Nani anafaa kuwa Mrithi wa IGP Simon Sirro?

Nani anafaa kuwa Mrithi wa IGP Simon Sirro?

Sirro is among of the fewer professional police we have.
Sirro ni viwango vya Donald Rumsfeld aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Marekani 2001 hadi 2006.
Sirro hajawahi kushindwa kwenye kazi, waulize majambazi waliovamia watalii mbugani watakuambia Sirro ni nani.
Jiulize kwa miaka hii ya Sirro wale majambazi waliokuwa wakitamba wako wapi?
Sirro chapa kazi baba.


Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
Hao majambazi wataiba nini ilhal watu hawatembei na lundo la pesa siku hizi.Dunia imebadilika pakubwa sana kwenye sekta ya ulinzi wa fedha.sasa hivi kuibiwa lundo la fedha iwe kimtandao au cash ni uzembe.Na ata kama vitaporwa vitu vitauzwa wapi kwa namna mifumo ya kuuza na kununua ilivyokaa dunia ya leo.Vinginevyo labda waibe vibaka kukidhi mlo wa siku ila sio ujambazi mkubwa wakuingiza mamilion ya pesa.Tecnolojia imekua kwahiyo lazima ipunguze vitu visivyo na ulazima kufanyika.
 
Wewe huyu asistaafu asubiri kwanza kwenda The Hague abaki kwenye cheo chake hivyohivyo hatujamalizana nae , msianze kumkwepesha kijanja anahitajika Sana ICC .
Tumekusikia beberu Amsterdam, mtu wako anaendeleaje huko kwako na matibabu?
 
Apewe Muroto ndio anaweza kwenda sawa na awamu ya kishindo. Au apewe Sabaya amsaidie kuuwa upinzani.
 
Sirro mwaka wake wa kustaafu kisheria kabla hajaongezewa muda ni 2023

Ungesema Mabeyo hapo sawa lakini Mabeyo nae muda kutoka kustaafu ameongezewa na mwenye mamlaka
Mabeyo sijawah hata kumuelewa huyu mzee.
 
ICC inamngoja. Pemba alikwenda na akasema maneno yaliosababisha vifo vya watu 14. na wengine kupigwa na watoto wasichana wadogo wameharibiwa na wanawake kunajisiwa.

Ushahidi wa matukio upo na yeye ndiye mkuu wa jeshi la polisi waliotenda maafa hayo.
 
Hivi unajua kwamba jeshini kuna ngazi za uongozi (ranks)?

Huwezi kumpa Mambosasa u-IGP halafu uwaache makamishna na manaibu makamishna pale Makao Makuu.

Hilo likifanyika basi itabidi Mhe. Rais pia awaondoe viongozo wote ngazi za juu za Polisi ili tu kumpa uhalali Mambosasa awe IGP kitu ambacho sioni kama kinaweza kufanyika.

Hivyo mtu ambae naona ni candidate wa u-IGP baada ya Sirro ni Sabas ambae kwa sasa ni Kamishna wa Operesheni.
Ana mpandisha cheo na kumpa u IGP, kwani kwa Mabeyo ilikuaje? Walikuwepo ma senior wakarukwa.
 
Majeshi yote ya Tanzania yana miradi ya maendeleo ili kupunguza utegemezi kwa Serikali. Lakini kwa Miaka mitano ameshindwa kubuni miradi hata ya kuwasaidia Askari.
Mnawaonea sana polisi
Katika majeshi yote polisi hawatoshi,huwezi kumtoa polisi lindoni akafuge kuku,tofauti na magereza,wanafunga mageti wanakwenda kulima Tena wanachukua wafungwa Kama nguvu kazi
Hayo ma lugumi yametokea wizarani sio polisi
 
Salaam Wakuu salaam

Tumsaidie Rais Magufuli kutafuta Watendaji wenye Uchungu na Nchi Watetezi wa Wanyonge.

Kumbuka sisi Wanachama wa JamiiForums ndio tulimpendekeza Sirro kwa Rais na akateuliwa na katuangusha.


Ni Wakati wetu wa kumsaidia kupa mrithi wake.

Weka Wasifu na kwanini unadhani huyo ulomtaja anaweza kuvaa Viatu vya Sirro?

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro, ana mambo mazuri kafanya katika Nchi yetu. Lakini kila mtu ana madhaifu yake kama ilivyo kwa Sirro.

Ila kutokana na Hotuba rais aloitoa Wakati anamuapisha Waziri Mkuu Majaliwa, ni ukweli usio na Shaka kwamba lolote laweza kutokea kwa IGP Sirro.

Afande Sirro kwa hii miaka Mitano, alitakiwa awe amejiuzulu. Hata rais alimpa nafasi ya kujitafakari akashindwa.

Kuna Makosa ambayo Sirro kafeli kutimiza ambayo yamefaya nimuondolee alama.

1. Lissu kupigwa risasi na Watu Kutekwa na kupotea. Hii imechafua sana Nchi yetu. Hii hali ilimchafua hadi rais kwani Uzembe wa Sirro kufanyakazi, kumefanya watu wadhani kwamba Watekaji wanalindwa. Hii kosa alitakiwa ajiuzulu. Ila amshukuru rais alimvumilia.

2. Kuna Sakata la sare za Polisi. Rais Magufuli aliibua Sakata la sare za Polisi ambazo ulifanyika ufisadi wa karibia Bil 60, akamuagiza afanyie kazi, lakini hafanyi chochote. Alitakiwa ajiuzulu.

3. Sakata la Lugumi. Kuna ufisadi wakaribia Bilioni 34 za kifunga mitambo ya alama za Vidole ambalo liliibuliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

4. Majeshi yote ya Tanzania yana miradi ya maendeleo ili kupunguza utegemezi kwa Serikali. Lakini kwa Miaka mitano ameshindwa kubuni miradi hata ya kuwasaidia Askari.

NB: Sitaki kuzungumzia Rushwa, Uchakavu wa Ofisi za Polisi na Uchakavu wa sare za Polisi,kubambikia kesi nk.

Hata akiendelea kuliongoza jeshi la Polisi kwa upande wangu naona kakosa uhalali wa kuendelea kuwepo hapa alipo. Namuombea kila la heri katika maisha yake ya baadaye. Na tunashukuru kwa Mchango wange hasa wa kudhibiti Ujambazi Nchi.

Kwa Upande wangu bado nafuatilia CV ya Afande wa Taifa Fortunatus Muslimu ambaye amefanikiwa kudhibiti ajali barabarani. Tangu 2017 yeye yupo Field. Ni Askari Mcha Mungu, Mwenye Upendo, hekima na Msikivu. Nafuatilia CV yake. Sisi watu wa barabarani tunaona mchango wake. Madereva Walevi wameisha. Huwa hakai Ofisini..

Simon Nyakoro Sirro kabla ya kuwa IGP, alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa 10 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwisho wa makala hii tutawaorodhesha wengine waliomtangulia kushika wadhifa huo.

Sirro alizaliwa eneo la Kiabakari wilaya ya Butiama mkoani Mara mwaka 1963.

Kuhusu elimu yake, Simon Sirro alisoma Shule ya Sekondari ya Ilboru jijini Arusha na Tosamaganga kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu kusoma Shahada ya awali katika Sheria.

Sirro amesoma pia seminari (masomo ya upadri) na kufikia ngazi ya juu kabla ya kuacha na kujiunga na Jeshi la Polisi.
Kamanda Sirro alisema kuwa kama isingekuwa baba yake basi leo yeye angekuwa ni Padri wa Kanisa Katoliki kwani ndiyo ndoto yake kubwa, lakini baada ya wazazi wake kumkatisha ndipo alipojiunga na jeshi hilo.

Unajua wazazi kule kwetu Musoma walikuwa hawakuelewi usipooa. Mzazi aliona mimi ni kijana mkubwa akasema haiwezekani,” alisema Sirro alipofanya mahojiano na Mwananchi kipindi cha nyuma.

Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Kituo cha Polisi Buguruni mwaka 1998, Mkuu wa Upelelezi Tarafa ya Magomeni kwa miaka 5 na Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Tabora.

Mwaka 2002 alikuwa Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam akiwa ni msaidizi wa Abdallah Zombe.

Sirro ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam wa tatu ambapo aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli Februari 15 mwaka 2006 akichukua nafasi ya Suleiman Kova aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2008. Kabla ya Kova aliyekuwa akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni Alfred Tibaigana.

Wakati Suleiman Kova akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sirro alikuwa msadizi wake ambapo baadae alirithi mikoba yake.

Kabla ya kuongoza Kanda Maalum Dar es Salaam, Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Tanzania. Moja ya opersheni kubwa alizowahi kuongozi ni Operesheni Kimbunga dhidi ya wahamiaji haramu mwaka 2012.

Lakini pia, Simon Nyakoro Sirro amewahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Mikoa mbalimbali ambayo ni Tanga, Mwanza na Shinyanga.

Wakuu wengine wa Jeshi la Polisi ni;
1. Elangwa Shahidi (1964-1970), alistaafu.

2. Hamza Azizi (1972-1973), aling’olewa na Mwl. Nyerere kwa matumizi mabaya ya madaraka.

3. Samwel Pundugu (1973-1975).

4. Philemon Mgaya (1975-1980),
aliachishwa kazi kwa manufaa ya umma.

5. Solomoni Liani (1980-1984), alihitimisha kipindi cha mwisho cha Mwl. Nyerere.

6. Harun Mahundi (1984-1996), alistaafu.

7. Omari Mahita (1996-2006), alistaafu.

8. Said Mwema (2006-2013), alistaafu.

9. Ernest mangu (2013-2017), atapangiwa kazi nyingine, na

10. Simon Sirro (2017-2020) yupo madarakani.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Nyakoro Sirro ameoa mke mmoja na ana watoto wanne.
Bila ya shaka yoyote,ni wewe
 
Mkuu kwa huu mfumo mbovu ulivyo hata wakuteue wewe mwenyewe hakuna utakachofanya maana unatakiwa ufuate maelekezo ya jiwe na siyo kutumia weledi wako
 
Hao wote hakuna aliyekua na busara kumzidi Sirro.

Mtu hawezi kuamini kama 2010 Sirro akiwa RPC Mwanza aliagiza tume imtangaze mshindi mbunge wa upinzani Wenje na akatangazwa.

Ila angalia anachokifanya leo?huwezi kuamini.

Kile kiti hata uwe na busara vp ukishakaa tu busara zinaishia hapohapo.
Naunga mkono hoja, tuna katiba mbovu sn ambayo inamtambua mtu mmoja pekee
 
Ma IGP walionivutia,
Harun mahundi.
Samweli pundugu,huyu nilifika hadi kuhiji kaburini kwake,
Said mwema.
Ezekiel Mangu.
 
Back
Top Bottom