Nani alikuwa mbishi kumwelewa Mwl.Magufuli na sasa anamwelewa vizuri?

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,944
Ndugu, tangu Nov.2015 mpaka sasa Headmaster wa Tanzania ni Magufuli, na kikatiba inaonekana sote tulimchagua ingawa tupo wengi tu ambao hatukumchagua na hatutamchagua kwa sababu zetu binafsi.
Huyu tangu aanze kazi ametuadabisha direct au indirect.
Wengi tuliwaambia hapa tumebugi huyu mtu wakabisha.
Ngoja nikupe mifano michache ya ambao somo limewaingia sasa hivi;
A:Kijana msomi wa ngazi ya
degree ya elimu (Arts), huyu kila nikimweleza haelewi, anasema Magufuli ananyoosha nchi mambo yatakaa sawa, weeee kapigwa juu kwa juu, walimu wa sanaa hawahitajiki, jamaa chali, somo kalielewa.
B: Mzee msaafu wa idara fulani, huyu kila mara alikuwa akifanya mahali pa duka langu kama kijiwe cha kuinadi CCM na Magufuli, kila nikimweleza hoja za nguvu habadiliki, weeee, anakuja mikono nyuma huku akikiri ujinga anataka
nimkopeshe unga, familia
ile.Hana hamu naye tena, somo limemwingia bila kujali umri wake.
3.Mama mmoja, huyu alikuwa mfanyakazi mwenzetu. Kama ilivyo ada ukiondoa kwenye majeshi , taasisi nyingi za umma asubuhi kabla ya kuanza majukumu ya kila siku first ni stori za siasa, huyu mama alikuwa haambiliki kuhusu CCM & Magufuli, majuzi kabainika kwenye list ya walioghushi vyeti. Hapatikani kwenye simu yake ya siku zote .Somo limemwingia.
Wataje kama kuna ambao walikuwa wabishi wa kuelewa masomo ya Magufuli na leo wanayapata vizuri.
Usiyeelewa masomo ya mzee wetu mpendwa nakusihi subiri utayaelewa vizuri.
 
Be. Mpelengana huyo ticha kwa wasomi somo wanalo lakini sisi wakulima tunaoamka nashughurikia mihogo yangu mpunga pamba NA dengu huwezi kuamini hiyo ticha ni keki ushahidi nimeuona kwenye chaguzi za mabalozi huku vijijini wanafurahi sana kusikia utumbuaji hawajui ni mini maana ya kukiuka katiba bado somo vijijini halijaeleweka la ticha wetu.
 
Mbishi kumwelewa Ticha hapo ni Bashite tu...piga ua.!

mie namwelewa,kwa tarakimu pia kwa namba.
 
Teacher wetu anaeleweka vizuri sana kwa sababu mazao yamekauka hata hao wakulima walipiga kelele ya kutaka chakula aliapa hatoi shibe kwa mtu NA aliye nacho apandishe bei sisi wakulima ni watu wa ajabu sana NA hii nchi itatawaliwa NA upinzani baada ya miaka 50 mpaka kati ya wakulima 10 angalau 8 wawe NA elimu ya chuo kikuu so kama Leo kati ya wakulima 10 %3 ni sekondari bado somo la teacher mtalisoma sana mjini
 
Usijari utamuelewa akistafu,,
Na utasema sana kwamba tunakukumbukaa,,,
Na ukipata nafsi ya kumuona utampigia makofii,,,lakin akistafu,,,
 
2020 wengi watamchagua tena zaidi, kwa sababu hakuna chama cha upinzani kitakachochukua madaraka kwa jinsi walivyo sasa na hawatabadilika.

Namba inasomwa na wengi sana kwa njia tofauti, ila ndio ilivyo na ni chini wa uongozi wa Raisi anayejali wananchi wake. Na mazoea ya zamani yatasahaulika na kupenda maisha mapya ya mnyooko.

Tutafika tu
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom