Nani anafaa kuwa Mrithi wa IGP Simon Sirro?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
1605869153530.png

Salaam Wakuu salaam

Tumsaidie Rais Magufuli kutafuta Watendaji wenye Uchungu na Nchi Watetezi wa Wanyonge.

Kumbuka sisi Wanachama wa JamiiForums ndio tulimpendekeza Sirro kwa Rais na akateuliwa na katuangusha.


Ni Wakati wetu wa kumsaidia kupa mrithi wake.

Weka Wasifu na kwanini unadhani huyo ulomtaja anaweza kuvaa Viatu vya Sirro?

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro, ana mambo mazuri kafanya katika Nchi yetu. Lakini kila mtu ana madhaifu yake kama ilivyo kwa Sirro.

Ila kutokana na Hotuba rais aloitoa Wakati anamuapisha Waziri Mkuu Majaliwa, ni ukweli usio na Shaka kwamba lolote laweza kutokea kwa IGP Sirro.

Afande Sirro kwa hii miaka Mitano, alitakiwa awe amejiuzulu. Hata rais alimpa nafasi ya kujitafakari akashindwa.

Kuna Makosa ambayo Sirro kafeli kutimiza ambayo yamefaya nimuondolee alama.

1. Lissu kupigwa risasi na Watu Kutekwa na kupotea. Hii imechafua sana Nchi yetu. Hii hali ilimchafua hadi rais kwani Uzembe wa Sirro kufanyakazi, kumefanya watu wadhani kwamba Watekaji wanalindwa. Hii kosa alitakiwa ajiuzulu. Ila amshukuru rais alimvumilia.

2. Kuna Sakata la sare za Polisi. Rais Magufuli aliibua Sakata la sare za Polisi ambazo ulifanyika ufisadi wa karibia Bil 60, akamuagiza afanyie kazi, lakini hafanyi chochote. Alitakiwa ajiuzulu.

3. Sakata la Lugumi. Kuna ufisadi wakaribia Bilioni 34 za kifunga mitambo ya alama za Vidole ambalo liliibuliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

4. Majeshi yote ya Tanzania yana miradi ya maendeleo ili kupunguza utegemezi kwa Serikali. Lakini kwa Miaka mitano ameshindwa kubuni miradi hata ya kuwasaidia Askari.

NB: Sitaki kuzungumzia Rushwa, Uchakavu wa Ofisi za Polisi na Uchakavu wa sare za Polisi,kubambikia kesi nk.

Hata akiendelea kuliongoza jeshi la Polisi kwa upande wangu naona kakosa uhalali wa kuendelea kuwepo hapa alipo. Namuombea kila la heri katika maisha yake ya baadaye. Na tunashukuru kwa Mchango wange hasa wa kudhibiti Ujambazi Nchi.

Kwa Upande wangu bado nafuatilia CV ya Afande wa Taifa Fortunatus Muslimu ambaye amefanikiwa kudhibiti ajali barabarani. Tangu 2017 yeye yupo Field. Ni Askari Mcha Mungu, Mwenye Upendo, hekima na Msikivu. Nafuatilia CV yake. Sisi watu wa barabarani tunaona mchango wake. Madereva Walevi wameisha. Huwa hakai Ofisini..

Simon Nyakoro Sirro kabla ya kuwa IGP, alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa 10 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwisho wa makala hii tutawaorodhesha wengine waliomtangulia kushika wadhifa huo.

Sirro alizaliwa eneo la Kiabakari wilaya ya Butiama mkoani Mara mwaka 1963.

Kuhusu elimu yake, Simon Sirro alisoma Shule ya Sekondari ya Ilboru jijini Arusha na Tosamaganga kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu kusoma Shahada ya awali katika Sheria.

Sirro amesoma pia seminari (masomo ya upadri) na kufikia ngazi ya juu kabla ya kuacha na kujiunga na Jeshi la Polisi.
Kamanda Sirro alisema kuwa kama isingekuwa baba yake basi leo yeye angekuwa ni Padri wa Kanisa Katoliki kwani ndiyo ndoto yake kubwa, lakini baada ya wazazi wake kumkatisha ndipo alipojiunga na jeshi hilo.

Unajua wazazi kule kwetu Musoma walikuwa hawakuelewi usipooa. Mzazi aliona mimi ni kijana mkubwa akasema haiwezekani,” alisema Sirro alipofanya mahojiano na Mwananchi kipindi cha nyuma.

Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Kituo cha Polisi Buguruni mwaka 1998, Mkuu wa Upelelezi Tarafa ya Magomeni kwa miaka 5 na Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Tabora.

Mwaka 2002 alikuwa Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam akiwa ni msaidizi wa Abdallah Zombe.

Sirro ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam wa tatu ambapo aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli Februari 15 mwaka 2006 akichukua nafasi ya Suleiman Kova aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2008. Kabla ya Kova aliyekuwa akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni Alfred Tibaigana.

Wakati Suleiman Kova akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sirro alikuwa msadizi wake ambapo baadae alirithi mikoba yake.

Kabla ya kuongoza Kanda Maalum Dar es Salaam, Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Tanzania. Moja ya opersheni kubwa alizowahi kuongozi ni Operesheni Kimbunga dhidi ya wahamiaji haramu mwaka 2012.

Lakini pia, Simon Nyakoro Sirro amewahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Mikoa mbalimbali ambayo ni Tanga, Mwanza na Shinyanga.

Wakuu wengine wa Jeshi la Polisi ni;
1. Elangwa Shahidi (1964-1970), alistaafu.

2. Hamza Azizi (1972-1973), aling’olewa na Mwl. Nyerere kwa matumizi mabaya ya madaraka.

3. Samwel Pundugu (1973-1975).

4. Philemon Mgaya (1975-1980),
aliachishwa kazi kwa manufaa ya umma.

5. Solomoni Liani (1980-1984), alihitimisha kipindi cha mwisho cha Mwl. Nyerere.

6. Harun Mahundi (1984-1996), alistaafu.

7. Omari Mahita (1996-2006), alistaafu.

8. Said Mwema (2006-2013), alistaafu.

9. Ernest mangu (2013-2017), atapangiwa kazi nyingine, na

10. Simon Sirro (2017-2020) yupo madarakani.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Nyakoro Sirro ameoa mke mmoja na ana watoto wanne.
 
Majibu ya hoja yako namba 4. Jeshi la polisi lina mradi mkubwa sana linaoufanya kwakushirikia na Tume ya uchaguzi. Mradi huo ni kuhakikisha CCM ngazi zote wanabaki madarakani na kuhakikisha wapinzani wote wanabambikiwa kesi ambazo hazina dhamana. Pia kuhakikisha wakosoaji wote wanaswekwa ndani na kupewa kesi ambazo hazina dhamana.
 
Serekali hii ya awamu ya 5 haina moral authority ya kuongelea vita dhidi ya ufisadi

1. Kukosa uwazi uendeshaji wa ATCL
2. Kukosa uwazi kwa mikataba ya Barrick, SGR & Stiegler's Gorge
3. Wabunge wa upinzani kughilibiwa (ikiwamo kumrejesha bungeni bila uchaguzi mbunge aliyehamia chama chengine)
4. Na mengine mengi kama haya
 
Kwasasa nawaona wawili tu wenye hekima za kutosha kuongoza jeshi la polisi
1. Salum Rashid Hamdini (RPC Arusha)
2. Ladson Mwabulambo Mponjoli (RPC Geita)

Lakini kwakua mheshimiwa mwenyekiti anapenda wateule makondoo, basi sitoshangaa kumwona Mambosasa akiukwaa u IGP.
 
Sirro is among of the fewer professional police we have.

Sirro ni viwango vya Donald Rumsfeld aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Marekani 2001 hadi 2006.

Sirro hajawahi kushindwa kwenye kazi, waulize majambazi waliovamia watalii mbugani watakuambia Sirro ni nani.

Jiulize kwa miaka hii ya Sirro wale majambazi waliokuwa wakitamba wako wapi?
Sirro chapa kazi baba.


Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
 
Kwasasa nawaona wawili tu wenye hekima za kutosha kuongoza jeshi la polisi
1. Salum Rashid Hamdini (RPC Arusha)
2. Ladson Mwabulambo Mponjoli (RPC Geita)

Lakini kwakua mheshimiwa mwenyekiti anapenda wateule makondoo, basi sitoshangaa kumwona Mambosasa akiukwaa u IGP.
Hivi unajua kwamba jeshini kuna ngazi za uongozi (ranks)?

Huwezi kumpa Mambosasa u-IGP halafu uwaache makamishna na manaibu makamishna pale Makao Makuu.

Hilo likifanyika basi itabidi Mhe. Rais pia awaondoe viongozo wote ngazi za juu za Polisi ili tu kumpa uhalali Mambosasa awe IGP kitu ambacho sioni kama kinaweza kufanyika.

Hivyo mtu ambae naona ni candidate wa u-IGP baada ya Sirro ni Sabas ambae kwa sasa ni Kamishna wa Operesheni.
 
Hivi unajua kwamba jeshini kuna ngazi za uongozi (ranks)?

Huwezi kumpa Mambosasa u-IGP halafu uwaache makamishna na manaibu makamishna pale Makao Makuu.

Hilo likifanyika basi itabidi Mhe. Rais pia awaondoe viongozo wote ngazi za juu za Polisi ili tu kumpa uhalali Mambosasa awe IGP kitu ambacho sioni kama kinaweza kufanyika.

Hivyo mtu ambae naona ni candidate wa u-IGP baada ya Sirro ni Sabas ambae kwa sasa ni Kamishna wa Operesheni.
Kwani Sirro kabla ya kuwa IGP alikuwa CP au SACP??
 
Kwasasa nawaona wawili tu wenye hekima za kutosha kuongoza jeshi la polisi
1. Salum Rashid Hamdini (RPC Arusha)
2. Ladson Mwabulambo Mponjoli (RPC Geita)

Lakini kwakua mheshimiwa mwenyekiti anapenda wateule makondoo, basi sitoshangaa kumwona Mambosasa akiukwaa u IGP.
Hao wote hakuna aliyekua na busara kumzidi Sirro.

Mtu hawezi kuamini kama 2010 Sirro akiwa RPC Mwanza aliagiza tume imtangaze mshindi mbunge wa upinzani Wenje na akatangazwa.

Ila angalia anachokifanya leo?huwezi kuamini.

Kile kiti hata uwe na busara vp ukishakaa tu busara zinaishia hapohapo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom