• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Isaya Mwita kuendelea na majukumu ya umeya Dar. Nywila za Ofisi yake zarejeshwa

S

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Messages
242
Points
250
S

Suley2019

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2019
242 250
2273303_1579079805674.png

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema ataendelea kutekeleza majukumu yake ya ofisini kwani halmashauri hiyo imerejesha nywila (password) zilizokuwa zikitumika.

Baada ya ofisi hizo kufungwa na kubadilishwa nywila na kuweka mpya, Mwita alisema halmashauri hiyo imerejesha nywila za zamani hivyo, ataendelea na kazi zake. Akizungumza na gazeti hili jana, Mwita alisema anachoamini kuwa yeye bado ni meya wa jiji hilo na kwamba kuna majukumu ya kuendelea kuyatekeleza.

Mwita alisema kanuni ya 84 (1) ya halmashauri inaelekeza ili kumwondoa madarakani inapaswa kuwepo kura theluthi mbili ya wajumbe wote wa halmashauri na makosa yatakayosababisha kuondolewa yameainishwa kwenye kanuni hiyo kuwa ni rushwa, kutumia madaraka vibaya na kubaka.

Alisema kanuni hizo hazikutimizwa katika kikao cha Januari 9, hivyo ataendelea kutekeleza majukumu ya umeya mpaka muda wake utakapokwisha.

“Nilipewa barua Januari 10 ya kukabidhi ofisi na Mkurugenzi wa jiji, nilimjibu kuwa mimi ni meya halali kwa sababu akidi haikutimia siku ya kikao na nikamkumbusha kanuni zetu. Kuhusu ofisi tayari wameshabadilisha nywila ya kuingia hivyo naweza kuendelea na majukumu yangu,”alisema Mwita.

Aliongeza kuwa wajumbe wa halmashauri ni kama wabunge ambao wakitaka kumuondoa Rais, Waziri Mkuu au Spika wanatakiwa kupata theluthi ya kura zote hivyo, kilichotokea ni kushindwa kutafsiri kanuni hiyo.

Alisisitiza kuwa wajumbe walikuwa na uwezo mzuri wa kumuondoa kwenye nafasi hiyo endapo watakaporubuni mmoja wa wajumbe ili kukidhi akidi na kwamba siku 45 bado za kufanya hivyo zipo hivyo, wangepata kura 17 za kumtoa na kwamba wajumbe wasipohudhuria vikao mara tatu baraza hilo litavunjwa na kumkosesha nafasi.

“Nimekuwa mwaminifu kwa kuleta maridhiano kwenye halmashauri yetu, sikuwahi kumvunjia mtu heshima wala kumdhalilisha mtu hivyo, haya ninayopitia nashangaa sana kwani nimedhalilishwa,”alifafanua Mwita

Aliongeza kuwa “Kama theluthi ingepatikana nisingeendelea kung’ang’ania kwa sababu ni ujinga tena ingefaa kukamatwa na vyombo vya dola lakini pia ningetakiwa kukata rufaa kwa Waziri husika wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na ingekuwa nafasi yangu ya mwisho lakini sijaondolewa,” Meya huyo alieleza kuwa akiendelea kupiga kelele atamzuia Rais kufanya kazi kwani anampenda na ni rafiki yake kwani ndiye aliyemfanya awepo hapo mpaka sasa.

Kwa upande wa wakili wake, Hekima Mwasipu alisema Mwita akiondolewa madarakani kisheria hawezi kunufaika na mafao yake kwa sababu atakuwa amepoteza sifa kwa mujibu wa taratibu.

“Endapo watamzuia kupata mafao yake, sisi tutafungua kesi nyingine mahakamani ili aweze kupata haki zake hata kama sio mwaka huu atazipata mwakani kwani bado ana sifa,” alisema.


Habari Leo
 
K

KIM JOHN UN

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2017
Messages
657
Points
1,000
K

KIM JOHN UN

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2017
657 1,000
huyu meya sasa awe makini coz walivobadili nywila hajui ni nini watu wa TISS wamemwaga huko ndani ya Ofisi.mark my words mtaanza kusikia wau wanaanza kutoa salamau za…
 
Lukaku Tanzania

Lukaku Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2017
Messages
843
Points
1,000
Lukaku Tanzania

Lukaku Tanzania

JF-Expert Member
Joined Sep 7, 2017
843 1,000
Dar viongozi cjui wakoje Juz MO Dewji nae kakatalia uenyekiti Leo huyu nae mwita hivo viti havihamishiki ee
 
3 Angels message

3 Angels message

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2017
Messages
2,345
Points
2,000
3 Angels message

3 Angels message

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2017
2,345 2,000
Mmmh kirahisi tu hivyo wameamua kumrudishia ili hali walidhamiria kumuondoa na gari kanyang'anywa hii huruma imetoka wapi? Na kwanini walifanya vile?
 
B

Boaziwaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2019
Messages
391
Points
250
B

Boaziwaya

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2019
391 250
Mmmh kirahisi tu hivyo wameamua kumrudishia ili hali walidhamiria kumuondoa na gari kanyang'anywa hii huruma imetoka wapi? Na kwanini walifanya vile?
kuna kitu najiuliza sipati majibu kabisa, adui akikuletea keki ichunguze vizuri kwanza usiibugie
 
Sang'udi

Sang'udi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Messages
2,005
Points
2,000
Sang'udi

Sang'udi

JF-Expert Member
Joined May 16, 2016
2,005 2,000
Meya huyo alieleza kuwa akiendelea kupiga kelele atamzuia Rais kufanya kazi kwani anampenda na ni rafiki yake kwani ndiye aliyemfanya awepo hapo mpaka sasa.
 
Damian J Ntundagi

Damian J Ntundagi

Verified Member
Joined
Jun 28, 2017
Messages
1,302
Points
2,000
Damian J Ntundagi

Damian J Ntundagi

Verified Member
Joined Jun 28, 2017
1,302 2,000
Hii nchi hii
 
900 Inapendeza zaidi

900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2017
Messages
2,061
Points
2,000
900 Inapendeza zaidi

900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2017
2,061 2,000
Utendaji wake wa kazi haukuwa Mzuri kwa baadhi ya Viongoz wa ngaz zake
Hawakua na imani nae,.Yote yalianzia huko
mbona watanzania hatuna imani na meko lakini anaendelea tu kupuyanga ,kwanini wanahangaika na huyu meya
 

Forum statistics

Threads 1,402,696
Members 530,972
Posts 34,402,648
Top