Namupenda, ananipenda

Namupenda, ananipenda

Kwani kuoa inaoa familia yako au jamii??? Wewe fuata kile moyo wako unakutuma,ukiamua kumuoa binafsi sioni tatizo coz watoto sio tatizo hata kidogo wala hawawezi kuzuia mtu kuoa.Ndoa ni yako wewe na yeye wala sio familia yako wala jamii.Ukitaka kufanya kila jambo kwa kusikiliza jamii na familia yako wanasemaje itafika mahali utashindwa kufanya mambo mengine maishani.
 
mumewe amefariki?kama yupo hai uo ni uzinzi kaka...amaaa kweli mapenz upofu..ila oa ila jiandae kukabiliana na matokeo -
 
Nina miaka 28 sasa, nimesoma mpaka chuo kikuu na shahada ya Business Administration nimeshuhudia jinsi marafiki zangu walivyowakimbilia kina dada wa chuo eti uchumba wakati tunasoma na wengi wao waliishia kubwaga, hali hi ilinikatisha tamaa kabisa na niliapa sitokaa nioe mwanamke alosoma.
sasa imetokea kumpenda dada aliye na watoto 3 aliachika kwa mmewe ananipenda ajabu nami nampenda zaidi, anataka nimuoe, kweli nampenda lakini najiuliza jamii na familia yangu watanielewaje? naomba ushauri wana JF

Katika hili kaka sikiliza moyo wako zaidi. Ila cha muhimu chunguza sana kisa cha kuachika maana watoto watatu ni kuwa dada amekaa na jamaa kwa muda usiopungua miaka saba, akipika na kupakua.
 
Kwani wao ndio wanaooa
Si wewe na moyo wako mmeamua na mmependana
Isitoshe wewe ndo utakayekuwa na maamuzi juu ya hao watoto wa mke wako kama utakaa nao au utafanyaje ni wewe
Wewe fanya maamuzi yako na huyo mke wako mtarajiwa na maamuzi yenu naamini hata wazazi watayaheshimu
(Mhhh sijui ni mimi au kuna mtu kaiba password yangu)

kuna mtu kaiba password yako aiseee........
hapo pagumu mwenzangu watalaka wameachana vipi
je ndoa yao ilikuwaje mtalaka hataleta fujo
je akitaka kuja kuwaona watoto masondi atakuwa tayari kumruhusu
huyo dada yupo tayari kwenda kwenye ndoa nyingine au kwa vile wameachana anatafuta pakujishikiza
mleta mada jaribu kuongea na mkeo mtarajiwa kuhusu malezi ya watoto naona itakuja kuwa tatizo huko mbeleni.......au la tumia msemo ukipenda boga penda na ua lake
 
Last edited by a moderator:
kuliko ununue mti mche uoteshe upalilie hadi uzae matunda sio leo wala kesho.
bora uchukue huo mti ambao ushazaa matunda kabisa
fata moyo wako!
 
kuliko ununue mti mche uoteshe upalilie hadi uzae matunda sio leo wala kesho.
bora uchukue huo mti ambao ushazaa matunda kabisa
fata moyo wako!

nimeipenda kula matunda tu au siyo. Kukuza mti kazi aisee..:majani7:
 
kuna mtu kaiba password yako aiseee........
hapo pagumu mwenzangu watalaka wameachana vipi
je ndoa yao ilikuwaje mtalaka hataleta fujo
je akitaka kuja kuwaona watoto masondi atakuwa tayari kumruhusu
huyo dada yupo tayari kwenda kwenye ndoa nyingine au kwa vile wameachana anatafuta pakujishikiza
mleta mada jaribu kuongea na mkeo mtarajiwa kuhusu malezi ya watoto naona itakuja kuwa tatizo huko mbeleni.......au la tumia msemo ukipenda boga penda na ua lake

Blaki Womani kuna mtu kaiba aise siwezi kucomment hivyo
hapo pagumu sana kwa mwowaji aise na haswa kwa wale watoto na sijui na kama yeye yuko tayari kulea watoto wa mwenzake au ndio kapenda boga na ua lake
 
Last edited by a moderator:
Blaki Womani kuna mtu kaiba aise siwezi kucomment hivyo
hapo pagumu sana kwa mwowaji aise na haswa kwa wale watoto na sijui na kama yeye yuko tayari kulea watoto wa mwenzake au ndio kapenda boga na ua lake

hahahahahaha nani tena samaki wanakuchanganya sana hadi wanaiba sijui kama utarudi salama Erickb52 shahidi.....

binadamu wachache wanapenda kulea watoto wa wenzao aise
mbali na wazazi kukubali wao wenye kuna mambo yakuwekana sawa na pia kuna changamoto za hapa na pale
zitakazopelekea watoto kuteseka kwa ajili ya maamuzi yao
 
Last edited by a moderator:
Nina miaka 28 sasa, nimesoma mpaka chuo kikuu na shahada ya Business Administration nimeshuhudia jinsi marafiki zangu walivyowakimbilia kina dada wa chuo eti uchumba wakati tunasoma na wengi wao waliishia kubwaga, hali hi ilinikatisha tamaa kabisa na niliapa sitokaa nioe mwanamke alosoma.
sasa imetokea kumpenda dada aliye na watoto 3 aliachika kwa mmewe ananipenda ajabu nami nampenda zaidi, anataka nimuoe, kweli nampenda lakini najiuliza jamii na familia yangu watanielewaje? naomba ushauri wana JF

kimbia acha us**ge, afrika hii baab. we jifanye huoni uishie kujitia d*le. nimemaliza
 
kuliko ununue mti mche uoteshe upalilie hadi uzae matunda sio leo wala kesho.
bora uchukue huo mti ambao ushazaa matunda kabisa
fata moyo wako!

hahah, umenikumbusha mmasai alieenda kuchumbia. Siku anakuja kuchukua binti akakuta ana mimba. Mmasai alifurahi! Sheeeh, tayari napandisa mtamba yangu!
 
Unatoka nje ya vigezo vyako. Kigezo ilikuwa mwanamke asiwe msomi. Huyo bi shosti watoto ni bonus tu. Kama kasoma piga chini!
 
Umenielewa vibaya sikuwa na maana hiyo dada'ngu
kwa hiyo mwanamke aliyezaa ni mzoga? kumbuka una dada, shangazi na mama, pia weote ni wanawake!
Je ! labda huyo mwanamke aliyena na hao watoto , akaachika na amepata wa kupendana naye ni dada yako, halafu watu wakamwita mzoga utajisikiaje? Tafadhali usipende kutumia maneno kama hayo kwa wanawake .
 
Mjomba unajaribu kuukumbatia mbuyu, huo ni ujinga mjomba. Ulisema hutaki mwanamke msomi, kwa hiyo huyo hajasoma, ni golikipa. Ana watoto watatu ina maana amekaa na mume miaka isiyopungua 5 kwa hiyo ni mke halali wa huyo mwanaume mwingine. Huyo mwanaume kwa vyovyote atawataka watoto wake walau kuja kuwaona, au mama kwenda kulala kwa huyo mume kusubiria hela ya matumizi. Una uhakika wamepeana talaka? Nini kilichowatenganisha?

My take
Kwa kuwa yeye hajasoma, na kwa kuwa watoto wanahitaji matumizi, na kwa kuwa wewe walau umesoma kidogo na kashahada kako kamoja, huyo anakufanya figa la tatu. Kama ukithibitisha haya yote yapo in your favour, go ahead and listen to your heart
 
Are you a psychopath?
Maana dalili za upsychopathy kwako zaonesha.
Unapenda mamlaka
Unapenda kumiliki
Ukiwa juu na mwanamke yupo chini yako ndio unafeel good.

Na mwanamke mwenye elim, mwenye pesa, mwenye akili timamu hamilikiki.
Ndio maana ukaapa hauto oa mwanamke hasio milikika.
You are weak, unaogopa saiz yako.

Na sasa umempata alio chini yako wa kummiliki.
Kaachika,( ni tatizo kubwa alilonao)
Ana watoto 3, (ni mzigo mkubwa anaubeba na anaitaji mtu wa kumsaidia)
Na pengine elim hana, (ana ziki za kimaisha, anaitaji mtu wa kumlisha).

Hapo unazoa tu kiurahisi na mamlaka yote unapewa bila upinzani.

Haufai kuwa raisi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania maana ungependa wanawake wasipate elim ili wanaume wapate mamlaka.

Hata ukigombea uraisi hamna mtu atakuchagua, watahisi utawakata miguu wote wasiweze kutembea ili uwamiliki, na ndio maana hata hao wanawake huko chuo waliligundua hilo, munatafuta mamlaka,:cheer2::cheer2::cheer2:

Na huyo ulie mpata atadumu na wewe kipindi hiko hiko cha shida, matatizo yake yakipungua atasepa.
 
angekuwa mtoto mmoja kidogo ningekushauli endelea lkn watoto watatu duuuu, itakula kwako, ndoa sio lelemama, baadae hao watoto ndo watakao wavuruga
 
Nina miaka 28 sasa, nimesoma mpaka chuo kikuu na shahada ya Business Administration nimeshuhudia jinsi marafiki zangu walivyowakimbilia kina dada wa chuo eti uchumba wakati tunasoma na wengi wao waliishia kubwaga, hali hi ilinikatisha tamaa kabisa na niliapa sitokaa nioe mwanamke alosoma.
sasa imetokea kumpenda dada aliye na watoto 3 aliachika kwa mmewe ananipenda ajabu nami nampenda zaidi, anataka nimuoe, kweli nampenda lakini najiuliza jamii na familia yangu watanielewaje? naomba ushauri wana JF

We hangaika tu hujui kama ada milioni?
 
Kwakweli haitokua rahisi hata Mimi mwanangu wakiume ndio Mara yake ya kwanza anataka kuanza maisha ananiletea mkwe anawatoto wa3 Mmmm kwakweli sio Siri ntasikia vibayaa sana, na kwa upande wako wewe kaka unampenda sababu hajasoma sana au walokua hawajasoma wamekwisha au hukujua mapema Kama Huyo mama Ana watoto au ulijua ukadhani unaonja halafu basi? Huyo lazima upagawe anaujuzi sana kuliko wewe, sasa nenda nae aste aste usikimbilie kuoa na kinga pia usisahau manake Mara na wewe utawacha wako awe wa4..
 
Duuh simba hali ambacho hajakichinja yeye, sasa ndugu kidume, rijari ingia mawindoni usake chako, sio unasubiri vilivyoachwa na wanaume wenzio, usiwe kama fisi anayekula mizoga
ndugu wote tunakula mizoga kama ulikua hujui, issue ni kwamba hujui fisi yupi ndo alie uacha huo mzog baada ya kuula...word to the brother..ebana kwahiyo unaona bora uzifiche insecurities zako za kua na mwanamke aliye soma ambae ni kijana mwenzio..na kuamua kubaki kwenye comfort zone za huyo mmama mwenye watoto wa tatu? nigga get off ur comfort zone rn go get yourself a life = decent girl hata kama amesoma acha uoga wewe...daaah..get a life brother namna gani hii wewe unafanya enh?..ova..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom