Namuunga mkono Hamad Rashid, juu ya ku-regulate shule za private | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namuunga mkono Hamad Rashid, juu ya ku-regulate shule za private

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Feb 11, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Niliwahi kuchangia thrad moja humu kuwa kama tunataka kuboresha shule za serikali, basi tufute shule za private.
  Hata hivo ninapotafakari uwezekano wa kufuta shule hizi, nahisi sio jambo rahisi ingawa ni zuri.

  Juzi nilimsikiliza Mh Hamad Rashid akichangia, na nikaona wazo lake juu ya kutatua ubovu wa viwango vya shule za serikali. Binafsi, namuunga mkono, kama nitakuwa nilimuelewa vizuri

  Tatizo
  Tatizo la uduni wa viwango vya shule za serikali pamoja na mambo mengine mengi, linachangiwa sana na uwepo wa shule za private, ambazo hazidhibitiwi. Kama nilivyoeleza awali kuwa hii inasababisha kuwapo kwa hali kuwa wadau karibia wote wa elimu, ukianza na wanasiasa, viongozi watendaji na walimu wanakuwa wakiwasomesha watoto wao katika Shule private. Ni wazi kuwa katika hali kama hii kunakuwa hakuna mwenye uchungu sana na shule za serikali, miongoni mwa hawa ambao, kwa kiasi kikubwa wanategemewa katika kuchangia kuboreshwa kwa shule za serikali.

  Wazo la Hamad
  Kwa jinsi nilivyomuelewa Hamad, ni kuwa shule za private ziendelee kuwepo lakini zichangie maendeleo ya shule za serikali. Kwa maana hiyo, kama mtu anaona kuwa ana uwezo wa kumpeleka mwanae private, then indirectly achangie mfuko wa kuendeleza gov. schools. Hii inawezekana kwa mfano ukiwekwa utaratibu kuwa asilimia hamsini ya malipo yeyote yanayolipwa na mwanafunzi katika shule ya private yanakwenda kwenye mfuko wa kuboresha shule za serikali.

  Faida yake
  - Shule za serikali zitaendeleza haraka zaidi kwani zitapata mchango wa nyongeza
  - Baadhi ya wadau wa elimu (walimu, watendaji wa serikali, na wanachi wengine), ambao awali walikuwa wanapeleka watoto wao kwenye shule za private, watalazimika kuepuka gharama na kupeleka watoto wao kwenye shule za serikali. Kwa kufanya hivi, kwa uwezo wao wa 'hali' na 'mali' wadau hawa watachangia maendeleo za shule hizi zaidi kwani watakuwa na uchungu zazo

  Hasara zake
  - Gharama za shule za private zitakuwa juu
  - Upo uwezekano wa hiyo michango kwenda shule za serikali kuishia mifukoni mwa mafisadi wachache

  Pamoja na hasara nilizozitaja hapo juu, bado naamini itakuwa muafaka kwa kuanzia, uwepo udhibiti wa namna hiyo wakati tukielekea katika sera ya kukataza kabisa shule za private katika ngazi ya primary na sekondari. Nimewahi kutembelea nchi ambazo shule za private haziruhusiwa, na huko perfomance ya shule za serikali ni ya kuridhisha...
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
   
 3. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Shule za kata zifeli alafu lawama zidondokee shule za private.
   
 4. J Rated

  J Rated JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  asichojua hamad rashid ni kuwa asilimia kubwa ya shule za private zinamilikiwa na wanasiasa..
   
 5. O

  Old ManIF Senior Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana lolote huyu pengine anachuki na mtu mwenye shule binafsi, sasa anataka kupata sababu ya kumkomoa, eti kuelekea kufuta shule binafsi, du! Labda wakafanye hayo huko ZNZ kwao si Tanganyika.
   
 6. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Naomba niseme kuwa pamoja na udhaifu wa serikali, lakini tatizo la shule za serikali halitatatuliwa na serikali peke yake, bali na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wazazi. Mojawapo ya namna ya kuwafanya wadau hawa washiriki kwa moyo mmoja katika kusaidia hizi shule, ni kwa kujenga mazingira ya kuwafanya watoto wao wasome katika hizo shule. Wewe fikiria mtoto wa mwalimu, wa diwani, wa afisa mtendaji, wa afisa elimu, wa mkurugenzi, wa mkuu wa wilaya, na hata wa mzazi mwenye 'uwezo zaidi' kimaisha. wooote, wanasoma private. Hawa watu kwa vyovyote vile ndio wanaotakiwa wapange na kutekeleza mikakati ya kuboresha hizi shule za serikali. Lakini watoto wao hawako pale, why should they insist?
   
 7. Lengeri

  Lengeri Senior Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na asichowekea mkazo ni shule za Pemba zinaongoza kwa kufeli...
   
 8. V

  Vipaji Senior Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hamad Rashid ana ufinyu wa kufikiri hasa katika swala elimu. Ana maono ya shule zile za Zanzibar ambazo hazifiki hata idadi ya shule zilizoko mkoa wa Kilimanjaro.

