Nani aliyemuumba Mungu?

Asante!
 
Nakubali.

Jibu vyote hivyo halafu utiririke kuthibitisha bila mkanganyiko wa kimantiki kwamba Mungu unayemsema yupo na si hadithi tupu tu.
 
Isome tena post yangu hiyo hapo juu inayo majibu ya swali lako hili ulilouliza hapa
 
Shida ni kwamba huyo Mungu mwenyewe wala haieleweki kama yupo kweli au ni stori tu zilizokuja baada ya sisi kushindwa kujua haswa asili yetu

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kuamini ni nini na kujua ni nini?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Kuamini ni kuwa na maoni ya moyo yenye kufanya kuwa na mkabala fulani juu ya jambo au kitu. Na Kujua ni kufahamu kwa yakini bila ya shaka wala wasiwasi;kuwa na habari.
 
Chunguza vizuri mifano yako hapo utaona si rafiki kadiri ya maneno "kutibitisha" na "uthibitisho."

Naweza kusema, kimsingi kwamba hauko makini. Hivyo ni mtu usiyetaka kujifunza; mpingaji.

Sina mda wa kupingana na mtu mara nyingi natafuta sababu ya kujifunza kitu kwa mitazamo mipya

Ila sipendi watu wasumbufu kama wewe

Mimi nimesema hayo maneno yanamsingi mmoja

Sasa ni jukumu lako wewe unayeyaona katika utofauti kuyatolea maelezo na si kunilazimisha mimi tena ninayeyaona katika umoja niyaone katika utofauti_umeelewa.!
 
Jibu vyote hivyo halafu utiririke kuthibitisha bila mkanganyiko wa kimantiki kwamba Mungu unayemsema yupo na si hadithi tupu
Tuanze na maana. Kwanza maana ya sayansi:

Sayansi ni nini?

Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.

Kwahiyo, sayansi ni shughuli za kiakili na vitendo zinazojumuisha kujifunza mifumo ya miundo na tabia za maumbile na ulimwengu asilia kupitia uchunguzi na majaribio.

Mantiki ni nini?

Mantiki ni kile kinachosemwa; neno au wazo au kinachofundishwa.

Uthibitisho ni nini?

Uthibitisho ni alama inayowakilisha kweli za akili.

Na

Mungu ni nini?

Mungu ni uwepo wa hali ya juu yenye akili.

Unakubaliana na maana hizi?

Karibu!
 
Mimi nimesema hayo maneno yanamsingi mmoja
Nimekubali ulivyosema huko mwanzo kwamba meneno hayo (kuthibitisha na uthibitisho) mzizi wake ni mmoja. Lakini je, yanaeleza hali moja? Hilo ndio swali hapa.

Wakati huo huo, ukiwa unaandika kuwa makini na maneno yako; kwani yanakinzana.

Huwezi kujifunza mambo mapya wakati tayari umejenga msimamo wako.
 
Hata ukisema ulichambue kisarufi hilo neno 'uthibitisho' bado mzizi ni mmoja na neno 'kuthibitisha' ni viambishi tu vinaweza kukupa viashiria kwamba moja ni mchakato na nyengine ni ukamili wa huo mchakato
nilishajibu hapa
 

Katika definitions zako zote, naweza kukubaliana nandefinitionnya sayansi tu.

Tukianza na mantiki, mantiki si kile kinachosema, neno au wazo au kinachofundishwa tu.

Mtu anaweza kusema neno au wazo, akalifundisha, likawa bado halina mantiki.

Unaelewa hilo?
 
Kuamini ni kuwa na maoni ya moyo yenye kufanya kuwa na mkabala fulani juu ya jambo au kitu. Na Kujua ni kufahamu kwa yakini bila ya shaka wala wasiwasi;kuwa na habari.
You are wrong on both counts.

Moyo kazi yake kusukuma damu, hauhusiani na kuamini.

Na unaweza kufahamu kwa yakini bila shaka kwamba wewe ni Rais wa Tanzania, wakati wewe si Rais wa Tanzania, na hivyo, ukawa hujajua wewe ni nani.
 
Maana ya sayansi tumekubaliana.

Vizuri.

Turudi kwenye maana ya mantiki.

Umesema, nanukuu " mtu anaweza kusema neno au wazo, akalifundisha, likawa bado halina mantiki. Unaelewa hilo?"

Ndio, naelewa hilo.

Kwa sababu mantiki ni kipengee cha sayansi kinachoshughulika na kuthibitisha kile kinachosemwa, neno au wazo; au kinachofundishwa kama kinakubalika kiakili.

Hivyo ulichoandika nakubaliana nacho; kwani umefafanua maana ya mantiki niliyoileza hapo.
 
Maana uliyoiandika ya mantiki ilikuwa batili.

Unakubali hilo?
 
You are wrong on both counts.

Moyo kazi yake kusukuma damu, hauhusiani na kuamini.

Na unaweza kufahamu kwa yakini bila shaka kwamba wewe ni Rais wa Tanzania, wakati wewe si Rais wa Tanzania, na hivyo, ukawa hujajua wewe ni nani.
Sawa,haya eleza mahusiano ya kujua na uthibitisho?
 
Kwa nini?
Kwa sababu umekuwa ukihusisha kujua na uthibitisho,kwamba ili useme jambo fulani najua basi lazima uweze kuthibitisha.

Ndio nataka kujua kuna mahusiano gani ya kujua na uthibitisho?
 
Kwa sababu umekuwa ukihusisha kujua na uthibitisho,kwamba ili useme jambo fulani najua basi lazima uweze kuthibitisha.

Ndio nataka kujua kuna mahusiano gani ya kujua na uthibitisho?
Wapi nimehusisha kujua na uthibitisho?

Unaweza kunipa mfano hai kutokana na maandiahi yangu mwenyewe nilipohusisha kujua na uthibitisho?

Kujua ni nini? Uthibitisho ni nini?

Kuhusisha kujua na uthibitisho ni nini?

Unajuaje unajua na si kwamba unafikiri tu unajua?

Unajuaje uthibitisho wako ninsahihi na si kwambabunafikiri tu ni sahihi?

Unajuaje usahihi, njw ya muktadha maalum finyu, ni kitu kilichopo kweli na si njozi inayotokana na upotofu uliojengwa katika fikra zetu dhaifu tu?
 

"Ukiweza kuthibitisha, umeondoka kwenye kuamini, uthibitisho wako unasema kwamba wewe unajua."

Maelezo yako hayo yamehusisha kujua na uthibitisho,kwamba uthibitisho ndio unafanya useme unajua bila uthibitisho inabaki imani tu hivyo kwenye imani hakuna kujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…