Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
...mimi ni mkazi wa kijiji cha Kinyerezi, nimezungukwa na high profiles politicains wa zamani na wa sasa ninawaona waliokuwa wazuri na wabovu kwa sababu you can tell kutokana na life style zao, mmoja wa majirani zangu wa karibu sana ni Mzee Apiyo na Mahita, you can tell kwamba Mzee apiyo alikuwa ni kiongozi safi, masikini ya Mungu hana kitu kabisaa, lakini ninawangalia majirani zangu wengine kama Mahita.
...sasa hatuwezi kuwatukana viongozi wetu wote kwa sababu ya wezi wachache
Kwamba kiongozi ambae hakuiba ndio kiongozi safi hilo sidhani ni kweli. Kutokuiba, unategemewa usiibe, si sifa. Kutokuiba yabidi kuwe the least common denominator. Zaidi ya maadili, tupime viongozi kwa ufanisi, maono uzoefu, matokeo, fikra, kujitoa katika utumishi, na uchochezi chanya, na pia kutovumilia maovu. Field Marshall ni muadilifu, msafi, sawa, je alifanya nini alipoona uchafu? Ana balls za kukemea maovu?
Na uadilifu wenyewe tusiupime kwa kuangalia "life styles" za wastaafu. Hao unaosema majirani zako wastaafu wasafi wa Kinyerezi, wametangaza mali zao zote Tume ya Maadili? Ni vigumu kujua. Utawezaje kujua mali na vipato vya Kingozi wa Tanzania wakati hata mshahara wa Rais ni siri kali ya serikali?