaka kuutumia ujasusi wako kueleza kwamba kiini cha machafuko nchini Congo DRC.

Ni kwa sababu Rwanda inatumika na mataifa makubwa ya nje ili kupora madini ya Congo DRC!.

Umeshindwa kutumia ujasusi wako kutueleza kiini cha majeshi ya kulinda amani nchini Congo DRC (Monusco).

Yamekuwa yakijiingiza kwenye utoroshaji wa madini ya nchi hiyo kwa miongo kadhaa,badala ya kutimiza wajibu wao uliowapeleka huko.

Pia umesifia majasusi wa Kagame walivyojaa Dunia nzima.
Lakini hukutwambia jinsi anavyowatumia kuwaua political opponents wake pamoja na kuwateka popote pale Duniani.

Huku hao mabingwa wa Demokrasia wa Dunia wakikaa kimya.
Sababu ya kutotaka kumuudhi mtoto wao Kagame anayewasaidia kuiba raslimali za Congo DRC!

Umeisifia Uganda kwa uwekezaji mkubwa ilioufanya kwa kuanza kutengeneza magari yenye teknolojia ya Solar nk.

Lakini umesahau kutuambia ni kwa nini waganda hao hao wanavyomkataa museveni kwa ukiukaji mkubwa wa Demokrasia nchini mwake huku mataifa hayo makubwa yakifumbia macho.

Tofauti na wanavyotupigia kelele sisi Tanzania kwa mambo ambayo kimsingi ni madogo kabisa kulinganisha na kinachotokea Rwanda na Uganda.

Umesifia Kenya kwa kuikaribisha Microsoft kuwekeza nchini humo,lakini hujatuwekea mfano hata mmoja wa faida ilizozipata Kenya kwa kuwa mnufaika mkuu wa uwekezaji huo.

Umesifia uwekezaji uliokuwa umepangwa wa Bandari ya Bagamoyo na ukasitishwa na Magufuli kwa sababu ambazo umeziita za kipuuzi.

Sasa ebu tumia Ujasusi wako mkubwa kwa sasa na umshawishi mama Samia aulete Bungeni huo mkataba ujadiliwe kipengele kwa kipengele na ikibidi wananchi tuupigie kura kabla ya kuingizwa mkenge kama tulivyofanywa kwenye Gesi na Mafuta.

Niishie kukupa taarifa kwamba,hata Magufuli aliona mbali kuhusu madini yetu na ndio maana aliamua kujenga masoko ya madini nchi nzima nahivyo kuondoa urasimu katika sekta ya wachimbaji wadogo wadogo wamadini..

Ili wananchi wauze madini kwa kulipa kodi halali na kwa bei halali ya Soko huku akiondoa utoroshaji wa madini kwenda nchi kama Rwanda na Kenya uliokuwa umekithiri.
Kwa kupitia walanguzi haramu wa Madini nchini kwa ushirika na mtandao wa nje.

Pia Magufuli aliona mbali kwa kuanza kujenga hizo refineries sehemu mbalimbali nchini na baadhi tayari zinafanya kazi.
Ikiwemo mojawapo kubwa iliyoko mwanza na inachenjuwa dhahabu kwa kwenda mbele.

Pia umesahau kutumia ujasusi wako kutufahamisha kwamba Angola inafanyauwekezaji mkubwa.

Katika jimbo la Cabinda kwa kutumia bandari ya Lobito,wanajenga reli ya kisasa ambayo itakuja mpaka kusini mwa Congo DRC.

commonmwananchi
10101.
hapa umemaliza kila kitu. Safi sana.
 
Hicho kinachoitwa ujasusi wa kiuchumi kilikuwa kipindi cha enzi za ujamaa

Kwa sasa ni somo tu la kawaida ambalo liko kwenye somo la marketing kipengele cha competitive strategy sokoni kupitia makert and product research na Unamshindaje competitor wako sokoni kupitia research zako za sokoni , ila Yeriko kalibatiza ujasusi wa kiuchumi!! Wote mliosoma makert strategy kwenye somo la Marketing hoja ya ujasusi wa kiuchumi ya Yeriko Nyerere mtaiona ya kitoto mno

Ni somo tu la makerting
 
Yericko Nyerere kajenga hoja zake, zinaweza kuwa sahihi au potofu
Hoja si nini au nani amesoma nini, hoja zake zipo wazi. Tafadhali zibomoe kwa hoja , zijibu kwa hoja
 
Yericko Nyerere.

Kazi yenu kubwa chadema ni kusifia nchi jirani bila Tafakuri.
Mkiamini katika nyinyi pekee kuyaona maono hayo.

Na kudharau wasio upamde wenu ki itikadi.

Umeisifia sana Msumbiji ya Philipo Nyusi iliyojaza majasusi Dunia nzima ila imeshindwa kupigana na kundi la Islamic state walioivamia na kulikalia jimbo la Cabo Delgado.

Nchi yenye majasusi Duniani kote ila imeshindwa kulinda uwekezaji mkubwa wa uchimbaji gesi uliowekezwa nchini kwake.

Nchi yenye majasusi kote duniani lakini imepigwa na magaidi hadi ikaomba msaada wa nchi ndogo ya Rwanda ili kujiokoa.

Umeisifia Rwanda kwa kujenga kiwanda cha uchenjuaji madini wakati haina madini yoyote ardhini kwake.

Ila hukutaka kuutumia ujasusi wako kueleza kwamba kiini cha machafuko nchini Congo DRC.

Ni kwa sababu Rwanda inatumika na mataifa makubwa ya nje ili kupora madini ya Congo DRC!.

Umeshindwa kutumia ujasusi wako kutueleza kiini cha majeshi ya kulinda amani nchini Congo DRC (Monusco).

Yamekuwa yakijiingiza kwenye utoroshaji wa madini ya nchi hiyo kwa miongo kadhaa,badala ya kutimiza wajibu wao uliowapeleka huko.

Pia umesifia majasusi wa Kagame walivyojaa Dunia nzima.
Lakini hukutwambia jinsi anavyowatumia kuwaua political opponents wake pamoja na kuwateka popote pale Duniani.

Huku hao mabingwa wa Demokrasia wa Dunia wakikaa kimya.
Sababu ya kutotaka kumuudhi mtoto wao Kagame anayewasaidia kuiba raslimali za Congo DRC!

Umeisifia Uganda kwa uwekezaji mkubwa ilioufanya kwa kuanza kutengeneza magari yenye teknolojia ya Solar nk.

Lakini umesahau kutuambia ni kwa nini waganda hao hao wanavyomkataa museveni kwa ukiukaji mkubwa wa Demokrasia nchini mwake huku mataifa hayo makubwa yakifumbia macho.

Tofauti na wanavyotupigia kelele sisi Tanzania kwa mambo ambayo kimsingi ni madogo kabisa kulinganisha na kinachotokea Rwanda na Uganda.

Umesifia Kenya kwa kuikaribisha Microsoft kuwekeza nchini humo,lakini hujatuwekea mfano hata mmoja wa faida ilizozipata Kenya kwa kuwa mnufaika mkuu wa uwekezaji huo.

Umesifia uwekezaji uliokuwa umepangwa wa Bandari ya Bagamoyo na ukasitishwa na Magufuli kwa sababu ambazo umeziita za kipuuzi.

Sasa ebu tumia Ujasusi wako mkubwa kwa sasa na umshawishi mama Samia aulete Bungeni huo mkataba ujadiliwe kipengele kwa kipengele na ikibidi wananchi tuupigie kura kabla ya kuingizwa mkenge kama tulivyofanywa kwenye Gesi na Mafuta.

Niishie kukupa taarifa kwamba,hata Magufuli aliona mbali kuhusu madini yetu na ndio maana aliamua kujenga masoko ya madini nchi nzima nahivyo kuondoa urasimu katika sekta ya wachimbaji wadogo wadogo wamadini..

Ili wananchi wauze madini kwa kulipa kodi halali na kwa bei halali ya Soko huku akiondoa utoroshaji wa madini kwenda nchi kama Rwanda na Kenya uliokuwa umekithiri.
Kwa kupitia walanguzi haramu wa Madini nchini kwa ushirika na mtandao wa nje.

Pia Magufuli aliona mbali kwa kuanza kujenga hizo refineries sehemu mbalimbali nchini na baadhi tayari zinafanya kazi.
Ikiwemo mojawapo kubwa iliyoko mwanza na inachenjuwa dhahabu kwa kwenda mbele.

Pia umesahau kutumia ujasusi wako kutufahamisha kwamba Angola inafanyauwekezaji mkubwa.

Katika jimbo la Cabinda kwa kutumia bandari ya Lobito,wanajenga reli ya kisasa ambayo itakuja mpaka kusini mwa Congo DRC.

commonmwananchi
10101.
Mkuu voicer naunga mkono hoja zako zote kasoro pale ulipoanza kumtaja Magufuli. Utanisamehe kwa hilo. Magufuli ndiye aliyekwamisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa kuwa tu mkataba umesainiwa na Kikwete na siyo kwa ubaya wa mkataba
 
mwatex walikia wanatengeneza kanga mashuka na vitambaa Vya suruali,,
havikutengeza finishing products kama,magauni,jeans,chupi,t-shirt etc,,,(poor management)
Ilitakiwa viboreshwe sio kuviua au kuvitupa kama ilivyofanyika, neno kubinafsisha ilikuwa ni sawa na kuvitupilia mbali !! Hata yeye hayati Mkapa alikuja kukiri kwamba alifanya kosa kubwa kuvibinafsisha !!
 
Tusipozinduka sasa, tutakuja kuamka na kukuta majirani wako dunia nyingine, Pamoja na hali ya siasa za ndani Uganda kuwa ni za kidikteta, Lakini taifa hilo linazidi kupiga hatua kubwa, Kupitia kiwanda chake cha Magari cha Kiira Motors LTD, Mwaka 2018 ilianza rasmi kuzalisha mabasi yanayotumia umeme jua.

Mradi huu sasa umekuwa mkubwa na kama unavyoona katika picha mabasi ya kiraia sasa yanazalishwa katika kiwanda hicho kwa wingi sana.

Ikumbukwe kwamba Tanganyika ilikuwa na kiwanda kikubwa cha kuzalisha magari kabla ya uhuru pale Keko Chang'ombe kiwanda hicho kilikuwa maalumu kuzalisha magari aina ya Land Rover, na baada ya Uhuru sera za ujamaa zilikiondoa kiwands hicho na waingereza wakarudi nacho kwao,

Baada ya Ujamaa kukolea Tanzania tulijengewa kiwanda kingine kule Kibaha kinachoitwa Nyumbu, (Lokomotiv), kwakutumia teknolojia ya Moscow tukafua vyuma na kuunda magari, lakini sera zetu za undumilakuwili yaani leo unakula soseji Moscow, kesho unakula siagi Washington, zilisababisha kiwanda kufa. Japo juzi kimerudi kianiaina.

Niliwahi kueleza katika Kitabu cha Ujasusi kwamba kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii linatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya makataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badi ingekusanya gawio toka kwa chombo kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake. Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai.

Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha iliutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa.

Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi kusitisha, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5, hii ni Bandari inayotajwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania la kutaka kujenga vinu vya kuchenjulia madini sasa imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Unaweza kufikiria, juzi tu kampuni kubwa dunia ya Microsoft imefungua kituo chake Nairobi Kenya kwa Afrika, Hiki ni kituo muhimu ambacho tungekipata kingesaidia sana ulinzi wa nchi kimtandao, kingetoa ajira kubwa kwa watu wetu, na kingelipa kodi kubwa na kusaidia uchumi wetu. Lakini masikini Tanzania, tuko na watu akina Kingai, Siro, Mahita, Urio nk wakufanana nao ambao ni mabingwa wa kubambika kesi za kigaidi wapinzani. Ilimradi wawafurahishe watawala.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Nimejitahidi kueleza Katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kwamba, Ujasusi wa Kiuchumi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo kwa Tanzania basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za Ujasusi wa Kiuchumi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive Navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya Navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker Junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa kifikra na Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers".

Ujasusi kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa ya sasa ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado "unaiserve CCM kwanza" kisha ndio Taifa linatafsiriwa liko salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm.

Kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Ujasusi wa kidola wa kulinda serikali na chama tawala limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, hii haikubaliki.

Tunahitaji mabadiliko makubwa ya lazima na ya haraka sana, mfumo wa Idara ya Usalama wa Taifa na Mfumo mzima wa Ulinzi na Usalama, Dunia haijasimama inasonga mbele, taifahaliwezi kushinda na majirani zetu ikiwa mfumo wa Usalama wa taifa bado uko kwenye usingizi wa Ujamaa, Mfumo ambao roho yake iko kwenye siasa za vyama hauwezi kulisaidia taifa kushindana kiuchumi.

View attachment 2167722View attachment 2167723View attachment 2167724View attachment 2167725
Kama umeamua kuwa mchambuzi basi tumia SWOC katika kujadili kwako. Mijadala ya kuelezea weaknesses tu inakuwa biased. Ikiwa biased basi inakuexpose wewe Yeriko uonekane;
1. Unachambua kichadema
2. Unachambua kuuza kitabu chako.
Kuna strengths za Tanzania na kuna challenges.
Usiandike kama vile ni Taifa lilofeli au ambalo halijawahi kufanikiwa katika sera yoyote au kana kwamba hayo mataifa mengine hayajawahi kufeli mahali.
 
Back
Top Bottom