Kauli ya Kabudi ni sahihi, ila alishindwa kuiwakilisha kwa usahihi na kwa mhusika sahihi

soine

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,113
2,329
Ukisoma kitabu cha 1 Samweli 2:8 kinasema:

"Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake".

Kabudi ni mtoto wa Mchungaji, yumkini alikulia kwenye malezi ya kufundishwa neno la Mungu, hivyo haya maandiko huenda aliyasoma au kukaririshwa kama mtoto wa Mchungaji au mkristo.

Tatizo sijui ni matumizi na chaguzi ya maneno, huenda jaani inabeba maana ya jalalani, mavumbini ni mavumbini, Mh. Rais kachukua nafasi ya Mwenyenzi Mungu.

Kabudi kupata bahati ya kuwa mbunge na waziri na inampa fursa ya kukaa ktk vikao na Mh. Rais, mawaziri, na wabunge wenzake...hii ndio kuketi na wakuu anayoisema (ingawa kuwa Udsm alikuwa na fursa hiyo ila sio sawa na sasa).

Professor kabudi nahisi kaonja utamu wa cheo, na hili linampa kuwa humble kunakovuka mipaka ya heshima yake kwenye jamii na nafasi ya Muumba wake.

Nimewaza tu kwa sauti
 
Back
Top Bottom