SI KWELI Nanasi huharibu ujauzito

SI KWELI Nanasi huharibu ujauzito

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Nanasi ni tunda lenye faida lukuki kwa afya. Miongoni mwa faida za tunda hili ni kuongeza kinga ya mwili, kutibu mafua, kupambana na saratani, kuondoa maumivu pamoja na kulinda moyo.

973EA762-2BEF-497A-AF05-43B0395AE9D4.jpeg

Pamoja na uwepo wa faida hizi kwa afya, nanasi huhusishwa na changamoto ya kuharibika kwa ujauzito kwa wanawake, hivyo baadhi ya jamii huwashauri wasitumie tunda hili kama njia ya kulinda ujauzito wao. Ukweli upoje?
 
Tunachokijua
Nanasi huhusishwa na kuharibu ujauzito mchanga kwa wanawake.

Athari hii hutokana na uwepo wa vimeng’enya vya bromelain ambavyo kiasili hupatikana kwenye nanasi pekee.

Kwa mujibu wa USDA, Bromelain ni kundi kubwa la vimeng’enya vinavyopatikana kwenye tunda la nanasi ambavyo pamoja na kazi zingine, husaidia mmeng’enyo wa vyakula vyenye asili ya protini pamoja na kutibu au kudhibiti uvimbe mwilini.

Kuhusu ujauzito, ni kweli kuwa Vidonge vyenye bromelain huwa havishauriwi kumezwa na mwanamke mjamzito kwa sababu vinaweza kumfanya apoteze damu nyingi pamoja na kuharibu ujauzito. Hii inatokana na uwepo wa dozi ya kutosha kwenye dawa hizo inayoweza kuleta athari.

Hata hivyo, JamiiForums imebaini kuwa Bromelain inayopatikana kwenye nanasi ni chache sana kuweza kuleta athari zozote kwa ujauzito, haifikii kiasi cha kawaida cha dozi ndogo inayohitajika kuamsha uchungu wa mapema.

Pia, hakuna tafiti za kisayansi zinazothibitisha madhara haya kwa binadamu.

Kwa maana hiyo, nanasi linabaki kuwa tunda bora na salama kwa mwanamke mjamzito kutokana na uwepo wa virutubisho vingi vinavyofaa kwa mama na mtoto.​
Ndo yale yale mjamzito asile mayai au kuku sijui atazaa mtoto hana tako mara sijui nini nywele eeh...?! WTF?
 
Ndo yale yale mjamzito asile mayai au kuku sijui atazaa mtoto hana tako mara sijui nini nywele eeh...?! WTF?
Mayai ni protein. Unapomlisha mjamzito mayai, kuku, samaki kwa kiwango kikubwa mtoto kuna uwezekano mkubwa akatoka mkubwa. Ikamletea shida wakati wa kujifungua ikalazimu ajifungue kwa operation.

Usipuuze maneno ya wahenga. Ulitumika uongo ili kusaidia jamii.

Miiko mingine ilikuwa ni marufuku kwenye kwenye misitu na vyanzo vya maji story zilikuwa kwamba kuna majoka makubwa ambayo ukienda linakumeza na kukugeuza chakula. Ili watu wasizoee kwenda maeneo ya vyanzo vya maji wakachafua na kuharibu.
 
 
Tusidharau wahenga.

Kama watu washasema nasisitiza mjamzito usile nanasi ,kama vitamin c kula machungwa.
 
Nanasi ni tunda lenye faida lukuki kwa afya. Miongoni mwa faida za tunda hili ni kuongeza kinga ya mwili, kutibu mafua, kupambana na saratani, kuondoa maumivu pamoja na kulinda moyo.

View attachment 2410631

Pamoja na uwepo wa faida hizi kwa afya, nanasi huhusishwa na changamoto ya kubaribika kwa ujauzito kwa wanawake, hivyo baadhi ya jamii huwashauri wasitumie tunda hili kama njia ya kulinda ujauzito wao. Ukweli upoje?
Nimewahi sikia hata damu ya mke na mme zisipoendanda Kinga ya mwili wa mwanamke huchukulia mimba kama ugonjwa na kuiharibu au kutoka mapema kabla ya muda wake
 
Mimba ikiwa changa haishauriki sana kwa sababu kuna acid ambayo ipo kwenye nanasi itakwenda kuchochea Hormone ya oxytocin na kuchochea uchungu ikapelekea mimba kutoka. Lakini kuanzia miezi 3 mtoto amekuwa amejishikiza vema kwenye mfuko na isilete madhara.
Wewe acha utapeli
 
Mimba ikiwa changa haishauriki sana kwa sababu kuna acid ambayo ipo kwenye nanasi itakwenda kuchochea Hormone ya oxytocin na kuchochea uchungu ikapelekea mimba kutoka. Lakini kuanzia miezi 3 mtoto amekuwa amejishikiza vema kwenye mfuko na isilete madhara.

Na wanashauri kama moja ya Kichocheo cha kuleta uchungu week zikitimia 40
 


Baadhi ya wasambazaji wa taarifa hiyo hususani katika mtandao wa facebook wanadai kuwa tunda la nanasi pamoja na matunda mengine kama zabibu hayafai kutumiwa kwa mjamzito hususani katika miezi mitatu ya mwanzo.
Moja kati ya machapisho yanadai kuwa matumizi ya tunda hilo yanasababisha kuharibika kwa mimba na kutoka kwa mimba katika kizazi.


Ufuatiliaji unaonesha kuwa madai hayo si yakweli bali hakuna Uhusiano kati ya matumizi ya nanasi na ongezeko la hatari ya kuharibika kwa mimba hata hivyo, madai mengi yanayounga mkono wazo hili hayana msingi. Uchunguzi wa kisayansi bado haujatoa hitimisho dhahiri linalohusisha kuharibika kwa mimba na kula mananasi. Imani hii inachukuliwa kuwa hadithi ya watu, na hivyo kusababisha kutengwa kwake kutoka kwa lishe ya mama wakati wa ujauzito kwa usalama wa mtoto

Uhalisia kuhusu taarifa hii

Japo ndani ya nanasi kuna kiambata kinachoitwa BROMELAIN ambacho hutumika kutengenezea dawa ya maumivu na kuvimba (ant inflammatory), dawa hii ikitumika kwa mama mjamzito husababisha mimba kuharibika na hairuhusiwi kutumika wakati wa ujuzito.ila kiwango cha kiambata hiki kilichomo kwenye Nanasi ni kidogo sana.Kipo katika kiwango kidogo mno ambacho hakiwezi kuleta madhara yoyote kwa mama mjamzito. Inahitajika ule mananasi 10 kwa wakati mmoja ndo ufikie kiwango cha Bromelain kinachoweza kuleta madhara kwa ujauzito.



Katika kuangazia hilo jedwali kuonesha Lishe ya Mananasi Kwa 100 g
Mananasi ni matunda ya kitropiki yenye ladha tajiri na ya kipekee. Imejazwa na vitamini na madini muhimu ambayo hutoa faida kubwa kiafya. Hii inafanya kuwa nyongeza nzuri kwa lishe ya mwanamke mjamzito. Ifuatayo ni muhtasari wa thamani ya lishe ya mananasi:


VirutubishoKiasi kwa 100 g
Nishati50 kcal
Wanga13g
Nyuzinyuzi1.4 g
Protini0.5g
Mafuta 0.1g
Vitamini Cmiligramu 47.8
Thiamini (Vitamini B1)0.1 mg
Riboflauini (Vitamini B2)0.03 mg
Niasini (Vitamini B3)0.5 mg
Folate (Vitamini B9)18 mcg
Vitamini Avitengo 58 vya kimataifa (IU)
Calcium 13 mg
Potasiamu109 mg

Nini husababisha mimba kutoka


Kwa mujibu wa tovuti ya afya ya Tanzmend, mimba huharibika kutokana na kutokuwepo kwa uwiano wa vichocheo (hormonal inbalance) hasa upungufu wa kichocheo aina ya “progesterone” ambacho ni muhimu sana katika ukuaji wa mimba.

Sababu zingine ni pamoja na uvimbe kwenye kizazi, kulegea kwa shingo ya kizazi, mjamzito kuwa na kinga ya mwili dhaifu, kufanya kazi ngumu na kwa muda mrefu, kupigwa kwa mjamzito kwenye tumbo, utapiamlo na uzito uliopitiliza.

Hivyo basi ulaji wa nanasi wakati wa ujauzito hauna madhara bali ni muhimu kwani nanasi lina kiwango kikubwa cha Madini chuma(iron) na folate ambayo ni muhimu katika kutengeneza damu.Pia nanasi lina vitamini Muhimu zinazohitajika na mama mjamzito.


Ni Wakati Gani kuna Hatari Kubwa?
  • Miezi mitatu ya mwanzo (trimester ya kwanza): Huu ndio wakati hatari zaidi kula nanasi kwa wingi, kwa sababu mimba bado changa na uterasi ni nyeti.
  • Kwa mama mwenye historia ya mimba kuharibika: Hasa kama alishawahi kupoteza mimba kabla ya wiki 12.


Haya ni baadhi Matunda 8 ambayo ni salama kuliwa wakati wa ujauzito ni pamoja na:
1. Apple
2. Guava
3. Parachichi
4. Berries
5. Matunda ya machungwa
6. Embe
7. Tikiti maji
Vyakula 6 ambavyo ni salama kwa matumizi wakati wa ujauzito:
1. Bidhaa za maziwa
2. Mboga za majani meusi kama vile mchicha, kabichi na beetroot
3. Kunde
4. Nyama konda kama samaki, kuku na mayai
5. Nafaka nzima
6. Berries na karanga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom