Nandy ni mwanamke mwenye uwezo mkubwa kimziki

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
.
By Sangu Joseph
.
Mwanzoni mwaka huu niliahidi kuandika makala ya kwanini kwa sasa msanii Nandy au African Princess ndiye msanii namba moja wakike Tanzania, ukilinganisha na dada yetu Vmoney (Kitu gani kimemkuta Vanessa Mdee? ) ambaye Kwa sasa yuko honey moon ya muda mrefu kulea penzi lake na Rotim.
.
Kuna baadhi ya watu walinishauri ungeachana nayo, kwa sababu isingejenga bali ingekuletea sintofahamu na baadhi ya mashabiki wenzako wa muziki, ikanifanya nisitishe lakini naamini watu walielewa ambacho nilieleza kuhusiana na hatua ya Vmoney (Soma zaidi Kitu gani kimemkuta Vanessa Mdee?).
.
Leo nimeona nimuelezee Nandy kwa namna nyingine kuwa ni mwanamke na Nusu kwa kutoa nyimbo kati kati ya wanaume wenye njaa.
.
Kwa uzoefu wangu ni mara chache kuona wasanii wengi hasa wakike kutoa nyimbo siku chache baada ya Msanii mkubwa kutoa nyimbo na bado ngoma ikafanya vizuri mtandaoni hasa ukizingatia nguvu waliokuwa nayo baadhi ya wasanii
.
Kiukweli nimeona Nandy ana kila sababu ya kuitwa Mwanamke na nusu na kupewa minyama yake kwa kuwa amefanya jambo kubwa sana Kwa kutoa ngoma katika wakati ambao Diamond, Darassa, Aslay na Janjaro lakini yeye ameweza kupenya katikati ya Simba wenye njaa ()
.
Nandy anakila sababu ya kupongezwa, na kila mpenda muziki wa Kitanzania hasa ukizingatia, jinsi ya ugumu ya game ya BongoFleva kwa wanawake ambao wengi wao wanashindwa kuonesha mabavu yao mbele ya wanaume ambao wanaonekana kutawala soko la BongoFleva.
.
.
#KijanaMzalendo #IloveTZ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kolabo sio kipimo pekee, kwahiyo Vanesa ni bora kuliko Alikiba? Nnachojua Vannesa ana connection (exposure) hata kabla hajawa mwanamuziki

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kiba sio levo za vanessa mzee,,, angalia international act.
Hapa bongo international ni mond,rayvan,harmonise,vanessa, na atleast trappers na watu wa style hizo.
Hawa wengine kina saida karoli wanaweza kuimba na kukiki kibongo zaidi ya hao juu lakini ndo ivyo mziki wao utabaki hapahapa tu.
 
Back
Top Bottom