Namuunga mkono Prof. Palamagamba Kabudi

Namuunga mkono Prof. Palamagamba Kabudi

kakuruvi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2009
Posts
770
Reaction score
259
Katika kusoma kwangu neno leo nimekuta andiko hili.

1 Samweli 2 8
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.

Ni baada ya kusoma haya nikakumbuka kundi kubwa la watu liliibuka ambalo hawakumwelewa Prof. Kabudi aliposema utawala umemtoa jalalani. Walimsema sana, wakamsimanga, wakamshusha. Lakini kumbukeni Prof. Kabudi ni miongoni mwa wanataaluma ambao nyuma yao kuna watu wengi pia wanaoheshimika.

Nakumbuka pia hata Rais mstaafu Mzee Mwinyi ambaye wengi tunamtambua kuwa mwenye hekima na hotuba zake zikiwa zinabebwa na wingi wa hazina wa tamathali za semi aliwahi kusema katika hutuba yake ya kushukuru kuchaguliwa kuwa Rais wa JMT, nanukuu''Mimi ukinilinganisha na Mwalimu ni kama Kichuguu na mlima Kilimanjaro ''.''Mimi na Mwalimu ni kama Jahazi mbele ya Manowari''.Mwisho wa kunukuu. Naye pia walidharau maneno yake.

Asikuambie mtu kupata uteuzi wa mamlaka hakuna asiyehitaji imtokee hata waliobeza maneno mazuri ya unyenyekevu yahekima wanatamani leo kupata kuinuliwa kama walivyoinuliwa Wazee hawa na wamefanya kazi nzuri na nchi yetu imefaidika.

Endeleeni kubeza Prof. anazidi kulitumikia Taifa.
 
KWA AKILI YAKO UNAJUA ALIKUWA JALALANI KWELI YAAN KWENYE MAUCHAFU HAKUWA NA KAZI YA KUFANYA WATU WABONGO TUNABIDI TUWE MUSEUM KWA MAANA HUKU UPSTAIR NI MBOMBO NGAFU
 
KWA AKILI YAKO UNAJUA ALIKUWA JALALANI KWELI YAAN KWENYE MAUCHAFU HAKUWA NA KAZI YA KUFANYA WATU WABONGO TUNABIDI TUWE MUSEUM KWA MAANA HUKU UPSTAIR NI MBOMBO NGAFU

We unaona sawa profesa kuita UDSM jalalani?

Kenge mkubwa!
 
Mkuu hata kama ni kujishusha huwezi sema ulikuwa jalalani...
Mwinyi alisema yeye ni kichuguu..kichuguu kina thamani ni nyumba ya mchwa. Kichuguu kina faida lukuki..ila jalalani alidharau kila kitu chake kuanzia wazazi ukoo mzima na elimu ya Tanzania yoote
 
Ni maneno ya tafsida na hekima wachache wataelewa
 
Naungana nawe. Prof Kabudi ni miongoni mwa wazalendo wa kweli nchini. Tutafurahi ikimpendeza Mheshimiwa Rais akamateua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje
 
Lugha za kebehi si nzuri, kuna wenzako waliwaita Viongozi wenye mamlaka Washamba, kawaulize leo watakuambia Mshamba ni nani?

Wenzangu wapi, wewe pia ni mshamba uliyechangamka!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom