BWANANDUGU
Member
- Jan 1, 2014
- 28
- 6
Kwanza tujiulize tofauti iliyopo kati ya uoga na unyonge. Rais angewaambia wana CCM waache uoga,hata mm ningepata wasiwasi,ila unyonge,sioni jambo la kutisha hapo. Mtu mnyonge huwa ana kiu ya haki,muoga ana kiu ya damu. Mnyonge halipi kisasi unyonge ukimuisha bali hufurahi kuipata haki yake,muoga atalipa kisasi. Unyonge humfanya mtu kukosa uwezo wa kuzungumza,unyonge ni ukimya usio na majibu. WanaCCM popote tulipo,umefika wakati wa kukipigania chama,wakati wa kuwaambia wapinzani wetu sisi ndio waasisi wa demokrasia na wajuzi wa siasa. Ushindi wa kata 23 kwenye siasa za ushindani hapa nchini sii haba..ni vema sasa tukaongeza juhudi kwenye mapambano ya hoja. Honge Mwenyekiti,tuko nyuma yako.