blackberry m
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 563
- 414
Salaam nyingi wanajamvi wenzangu.
Baada ya salamu ningependa niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Baada ya tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Paul Makonda la kudaiwa kuvamia na kupora kama inavyodaiwa, mimi binafsi napata mashaka kutokana na sababu mbalimbali kama vile,
1. Kwa ninavyofahamu ni kuwa, milango ya pale ina nywila (password) ambayo huzuia uingiaji wa mtu ambaye si muhusika wa hapo. Sasa swali ninalojiuliza ni kwamba; endapo wao hawahusiki basi ni nani aliyempa Makonda hizo password?
2. Kwanini wanang'ang'ania kutaka kuwepo kwa mipaka badala ya kuchukua maamuzi magumu?. Kumbuka kauli ya mkurugenzi wao, kwamba endapo Makonda ataomba msamaha basi yataisha.
Uono wangu. Japokuwa naamini kuwa ni hafifu lakini nauamini kuwa hiyo ishu ni ya kupangwa ili kutuaminisha jambo au kutuondoa kwenye reli.