Katika kusoma kwangu neno leo nimekuta andiko hili.
1 Samweli 2 8
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
Ni baada ya kusoma haya nikakumbuka kundi kubwa la watu liliibuka ambalo hawakumwelewa Prof. Kabudi aliposema utawala umemtoa jalalani. Walimsema sana, wakamsimanga, wakamshusha. Lakini kumbukeni Prof. Kabudi ni miongoni mwa wanataaluma ambao nyuma yao kuna watu wengi pia wanaoheshimika.
Nakumbuka pia hata Rais mstaafu Mzee Mwinyi ambaye wengi tunamtambua kuwa mwenye hekima na hotuba zake zikiwa zinabebwa na wingi wa hazina wa tamathali za semi aliwahi kusema katika hutuba yake ya kushukuru kuchaguliwa kuwa Rais wa JMT, nanukuu''Mimi ukinilinganisha na Mwalimu ni kama Kichuguu na mlima Kilimanjaro ''.''Mimi na Mwalimu ni kama Jahazi mbele ya Manowari''.Mwisho wa kunukuu. Naye pia walidharau maneno yake.
Asikuambie mtu kupata uteuzi wa mamlaka hakuna asiyehitaji imtokee hata waliobeza maneno mazuri ya unyenyekevu yahekima wanatamani leo kupata kuinuliwa kama walivyoinuliwa Wazee hawa na wamefanya kazi nzuri na nchi yetu imefaidika.
Endeleeni kubeza Prof. anazidi kulitumikia Taifa.