Nandy usije kulia kama Vanessa Mdee

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
By Sangu Joseph

Njia ya kuanguka kimuziki ya Vanessa Mdee nadhani inafaa kuwa fundisho Sana kwa Wasanii wakike nchini lakini Kwa Leo naomba niidedicate Kwa Nandy zaidi.

Inawezekana mkaniona wa ajabu Kwa hili la Vanessa kuliita anguko muziki Kwa sababu nalifananisha na anguko la Lina Sanga tofauti nu nyakati na style ya kuanguka.

Kwa sasa Nandy ndiye Best Female Artist Kwa Tanzania, na kabla yake alikuwepo Vanessa Mdee ambaye anguko lake tuliliona limeanza 2020, lakini kabla VMoney hajapanda aliyekuwa juu ni Linab Sanga ndiye aliyempa Kijiti V tunajua level ambayo alifikia Lina alirekodu Ngoma mpaka kimataifa, Kolabo za Ndani zilikua ni shikamoo hasa Ile Yalaiti na Gwiji FA ni Shikamoo Sana.

Sitaki kumzungunzia Lina Kwa leo na Vanessa Kwa leo, Ila wote Stori zao zinapaswa kuwa fundisho Kwa Msanii namba moja wakike. Kwa sasa Nandy, ameona jinsj Lina Maisha anayoishi sasa kupost Picha za zisizoeleweka / VMoney analialia akidai mziki ni ngumu wakati Maisha ya muziki aliyoishi aliyachagua mwenyewe.

Siamini Kwamba Nandy mpaka sasa hajawekeza sehemu yeyote, kama hajafanya hivyo wakati bado upo Kwa sababu itafika wakati ladha zake zitapita na vizazi vipya vitakuja na Watanzania watahitaji Sana kuvisikia hivyo ajifunze Kwa hawa ndugu zake wawili ambao Kwa sasa hawaeleweki.

Sidhani kama 2020 ndiyo Mwaka wa mwisho wa Nandy kushine hapana Ila akijipanga vizuri Sana na akawa kama underground anayetoka Leo nadhani bado anamiaka mingine 5 mbele ya kufanya vizuri ila kama atakuwa kama Yule Nandy aliyefanya Show mbovu kwenye Onesha la siku ya Africa pale MTV simuoni Nandy wa miaka 5 mbele.

Nandy wa miaka 5 hatuhitaji aitelekeze Album yake na kutoa nyimbo nyingine Japo nazo ni Kali sana.

Nandy wa miaka 5 arejeshe Tamasha Lake na #NandyFestival ili kusambaza soko lake Tanzania nzima.

Nandy wa miaka 5 asiweke mbele mapenzi akashindwa kumantain na kazi, Japo sijaona Negative direct effect za Mahusiano ya Nandy na Billnass Ila nilishawahi kuhisi ilimfanya afanye show mbovu la MTV.

Next time nitaeleza Jambo kuhusu Maua Sama.

Nicheki Insta : FB : Twitt : Sangu Joseph

#KijanaMzalendo #IloveTZ

Tazama hapa
 
Mmmh hebu niambie kwa kifup.

Kwani vannesa ana shida gani ? Kaolewa ?
 
nilivosoma bandiko nmecheka hadi mbavu zinauma, khaaaah yaan Nandy amfikie Vanessa?
Halafu nilichokigundua wengi wameingia kichwa kichwa ile interv ya vee, vee pesa alishawekeza had ana label yake,
Vee ana brands had na kufanyiwa re - imagned nyimbo zake
Aliwa hadaa mashabiki ili wawe wapole, yeye aendelee kula kwan good time vs pause na Rotimiiiih, ila mziki hawezi kuacha kamweeeh.
 
nilivosoma bandiko nmecheka hadi mbavu zinauma, khaaaah yaan Nandy amfikie Vanessa?
Halafu nilichokigundua wengi wameingia kichwa kichwa ile interv ya vee, vee pesa alishawekeza had ana label yake,
Vee ana brands had na kufanyiwa re - imagned nyimbo zake
Aliwa hadaa mashabiki ili wawe wapole, yeye aendelee kula kwan good time vs pause na Rotimiiiih, ila mziki hawezi kuacha kamweeeh.
Kwasis ambae vanesa tunamfahamu.na hata pia tunapiga nae stor...tukikwambia alichoongea ni ukwel mtupu utaamini?..
 
Kwasis ambae vanesa tunamfahamu.na hata pia tunapiga nae stor...tukikwambia alichoongea ni ukwel mtupu utaamini?..
Sijakataa km sio kweli ila sio kwamba eti atakua maskin n uwongo. Maan katokea familia inayojiweza.
 
Back
Top Bottom