  Kwanza; Tatitizo sio shule za private ninvyoona mimi wala si waalimu bali ni UFISADI ULIOKIDHIRI. Fedha nyingi za serikali wanalipana mafisadi, kwa ajili ya kuendeshea miradi yao au kwa ajili ya vikao vyao vya BOARD wanavyofanya kila siku bila kuwashirikisha wadau yaani Waalimu, wakati hao walimu wakiteseka kwa mishahara midogo na mazingira yasoyoridhisha. Shule za Private zinakuwa na mafanikio mazuri kwa kuwa zina Waalimu wazuri na pia Waalimu hao wanatunzwa na kulipwa vizuri.

  Pili; Serikali ya CCM na CUF hawataki kusimamia swala zima la ELIMU. Ndiyo maana Wanapenda kupinga hoja ya upinzani hata kama ni ya Msingi. Waboreshe maisha ya Waalimu na mazingira ya shule. Matunda yataonekana. Kama serikali haioni kutoa mihistari kwenye mashule unategemea nini. Baraza la Mitihani linatunga mitihani bila kufanya utafiti wa kuwa Silabasi waliyoitoa imefikia lengo? Upuzi mtupu.
   
 9. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hoja haina nguvu tatizo la kufeli shule za serikali ni utawala mbovu na mamuzi ya wasiasa waboreshe shule za serikali ili zishindane na private na siyo kuua private na haitawezekana kuborehs za serikali. Wakiua private Tanzania bado wazazi watapeleka vijana wao Uganda na Kenya
   
 10. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  total crap... hii inamaana serikali imekufa kifikra na kiuwezo na haiwezekani tena kuifufua, kama mawazo ya hamad ndio haya basi huyu jamaa amefilisika kisiasa zaidi ya mrema anaonesha hana uchungu kabisa na nchi hii kwakuwa kafu wanapata mgao serikali basi.. wenyewe waweke kalio wasubiri mavuno bila kutoa jasho
   
 11. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Shule za private haziusiani kabisa na ubovu wa sekondari kata, ubovu unatokana nautekelazaji mbovu wa sera za elimu uhujumu wa uchumi na mambo mengi ikiwapo kuwazuuumu walimu wetu hela zao. Wazazi kama wazazi wameishajitolea sana ikiwa kushiriki pia kwenye ujenzi wa madarasa, sasa unataka bado waongezewe ada ili hela iendelee kuliwa na wachache!? Mkuu haki jitendee mwenyewe sasa wewe unataka kujizulumu.
   
 12. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu tuulize sisi walimu tunavyoteswa, hebu fikiria mtu unaishi dar mshahara laki 2, hivi kweli mwezi utaumaliza, je utafanya kazi kwa moyo? Je hutakuwa na kitu kingine pembeni ku boost maisha? hebu fikiria hapo una mke na watoto na unasomesha kwa kutegemea huo mshahara hata kama ni wewe sidhani kama utafanya kazi kwa moyo. wa kulaumiwa ni serikali wao wanajirundikia posho na mishahara mikubwa, mwalimu hana hata marupurupu yaani hiyo laki mbili mpaka baada ya mwezi mmoja ndo anapata. Serikali ingefikiria mara mbili. Tatizo si walimu
   
 13. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Shule za private mishahara iko juu, kwa hiyo mwalimu anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa hawazi watoto watakula nini na watasoma wapi? kwa hiyo kazi yake inakuwa ni kufikiria tu jinsi ya kuboresha ufundishaji wake na jinsi ya kuwasaidia wanafunzi. Tatizo nchi yetu siasa zimezidi, Kuchanganya siasa na utaalam ni sumu kubwa, kwani siasa ni uongo mtupu
   
 14. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  ..Sababu zilizosababisha UDA 'ife' kwa madai mengi wakati kuna watu binafsi wanafanya biashara hiyo hiyo ndio kinachoua shule za serikali (kata?).

  ..Shule nyingi za binafsi ni biashara; na mfanyabiashara yeyote makini atahakikisha anapata wateja wengi kadiri iwezekanavyo. Ataboresha mazingira, ataongeza vile visivyopatikana kwingine ili wavutiwe wengi zaidi na wale waliopo wasiondoke.

  ..Kuzifunga hakuna tija. Private schools zina waalimu wale wale waliokuwa trained kwa kutumia mifumo iliopo na zinafuata mitaala na taratibu zinazosimamiwa na serikali hii hii, sawasawa na wale wa shule za serikali. Ila wana morale ya juu zaidi, wanathaminiwa (ieleweke hivyo hivyo), wana motisha, wanatamani kila wakati kufaulisha (kusaidia wanafunzi wao kupata matokeo mazuri).

  ..Njia mojawapo ya kujifunza ni kuangalia mwenzako anafanya nini kupata (au kutopata) mafanikio hayo aliyonayo na aidha kuiga au kuboresha na kufanya tofauti. Wataalamu wapo, tunahitaji utashi wa kisiasa.
   
 15. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,611
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Hizi ni idea za ujamaa ambazo zimesababisha Tanzania imefika hapa ilipo, kwa nini mimi nichangie shule ya serikali wakati mwanangu anakwenda shule binafsi? Why?

