The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 7,382
- 8,437
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu amesema Kuna Taasisi za umma Kwa makusudi zinagoma kuhamia Makao Makuu ya Nchi Dodoma..
Suala kama Kuna wakuu wa Taasisi wanagomea uamzi wa Nchi je huu sio uhaini? Nani anawapa hiyo jeuri? Wanagoma kama kina nani?👇
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene ameziagiza taasisi 42 za serikali kuhamia Dodoma mwaka wa fedha 2022/2023 huku taasisi 36 zikielekezwa kufanya hivyo mwaka wa fedha 2023/2024 bila kuwa na kisingizio chochote
Ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma kwenye zoezi la utoaji vibali vya Ujenzi wa Ofisi za taasisi mbalimbali ambapo amesema kuwa taasisi 19 zitahamia Dodoma mwaka wa fedha 2024/2025 huku Taasisi 27 zikielekezwa kuzingatia aina ya majukumu zilizonazo na kuendelea kutekeleza majukumu yake mkoani Dar es Salaam kwani mpaka sasa tayari taasisi 65 zimeshahamia Makao makuu ya nchi.
Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene amesema jumla ya taasisi 189 zilikua zinatekeleza majukumu yake Jijini Dar Es Salaam ambapo taasisi 55 zimetekeleza maelekezo hayo kwa kujenga ofisi zake Dodoma na hadi sasa taasisi 20 zimekamilisha ujenzi na 16 zinaendelea na hatua mbalimbali huku 19 zikiendelea na maandalizi ya ujenzi baada kupewa vibali.👇