Nani aliita SIMU 2000 pale Mawasiliano?

Nani aliita SIMU 2000 pale Mawasiliano?

vibaka walikuwa wakikwapuo simu kule ubungo stand wanakimbilia kwenye hiko kituo na si unajua tena biashara ya mali ya wizi inapochelewa kununuliwa bei inavyoshuka mishowe simu ikaanza kuuzwa tsh 2000 ili kibaka akapate kete moja ya dawa ya kulevya.hivyo hapo simu ilikuwa ikiuzwa 2000.jibu safi na makini

Kwahiyo na serikali nayo imebariki na kuenzi maovu yaliyokuwa yakifanyika hapo pamoja na hilo jina la a.k.a walilokuwa wakitumia kuita hao mapusha na vibaka?
Hapo serikali Wamechemka kama sio kutokota kabisa kwa jina la ajabu ajabu namna hiyo.
 
Basi kuna daladala leo limeandikwa Simu 2000/ kkoo, kila mtu analishangaa pamoja na kwamba limesimama kwenye kituo chenyewe.
 
lilikuwa eneo la posta na simu ( tp&tc) likatwaliwa na simu 2000 sasa linamilikiwa na manispaaa kinondoni!

Safi sanaa na inaonekana unajua mengi kuhusiana na eneo husika, basi saidia kuwaeleza wapaite MAWASILIANO au SIMU ita sound vizuri.
 
Basi kuna daladala leo limeandikwa Simu 2000/ kkoo, kila mtu analishangaa pamoja na kwamba limesimama kwenye kituo chenyewe.

Yani ni shideeeeee.....sijui akili za Yusuph mwenda hizi, nimeona bandiko la diwani wa sinza R.PAMBA anapaita SINZA BUS TERMINAL.

Yaniiiii!!!
 
eneo lilikuwa bado chini ya serikali, simu 2000 ltd haipo siku hizi, halmashauri pia ni serikali

Sawa sasa kwanini upaite sasa jina hilo wakati coy lenyewe alipo, na lilifisadi tuuu mali ya uma unafundisha nini vizazi vya sasa.

Wambie wapaite MAWASILIANO.
Unasikia?
 
Sawa sasa kwanini upaite sasa jina hilo wakati coy lenyewe alipo, na lilifisadi tuuu mali ya uma unafundisha nini vizazi vya sasa.

Wambie wapaite MAWASILIANO.
Unasikia?
tatizo ni ndugu zako wa sumatra wanaolazimshaa paitwe hivo,pia wanasiasa wanalumbana paitweje ila jina sahii ni SINZA A, wanaogopa wakipaita hivyo watampa promo diwani wa hapo kutoka chadema ukawa
ndio maana jina la SIMU 2000 Linalazimishwa liendelea kudumisha historia ya CCM kuhusu sera za ubinafsishaji (privatezation)
 
Mkuu ahsante sana kwa kunifumbua macho niliona daladala imeandikwa SIMU 2000 - TEGETA nikashindwa kuelewa kumbe ndo hvyo
 
tatizo ni ndugu zako wa sumatra wanaolazimshaa paitwe hivo,pia wanasiasa wanalumbana paitweje ila jina sahii ni SINZA A, wanaogopa wakipaita hivyo watampa promo diwani wa hapo kutoka chadema ukawa
ndio maana jina la SIMU 2000 Linalazimishwa liendelea kudumisha historia ya CCM kuhusu sera za ubinafsishaji (privatezation)
okay nimeanza kuelewa kwanini panaitwa hivyo kwasababu ya huyu pamba...ata pata promo, na makonda ndio naona wanazidi kupaita mawasiliano...
 
acha tuu ni akili ya yusuph mwenda hiyo....na maCCM ya halmashauri ya kinondoni Mnyika sema hili basi

Mkuu hata mm sikuamini km dala dala ya Tanzania imeandikwa SIMU 2000
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo na serikali nayo imebariki na kuenzi maovu yaliyokuwa yakifanyika hapo pamoja na hilo jina la a.k.a walilokuwa wakitumia kuita hao mapusha na vibaka?
Hapo serikali Wamechemka kama sio kutokota kabisa kwa jina la ajabu ajabu namna hiyo.

na wewe unaskiliza story za KOLOKOLONI ? hilo eneo lilikuwa la SIMU 2000, mamlaka iliyokuwa na dhamana ya kusimamia mali za POSTA NA SIMU wakati wa kipindi cha mpito. ni sawa na kituo kiitwe KAMATA nk
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa najiuliza kwanini panaitwa hivyo leo nimepata jibu Ahsante mleta mada
 
Ingefaa paitwe ESCROW jina zuri kabisa hilo. Kama ni dala dala la kwenda Tegeta utakuta limeandikwa TEGETA ESCROW
 
Back
Top Bottom