Nani amewapa TFS idhini ya Kujenga Makao Makuu yao Mwanza wakati Makao Makuu ya Nchi ni Dodoma?

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,138
Moja kwa moja kwenye mada,

Site tunatambua kwamba Makao Makuu ya Nchi na Serikali ni Dodoma ambapo ndipo kunapaswa kujengwa Makao Makuu ya taasisi zote za Kiserikali ikiwemo Ikulu.

Kwamba toka Jobo Ndugai ametolewa kwenye kiti Dodoma imekosa msemaji wake au?

Swali nani katoa ruhusa kwa TFS na Wizara ya Maliasili kujenga Makao Makuu yao Mkoa wa Mwanza Kwa kisingizio cha deforestation Kanda ya Ziwa?

Huo ni upuuzi na utoto kuleta hoja ya kijinga na kukiuka sheria ya Nchi.Hivi Kati ya Dodoma na Kanda ya Kati kiujumla ukilinganisha na Kanda ya Ziwa wapi kunahitaji nguvu kubwa ya kupanda miti Ili kuboresha mazingira?

Waziri husika achana kabisa na huu mpango vinginevyo inakuwa haina maana ya kuwa na Makao Makuu ya Nchi na hivyo tuanze kusambaza taasisi za Kiserikali kikanda na kimkoa..

Mh.Waziri Mkuu zuia huu ujinga. Ingewezekana na TPA wangehamia Dodoma ila hakuna Bahari.👇

FB_IMG_1656448473829.jpg
 
Nataka nitofautiane na mawazo ya wengi, kwangu haikuwa na maana hata kujenga makao makuu Dodoma niliwaza kwa sauti kama wanavyofanya wenzetu wa huko duniani kwamba huduma zisambazwwe kote nchini, huwezi kuwa na Wizara ya Kilimo makao yake makuu yakae sehemu ambayo hawalimi, mtazamo wangu Maliasili na Utalii ingekua kule Arusha kama ilivyo TANAPA hao wa mamiti na misitu wangekaa hata Iringa ama Sumbawanga, watu wa Kilimo wangekaa mikoa inayolima Mbeya, Iringa etc, wengine ambao hawana specific tasks wangekaa sehemu moja , hii inasaidia kusambaza huduma nchi nzima sio kukaa sehemu moja tu.Hata hao wanaojiita wamehamia Dodoma wako Dar siku zote wanafanyiwa Massage na Scrub ni usanii tu.
 
Wenzetu wa wapi wanafanya hivi unavyosema? Toa mfano wa hizo nchi
 
Tulia dawa iingie, aliyekuambia kuna sheria inayorazimisha kila taasisi ya serikali ijengwe Dodoma ni nani?
Sheria ya kuwa Dodoma ni Makao Makuu ilipitishwa Ili iwaje?

Makao Makuu sio maneno bali ni taasisi za Kiserikali kuwepo sehemu ambayo ndio makao makuu ya Nchi.
 
Nataka nitofautiane na mawazo ya wengi, kwangu haikuwa na maana hata kujenga makao makuu Dodoma niliwaza kwa sauti kama wanavyofanya wenzetu wa huko duniani kwamba huduma zisambazwwe kote nchini, huwezi kuwa na Wizara ya Kilimo makao yake makuu yakae sehemu ambayo hawalimi, mtazamo wangu Maliasili na Utalii ingekua kule Arusha kama ilivyo TANAPA hao wa mamiti na misitu wangekaa hata Iringa ama Sumbawanga, watu wa Kilimo wangekaa mikoa inayolima Mbeya, Iringa etc, wengine ambao hawana specific tasks wangekaa sehemu moja , hii inasaidia kusambaza huduma nchi nzima sio kukaa sehemu moja tu.Hata hao wanaojiita wamehamia Dodoma wako Dar siku zote wanafanyiwa Massage na Scrub ni usanii tu.
Wenzenu wa Dunia ipi? Wanafanyaje? Kwani lazima kupiga kila kitu huko unakoita Duniani?
 
Hapo shida sio makao makuu ya taasisi kutojengwa Dodoma bali shida ni makao Makuu kujengwa Mwanza, mtoa mada ana historia mbaya sana na Mwanza, wasukuma na Kanda ya ziwa kwa ujumla, back hazikabi.
 
Back
Top Bottom