Nani anaifadhili CHADEMA?

Nani anaifadhili CHADEMA?

Mi najiuliza ni vyama vyote vimeruhusiwa kufanya siasa au ni CHADEMA tu? Maana sioni wengine wakichangamkia fulsa
 
Mkuu Resilience , tuko baadhi yetu tunamjua mfadhili mkuu wa Chadema, kwa vile wenyewe hawamtaji na mfadhili mwenyewe ni muungwana sio mtu wa kujitapa, naomba na mimi nisimtaje.

Hapa nimemdokeza https://www.jamiiforums.com/threads...-zaidi-ya-mshambuliaji.2059203/#post-45063875

Na hapa nimefafanua https://www.jamiiforums.com/threads...li-na-watanzania.1702195/page-6#post-45066996
But you have to connect the dots!.

P
CDM ni taasisi kubwa. Acha propaganda.
 
CDM ni taasisi kubwa. Acha propaganda.
Hilo halina ubishi na tumelisema toka ile 2010, tatizo ni hawajajipanga. https://www.jamiiforums.com/threads/ccm-imechokwa-chadema-haijajipanga.87532/
Wanabodi,
.
Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja yenye impact ikiwemo kuyashika majiji makubwa katika mikoa the big five!, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga mkao wa kichama tawala, ili kikabidhiwe nchi, kitawale, Chadema bado kimekaa kichama harakati, hivyo kuna wengi wanakiona kama bado hakijakomaa kiasi cha kukabidhiwa ikulu yetu!.

Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu kwa sasa japo kipo juu, lakini bado hamjakomaa kufikia kiwango cha kukabidhiwa nchi, bado mko kiuana harakati zaidi kuliko ki chama tawala, na hamjajipanga kwa sura ya kitaifa na utayari wa kutawala nchi.

Kwa upande wa Chadema, lazima kibadilike, first and foremost, anzeni na Mwenyekiti wenu Freeman Mbowe, he should go!. Ajiuzulu uenyekiti, ampishe more able person kama Dr. Slaa kwenye usukani wa chama, Katibu Mkuu mpeni Zitto strategically, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, na kulivua lile koti la ukanda na ukabila ili walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura 2015 kwa kujionyesha Chadema ni chama cha wote, dini zote na kanda zote.

Kupumzishwa kwa Freeman Mbowe sio kuwa hafai no, anafaa sana lakini kwa background yake na nature ya kazi zake, as a businessman, hapo alipoifikisha Chadema amaishafanya kazi kubwa na kufikia mwisho wa uwezo wake. Kwa background yake ya a former DJ na sasa ni mfanyabiashara, focus ya wafanyabiashara kote dunia nzima ni maximisation of profits, hivyo Mbowe atahitaji ruzuku ya Chadema itumike kuivest kwenye assets, kwenye vitu vya kuonekanika yaani assets kama magari, mavazi, etc

Ili Chadema kiweze kushika nchi 2015, it has to invest on people na sio ku invest kwenye vitu. Chadema must invest kwenye mass mobilisation na sio kutegemea mikutano ya hadhara na maandamano. Chadema needs to have able people kuiwezesha kushika dola five years to come kwa kutumia reaching out mechanism kuwafikia the mases kwa kumiliki media yake yenyewe. Chadema lazima ifanye recruitment ya loyal able people, watakaokuja kuendesha serikali ya Chadema. Mbowe hawezi kukubali ruzuku ya Chadema itumike to invest on people, kwasabu it's a loss making venture kwa mfanyabiashara na kuivest kwenye mass media sio profitable investment kwa business man ambaye ni in for profits making!. Dr.Slaa na Zitto sio wafanyabiashara hawa ni ma technocrats. Chama kishikwe na wanasiasa watendaji ma technocrats na sio wanasiasa wafanyabiashara!. Chadema iwekeze kwenye watu na kupanua mtandao wake hadi vijijini, ili kwenda kuiongoa CCM kuanzia kule chini kabisa kwenye mizizi yake ambako ni kule kwenye mashina. Chadema imiliki media yake yenyeshe for mass mobilization na sio kutegemea mikutano na maandamano, huko ni kuendeleza uanaharakati, Chadema inatakiwa kukaa mkao wa kutawala, ikitangaza kitu, kinafika Tanzania nzima!

Chadema ina tatizo la umimi. Kitendo cha Chadema kuihodhi kambi rasmi ya upinzani Bungeni, huu ni udhaifu mkubwa ambao hautawafikisha mbali. Pamoja na kanuni za Bunge kuruhusu Chadema kuunda kambi rasmi ya upinzani peke yake, Chadema peke yenu hamuwezi!. Lazima muwashirikishe wapinzani wengine wote hata kama hawastahili. You have to unite and work as one against a common enemy. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

Kama CCM ndio hii iko ICU na Chadema haijajipanga, spika ndio huyo mama ma over confidence na over reaction, 2015 tutegemee nini?. Kama Chadema haitabadilika, then 2015, japo imechokwa, japo chovu, ni CCM tena!.

Angalizo: Paskali wa Jamii Forums ni political commentator ambaye yuko objective, bila kuegemea chama chochote, upande wowote na hufanya kazi kwa wote, ila ni muumini wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge for the balance of power, hivyo nashangilia sana kambi ya upinzani kuingiza vichwa 100 bungeni, ni matumaini yangu, 2015 kazi itakamilishwa!.

Paskali
P
 
Hata wewe ni mfadhili,Samia,majaliwa wote ni wafadhili CDM indirectly
 
Mkuu Resilience , tuko baadhi yetu tunamjua mfadhili mkuu wa Chadema, kwa vile wenyewe hawamtaji na mfadhili mwenyewe ni muungwana sio mtu wa kujitapa, naomba na mimi nisimtaje.

Hapa nimemdokeza https://www.jamiiforums.com/threads...-zaidi-ya-mshambuliaji.2059203/#post-45063875

Na hapa nimefafanua https://www.jamiiforums.com/threads...li-na-watanzania.1702195/page-6#post-45066996
But you have to connect the dots!.

P
Propaganda speculation aiming on damaging
 
Naona CHADEMA bila ruzuku bado kinafedha za kuandaa mikutano ya adhara, ufafhili wao upo chini ya nani? Mbona vyanzo vya mapato havipo wazi?
Watanzania wa kawaida tu ndio wafadhili wakubwa wa CHADEMA.
 
Back
Top Bottom