Umenena vema mkuu, kitila Mkumbo ni mtu makini sana, na siasa zake zilikuwa perfect, laiti asingekuwa na hii kashfa na kwa kupitia CHADEMA angemshinda Savimbi.....lakini wacha tujiulize, kama amekiri usaliti na kuomba msamaha.....hamna jinsi kamati kuu ikajiridhisha naye na kuendelea na uanacham wake? sizungumzii yeye kurudishwa ndani ya kamati kuu na wala sizungumzii msamaha kwa ZZK........! yaani hii yote ni jinsi gani nisivyopenda siasa za ndugu SAVIMBI, siasa za chuki, ushirikina na uadui uliokithiri........naamini Dr. Kitila alishaanza kueleweka kidogo na wana Iramba kuliko aje mtu mwingine ambaye SAVIMBI atajitwalia jimbo kilaini kabisa
Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema aliyetimuliwa hivi karibuni Dr Kitila Mkumbo amemuonya vikali Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba kwamba akae mbali na yeye.
Dr Kitila amedai kushangazwa na machozi ya mamba ya Mwigulu ambaye kwa unafiki mkubwa eti amemsikitikia kwa yaliyomfika.
Dr Kitila amesema siku zote Mwigulu Nchemba amekuwa akimchafua lakini tangu atimuliwe uongozi Chadema Mwigulu amejifanya kumsifu sana na kumhurumia.
Dr Kitila amemuonya Mwigulu kwamba inyeshe mvua au liwake jua ni lazima atamvaa katika uchaguzi wa Ubunge jimbo la Iramba Magharibi ama kupitia Chadema au kwa njia nyingine yoyote.
Dr Kitila amemtaka Mwigulu kutambua kwamba yeye bado ni mwanachama wa Chadema.
sarakasi ni nzuri lakini sio mbele ya mama mkwe.
Iramba ni CCM tu. Vijana wote wameona chadema wababaishaji tu. Huwezi kumtoa NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA TAWALA uchague msaliti sijui hata atapitia chama gani. Sijui chadema hata itamweka nani. In short CDM ina mlima mrefu kupanda Iramba