  Nitakubaliana na wale wanaosema kwamba shule hizi zinaitaji strong regulation, na hili litasaidia kuondoa shule jina zote za private. Lakini hivyo hivyo shule za serikali zinatakiwa new regulations ambazo itaziongoza.

  Moja ni kupunguza uwiano kati ya mwanafunzi na mwalimu. Kuondoa Mitaala yote na kuandika mitaala ya karne ya 21. Mimi nimesoma PCM pale Azania mtaala wa PCM hamuandai mtu yoyote kushindana hata kwenye ngazi ya uselemala. Tunaitaji more hands on Mtaala. Vile vile baadhi ya shule za serikali zinaweza kuendeshwa in partnership with private sector, hii itazipa shule hizi kipato zaidi.

  Restriction kuhusu walimu wanaofundisha watoto wetu, serikali inatakiwa itafute mchakato ambao utaongeza kipato kwa walimu. Kuvutia watu wengi kuona kama uwalimu ni njia safi ya maisha. Na hili litawezekana kama tutatoa motisha kwa walimu kama vile walimu watengenezewe mfuko wao peke yao wa retirement ambao utahakikisha kwamba wanapata same amount wakiretire plus adjustment on inflation. Wapewe good relocation bonus ili wengine wakubali kwenda mikoani.

  Hakuna gain bila pain, baadhi ya shule zifungwe kabisa. Shut it Down, shule kama Ubungo Jioni, sijui mapambano usiku ni lazima zifutiliwe mbali au zikubali kufanya new application.

  Dawa sio kuchangia pesa shule za serikali, dawa ni kubadilisha the way of doing biz.
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hamad Hawezi kutoa Mawazo Mgando kama haya
   
 17. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii inachekesha kwa kweli!! Yaani ni sawa na wakulima wawili mmoja anatumia kanuni bora za kilimo na anazalisha kwa wingi, na mwingine hatumii kanuni bora za kilimo na anazalisha kidogo, halafu tumkataze wa kwanza ili kumsaidia wa pili!!!! Yaani badala Serikali inakili kinachofanyika katika shule binafsi.... tuamue kuzifunga shule binafsi!!!!...... How can someone think in that way???!!! How insane???!!!
   
 18. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hiyo itakuwa husda. Shule za private hazijazuia serkali kusimamia shule zake vizuri, kumotisha watumishi wake na kuweka nguvu katika ufundishaji. Kuna wakati nilimsikia Afisa elimu wa wilaya akimsihi mwalimu aliye katika shule ya private ahamie serkalini. Argument yake ilikuwa shule za private wanafanyishwa kazi nyingi na ni rahisi kufukuzwa kazi kama hutimizi matakwa yao. Lakini akasema sisi serkalini huwezi kufukuzwa labda uhukumiwe kifungo na mahakama. Sasa kama Afisa elimu anajua serkalini mtu anaachwa afanye lolote. Afundishe asifundishe yote sawa. Leo utawalaumu shule binafsi kwa vile wako strict kuhakikisha mwalimu ana cover syllbus?

  Shule nyingi binafsi zinamhamashisha mwanafunzi kujifunza. Zinajenga urafiki baina ya mwalimu na mwanafunzi kiasi kwamba mwanafunzi anakuwa huru kuuliza na kufuatilia yale yanayomtatiza. hivi hilo ndiyo kosa la shule binafsi? Na wazazi wanavutiwa kupeleka watoto mahali wanapoona panafaa. Serkali wasitafute mchawi ni wao wenyewe. Shule nyingi hazina walimu, zenye walimu hawasimamiwi ipasavyo.

  Ubunifu katika ufundishaji umeuwa kwa vile wakaguzi wako very rigid. Shule binafsi unaruhusiwa kujaribu ufundishaji wako na unaruhusiwa kubuni vitu. Serkalini hadi wizara itoe tamko. Ubunifu ukiuawa mambo yanabaki vile vile mafu.

  Kama kuna shule zina hela check bajeti za serkali. Shule za binafsi zingekuwa na hela kama shule za serkali tungekuwa mbali. Hakuna economization serkalini watu wanafuja. Mara semina zisizo na tija, mali za mashule zinaibwa na kuharibiwa bila mwangalizi. Fedha za ujenzi zinaibiwa ovyo n.k n.k
   
 19. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #19
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Tanzania haina uwezo wa kuwasomesha watoto wote bure? Kufunga shule za private si ufumbuzi wa kuziinua shule za serikali. Kwa kupunguza mashangingi tu, sikwambii posho za vikao vya kila siku, mishahara na pensheni za viongozi, bila ya kuingilia utajiri wa maliasili.
  Shule za serikali zinauliwa na serikali.
   
 20. O

  Old ManIF Senior Member

  #20
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu anakuambia kajenga shule kila kata katika nchi nzima, kwingine anakuambia kata moja ina shule mbili ua zaidi shule ambazo ubora hazina. Unajiuliza kwa nini asingejenga idada ambayo ni nusu ya hizo na fedha iliyo baki akaifanyia maboresho, ubunifu wa priroties zero.
   
Loading...