Nani aliita SIMU 2000 pale Mawasiliano?

Nani aliita SIMU 2000 pale Mawasiliano?

naona mnadanganyana sasa!
SIMU 2000 ilikuwa ni kampuni iliyokuwa inahodhi mali za serikali wakati wa ubinafsishaji awamu ya tatu ya ben mkapa, hii kampuni ilimaliza kazi zake mwishoni wa awamu ya tatu na kazi zake nafikiri siku hizi zinafanya na consolidate holding corporation wapo pale mirambo st opposite na ofisi za world bank tanzania ,pia nilisikia CHC muda wake wakufanya kazi ulitakiwa uishe mwaka huu wa fedha,pia kulikuwa na kampuni nyingine zinazofanana na SIMU 2000 kama LART, ATHCO
kwa hiyo kile kituo kipya cha mabasi kilikuwa kinaodhiwa na hiyo kampuni inayoitwa SIMU 2000 Tanzania ltd ndio maana bado panatambulika kama eneo la kampuni tajwaa iliyohodhi eneo hilo

hilo swala la vibaka kuiba simu na kuuza shilingi 2000 wapate pesa ua unga ni uongo mkubwa,
unaweza kupata info za kampuni ya SIMU 2000 kupitia tovuti ya ::CHC Homepage::

Mkuu Mimi nimekupata vyedi. Hii ndo JF, the house of great thinkers. No data no right to bwabwaja!
 
Salamu nyingi sana kwenu.
Napatwa shida kidogo kufahamu maana na asili ya neno simu2000 ambalo lipo kwenye mabasi ya mawasiliano.
Kwa mwenye ufahamu anijuze tafadhali.
Asante.
 
Hili jina limetokana na kampuni iliyoanzishwa baada ya kampuni ya TTCL kubinafsishwa!

Kampuni hii ilikuwa inamiliki mali zote za ttcl nje ya kile kilichobinafdishwa!! Namaanisha viwanja na majengo (real estate) hivyo kampuni yenyewe iliitwa simu2000 kwa vile ilianzishwa mwaka 2000! Mali za iliyokuwa TTCL ni nyingi ila wajanja wachache walizifaidi!

Hivyo basi eneo la stand lilikuwa mali pia ya Simu2000
 
Duh! Vipi mbona sijasikie sehemu nyingine inaitwa simu2000 au kamuni ilikuwa inamiliki eneo lile la mawasiliano pekee?
 
Lile ni eneo ambalo vibaka wa Ubungo Darajani na ubungo mataa walikuwa wanajificha...Siku polisi wameenda kupiga msako wakakuta simu ndani ya vichaka,baada ya kuhesabu zikawa simu 2000 ikiwemo ya Kamanda Tibaigana aliyoibiwa akiwa kwenye foleni ya kusubiri mataa ya Ubungo,toka hapo pakaitwa Simu 2000
 
Hili jina limetokana na kampuni iliyoanzishwa baada ya kampuni ya ttcl kubinafsishwa! Kampuni hii ilikuwa inamiliki mali zote za ttcl nje ya kile kilichobinafdishwa!! Namaanisha viwanja na majengo (real estate) hivyo kampuni yenyewe iliitwa simu2000 kwa vile ilianzishwa mwaka 2000! Mali za iliyokuwa ttcl ni nyingi ila wajanja wachache walizifaidi! Hivyo basi eneo la stand lilikuwa mali pia ya simu2000
Asante Mkuu nimejifunza kumbe
 
Tulijadili miaka miwili iliyopita jaribu kuangalia related threads humu jf IPO
 
Lile ni eneo ambalo vibaka wa Ubungo Darajani na ubungo mataa walikuwa wanajificha...Siku polisi wameenda kupiga msako wakakuta simu ndani ya vichaka,baada ya kuhesabu zikawa simu 2000 ikiwemo ya Kamanda Tibaigana aliyoibiwa akiwa kwenye foleni ya kusubiri mataa ya Ubungo,toka hapo pakaitwa Simu 2000

hahahah bado hujaacha tu cha arusha
 
HAHAHAHA,HIYO YA VIBAKA KAKA,KACHEMKA.KWANI VIBAKA HAWAWEZI KUKAAA NA HIZO SIMU ZOTE,KWAN KIBAKA AKISHAIBA ANAKWENDA KUUZA,SASA KUSEMA POLICE WAMEKUTA CM2000 HAPO UMETUPIGA,CHITING_CHALAGA
 
MD wa Simu 2000 alikuwa ni mtoto wa Ben Mkapa. Watu walipiga sana ela kupitia hiyo company
Kuna siku nilibishiwa na kutukanwa matusi makubwa sana kwa kusema B. Mkapa ana mtoto aisee yaani kuna watu huku uswahilini ni wabishi balaaa

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Mi nikajua pameitwa simu2000 kama maana nyingine ya neno MAWASILIANO. Yaani huwezi kufanya mawasiliano kwa simu moja tu (utajipigia mwenyewe?!!), so ili mawasiliano yafanyike kuna uhitaji wa simu nyingi kwa kupasiana ujumbe tofauti tofauti ndo wakaamua kupaita SIMU2000!! Dahh kumbe nilikua mbali kweli.

Ni vizuri kujua chimbuko la hilo jina lakini japo kweli baya.

Heheheee...
 
Sijaelewa mantiki ya kuita kituo cha daladala eti SIMU 2000 Kisa pale kulikuwa na coy husika na aliyo fisadi mapesa kibao enzi za Mkapa.

Unavyoanzisha jina la biashara au sehemu linatokana na urahisi wa kutamkwa na watu wa pale, wazawa n.k, leo nilikuwa kwenye NIDA kuchukua national ID, idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika ni kubwa sana.

Hoja yangu kwanini kituo husika wasikite MAWASILIANO kama watu na makonda wengi wanavyokiita wao. Leo nilikuwa Ubungo muda nimewasikia sana baada ya kupata news ya kusitishwa mdahalo nikiwa nimefika, wakiite kama ilivyokuwa Makumbusho au wakiite TANESCO majina mepesi kuliko jina hili ambalo alina mvuto eti "simu elfu mbili".

Pia kituo kiko poa sanaaa, ila maingilio yake toka Shekilango na Mandela road kuna vumbi ya maana.

Nawasilisha.

Mtoto wa Mkapa
 
Lile ni eneo ambalo vibaka wa Ubungo Darajani na ubungo mataa walikuwa wanajificha...Siku polisi wameenda kupiga msako wakakuta simu ndani ya vichaka,baada ya kuhesabu zikawa simu 2000 ikiwemo ya Kamanda Tibaigana aliyoibiwa akiwa kwenye foleni ya kusubiri mataa ya Ubungo,toka hapo pakaitwa Simu 2000

Hehehe.... Hihihiiiii
 
We mzee😀😀😀😀
 
vibaka walikuwa wakikwapuo simu kule ubungo stand wanakimbilia kwenye hiko kituo na si unajua tena biashara ya mali ya wizi inapochelewa kununuliwa bei inavyoshuka mishowe simu ikaanza kuuzwa tsh 2000 ili kibaka akapate kete moja ya dawa ya kulevya.hivyo hapo simu ilikuwa ikiuzwa 2000.jibu safi na makini
Kumbe barafu hujadanganya?
 
Back
Top Bottom