Nani anahitaji tiba?

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Messages
3,412
Points
1,225

Jaguar

JF-Expert Member
Joined Mar 6, 2011
3,412 1,225
Jamaa baada ya kutoa maelezo kwa daktari kuhusu matatizo ya mkewe kutokusikia vizuri,daktari alimshauri aende nyumbani,akajaribu kumsemesha kwa umbali tofauti tofauti mpaka pale atakapomjibu ili ijulikane ukubwa wa tatizo lake.Jamaa alipofika nyumbani,akaanzia mlangoni kwa kusema;"mke wangu,umepika nini leo?..(hakusikia jibu).Akasogea hadi sebuleni,akauliza tena;"mke wangu,umepika nini leo?..(bado hakusikia jibu).Akaingia hadi jikoni,akamkuta mkewe anapika,akamwuliza kwa mara ya tatu;"mke wangu,umepika nini leo?".Mke akajibu kwa hasira;"mume wangu mbona husikii?,sasa nakwambia mara ya tatu,nimepika ugali kwa samaki!".
 

Forum statistics

Threads 1,390,892
Members 528,285
Posts 34,065,503
Top