Namupenda, ananipenda

Namupenda, ananipenda

masondi

Member
Joined
Feb 3, 2013
Posts
12
Reaction score
3
Nina miaka 28 sasa, nimesoma mpaka chuo kikuu na shahada ya Business Administration nimeshuhudia jinsi marafiki zangu walivyowakimbilia kina dada wa chuo eti uchumba wakati tunasoma na wengi wao waliishia kubwaga, hali hi ilinikatisha tamaa kabisa na niliapa sitokaa nioe mwanamke alosoma.
sasa imetokea kumpenda dada aliye na watoto 3 aliachika kwa mmewe ananipenda ajabu nami nampenda zaidi, anataka nimuoe, kweli nampenda lakini najiuliza jamii na familia yangu watanielewaje? naomba ushauri wana JF
 
Kwani wao ndio wanaooa
Si wewe na moyo wako mmeamua na mmependana
Isitoshe wewe ndo utakayekuwa na maamuzi juu ya hao watoto wa mke wako kama utakaa nao au utafanyaje ni wewe
Wewe fanya maamuzi yako na huyo mke wako mtarajiwa na maamuzi yenu naamini hata wazazi watayaheshimu
(Mhhh sijui ni mimi au kuna mtu kaiba password yangu)
 
Ungekuwa ndo wewe una watoto je?
Halafu ye hana na unampenda....ungefanyaje.
 
Dah! us2kane mkunga! zingatia myo wako kaka yang...if i waz me shit
 
Duuh simba hali ambacho hajakichinja yeye, sasa ndugu kidume, rijari ingia mawindoni usake chako, sio unasubiri vilivyoachwa na wanaume wenzio, usiwe kama fisi anayekula mizoga
 
Yelewii, watoto 3? wee una wangapi?

Una kifua? Kama unakifua cha panzi usioe
Kuna kila aina ya maneno ya kashfa utayasikia plus baba (wa)mtoto wake kuwa anakuja kusalimu watoto ama wanaongea, utaweza?

Mmependana au wewe ulikuwa na 'Depletion of Love' sasa yule kaja kujaza ile nafasi ilokuwa wazi kwa muda mrefu, hebu jichunguze vizuri.

Nakuona unauvaa mkenge kama si mmamba kiulaini
 
Wanamme waliozalishwa nao ni mizoga?

Duuh simba hali ambacho hajakichinja yeye, sasa ndugu kidume, rijari ingia mawindoni usake chako, sio unasubiri vilivyoachwa na wanaume wenzio, usiwe kama fisi anayekula mizoga
 
Duuh simba hali ambacho hajakichinja yeye, sasa ndugu kidume, rijari ingia mawindoni usake chako, sio unasubiri vilivyoachwa na wanaume wenzio, usiwe kama fisi anayekula mizoga
kwa hiyo mwanamke aliyezaa ni mzoga? kumbuka una dada, shangazi na mama, pia weote ni wanawake!
Je ! labda huyo mwanamke aliyena na hao watoto , akaachika na amepata wa kupendana naye ni dada yako, halafu watu wakamwita mzoga utajisikiaje? Tafadhali usipende kutumia maneno kama hayo kwa wanawake .
 
Masondi , kama umempenda kwa moyo wako, usiangalie mambo mengine.wewe fuata moyo wako unaemaje.
 
Yaweza kuwa kakupenda kwa sababu una uwezo kimaisha na unaweza pia kuwalea wanawe na kaa ukumbuke kwamba ukimuoa huyo kubali kuwatunza pia wanawe kwa kuwa umekuta akiwa na mji wake tayari na uwezi kumtenga yeye na mji wake hivo ukubali kuwa baba wa watoto wake. FIKIRI CHUKUA HATUA
 
Kipenda roho hula nyama mbichi.
::
Mapenzi ni upofu
::
Apendae moyo haoni chongo
::
Kupenda fungo litunzalo siri kama kaburi lifunikavyo maiti.
::
Go ahead ila kumbuka mapenzi ya mwanadamu si jambo la dawamu.
=
 
Duuh simba hali ambacho hajakichinja yeye, sasa ndugu kidume, rijari ingia mawindoni usake chako, sio unasubiri vilivyoachwa na wanaume wenzio, usiwe kama fisi anayekula mizoga

unaweza ukasaka yako na yakakushinda, mwache mwenzeio afanye maaumuzi yake ni na sio wewe.
 
Kama mnapendana nyie oaneni.Unaweza pata asiye na watoto mkaishia ugomvi kila siku.Na hao watoto isiwe ishu kwani wanaweza kuwa ndio msaada wako badae.Kuna watu wanatafuta watoto hata wa kusingiziwa hawapati. Cha msingi wekeni mambo sawa tu kisheria.
 
Nunua nyumba angani na uishi huko na huyo unayempenda lakini si mtaani kwani kwa umri wako huwezi kuhimili mikiki mikiki ya wazabinabina.
Angalia zaidi moyo wako unataka nini na jiulize mara mbili mbili kabla ya kuchukua uamuzi isije ikawa una mapenzi ambayo hujui kesho yake yatakuwaje,inaelekea mama anajua kukupa ile kitu roho inapenda du!ukikutana na mzoefu wa mambo bwana huwa raha sana kijana umedata kabisa!!!!
 
Yelewii, watoto 3? wee una wangapi?

Una kifua? Kama unakifua cha panzi usioe
Kuna kila aina ya maneno ya kashfa utayasikia plus baba (wa)mtoto wake kuwa anakuja kusalimu watoto ama wanaongea, utaweza?

Mmependana au wewe ulikuwa na 'Depletion of Love' sasa yule kaja kujaza ile nafasi ilokuwa wazi kwa muda mrefu, hebu jichunguze vizuri.

Nakuona unauvaa mkenge kama si mmamba kiulaini
Mwenzio tayari ana jibu lake moyoni. Jitahidi ushauri wako usiende kinyume na matarajio yake.
 
wonders shall never end ooooo!

uliapa hutaoa mwanamke alie soma...hii ni ngumu kumesa aisee!
Nawaza nje ya box tuu ... baba wa hao watoto watatu anaweza kuja kumdai mke wake lolz (na je hao watoto ni wa baba mmoja au?)

BTW .... kwa nini utake risk ya kujicomit katika mahusiano ya aina hii kwa umri ulio nao??????
 
Mke ana watoto watatu bado umekomalia hapo hapo???? Sema umetokea kumpenda mama mwenye watoto watatu....... Kweli mapenzi uppofu...
 
Hao watoto watatu wana baba wangapi? Embu tuanzie hapo ili nikusaidie kutegua hiki kitendawili
 
Masondi , kama umempenda kwa moyo wako, usiangalie mambo mengine.wewe fuata moyo wako unaemaje.

http://Lisa ya moyoni haya? yaaaaaaaaaaaaani amefungwa 3 bila dk ya 85 ndio anamwingiza uwanjani mchezaji mahiri, hapa sishauri hata kidogo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom