Nani amelipa Tsh Milioni 200 tangazo la Tanzania kwenye jengo la Burj Khalifa, Dubai?

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,480
37,756
Mamlaka ya uendeshaji wa jengo refu zaidi duniani la Burji Khalifa lililoko Dubai hutoza kati ya dola 67,000 hadi 87,000 ambazo kwa ubadilishaji fedha kwa haraka haraka inafiki Tshs. Milioni 157 hadi 200 hivi kwa dakika 3 kuweka tangazo kwenye jengo lote la Burji Khalifa.

Fedha hii kwa nchi masikini kama hii bado ni kubwa na ingeweza kufanya jambo la maana. Jana Februari 28 jengo hilo limetangaza bendera ya Tanzania kwa dakika 3 na wenye Serikali yao wakatutangazia neema kwamba nasi tumeonekana Dubai.

Hebu tuzionee huruma fedha za walipa kodi wanaojikamua huku sisi viongozi tukiishi kwa anasa.

burji.jpg
 
Unakuwa mvivu hata kwa mambo ambayo yako wazi duniani? Ingia google halafu endelea kubishana. Mimi nauliza nani kalipa kama hela zetu tujulishwe faida tuliyopata kwa dakika 3 au tumelipiwa tujiandae?
Vijana wa Mbowe hamna akili kabisa
 
Umelipa wewe,

Unajua faida ya kilichofanyika hapo au ndio "Join the Chain "🤣🤣🤣

Nikusaidie tu, Tanzania haijatoa hata Mia,

#HAKUNA KAMA SAMIA
Wewe jamaa nawe uwe unajibu maswali kwa logic basi.

Unatuaibisha hatari humu JF.

Wewe unazani kuseti hiyo mitambo ni bure?. Sabasaba tu hapo unalipia sembuse na hiyo mitambo?.

Afu bora wanetangaza utalii na utamaduni, na uwekezaji?.. Wao wanatangaza bendera.

Khaaaaa
 
Mamlaka ya uendeshaji wa jengo refu zaidi duniani la Burji Khalifa lililoko Dubai hutoza kati ya dola 67,000 hadi 87,000 ambazo kwa ubadilishaji fedha kwa haraka haraka inafiki Tshs. Milioni 157 hadi 200 hivi kwa dakika 3 kuweka tangazo kwenye jengo lote la Burji Khalifa.

Fedha hii kwa nchi masikini kama hii bado ni kubwa na ingeweza kufanya jambo la maana. Jana Februari 28 jengo hilo limetangaza bendera ya Tanzania kwa dakika 3 na wenye Serikali yao wakatutangazia neema kwamba nasi tumeonekana Dubai.

Hebu tuzionee huruma fedha za walipa kodi wanaojikamua huku sisi viongozi tukiishi kwa anasa.

View attachment 2134765
Washamba hawataisha!
 
Acha ujinga kijana,mnataka maendeleo ila kuumia hamtaki.
Hilo ni tangazo la muhimu kama ya nchi nyingine tu.

USIJE NIITA CCM,SIJAWAHI IPENDA CCM TOKA NIZALIWE lakini tusiwe wajinga wa kubisha tu hata jambo lenye manufaa kwa taifa kama hilo.
Bendera ya Tanzania inapepea UN na kwenye balozi zetu duniani kote, Leo lipi jipya kuonesha bendera kwa dakika 3?
 
Back
Top Bottom