Namwambia Mungu

Mungu akufanyie wepesi mkuu katika kila jambo.

Usikubali kushindwa anza upya na nguvu mpya ondo negative feelings zote jiandae kushinda kwa kila utakachoanza nacho.
 
Ulichokisema ndio uhalisia kwa niliyoyapitia. Sina mganga Wala mnajimu zaidi ya Mungu mwenyezi na nnaimani atafanya
 
Hujamsoma vizuri.... Kwasababu anasemehe saana kuliko kuhukumu
Usidhani hali mbaya ya uchumi unayopitia ni yako peke yako! Nina muda tangu nimeporomoka na nimeomba sana anisaidie kumbe najilisha upepo

Hamna kitu nilikuwa na imani kukuzidi sema nimekuja gundua haya mambo usipokuwa makini unakufa na umasikini wako hivihivi!

Hizi dini ni project za watu
 
Mwenyewe haeleweki binafsi nimeshamwambie aje hataki nataka nadhani ni Hali yangu ya uchumi
Pole sana, badili mazingira ikiwezekana hata mkoa. Kama haeleweki fanya maamuzi magumu ili umsahau maazima....najua utaumia kwa muda ila with time utazoea na hutaumia tena. Huyo asiyeeleweka anaweza rudi ila akupatie mateso ya kila siku ....ila ukisonga mbele utaumia mara moja mbeleni utapoa.
Kuhusu watoto ni kweli unaumia lakini ukiumia hadi ukifa ndio utawalea?? So ni vyema ufanye maamuzi magumu ila yatakayofaa baadaye.
Kuhusu uchumi Mungu ndio mgawa riziki endelea kumtumaini atakuletea kwa wakati wake, kwa sasa usichague kazi hata ukuli kafanye usongeshe maisha huku ukipigana kutafuta kilicho bora.
Maisha ni mafupi kuyapoteza na maumivu na Majuto....amka jifute vumbi ikimbie hali yoyote inyokurudisha nyuma.
 
At least ungekua mwanasayansi ukajua mambo yanavyoenda na ukabuni kitu chako mwenyewe Kama alivyobuni Mungu ningalikua na wakati mgumu kukuelewesha. Kinyume na hapo Tia Nia moyoni mwako ajidhihirishe kwako umjue.

Kuhusu Nini kilitokea Mungu alinipa uwezo wakumponya mtu ambaye matibabu yake hayakuwezekana hospitalini na punde nilipomuita Mungu alijibu hapo Happ.
Na si Mara moja
 
Ushauri mzuri huu naufanyia kazi
 
Usifike huku. Mungu anahitaji subra na wajbu. Pole saana ndugu yangu
 
Yaani Mungu anakuaje Baba Mlezi!??

Yaani Mungu akiwa Baba Mlezi wewe unaye BABA mwingine si ndiyo?

Naomba nikwambie-Badili mtizamo wako DHIDI ya Bwana Mungu wako..

Sala yako itakuwa hai..

Mungu alikujua wewe kabla hujatungwa Mimba...sasa huyo bado ni Mlezi?

Find yourself and pray again..

God Is and shall HE BE YOUR FATHER FOREVER!
 
Isaya 41: 21, Mungu anasema leta hoja zako zenye nguvu mbele yangu.
Hoja zako ni zipi? Ni kazi? Ni mke kurudi? Ni idea mpya? Ni nguvu ya kuomba tena kwa Mungu? Mshawishi Mungu kwa hoja nzito na uweke maombolezo kando
 
Ahsante kwa ushauri japo Nia yangu Haina tofauti na ulichomaanisha
 
Isaya 41: 21, Mungu anasema leta hoja zako zenye nguvu mbele yangu.
Hoja zako ni zipi? Ni kazi? Ni mke kurudi? Ni idea mpya? Ni nguvu ya kuomba tena kwa Mungu? Mshawishi Mungu kwa hoja nzito na uweke maombolezo kando
Hapa ndipo nimpendapo Mungu... Hallelujah!
 
Mungu na akusamehe maana hujui ulitendalo
 
Mnh.... What a Coicedence....!!!! Mkuu Kweli Duniani wawili wawili... Na Mimi natembea katika Njia hiyo hiyo.... Tafadhali tusife Moyo. Leo Asubuhi nimejitazama kwenye Kioo nikajiambia Lazima Lengo la kuja Duniani Litimie.....!!!! Tutavuka... Never Stop The Race.....!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…