Namuonea huruma huyu binti

Namuonea huruma huyu binti

Nipo katika mahusiano na huyu binti wa kiiraqwi kwa miaka miwili na ziada sasa. Ki ukweli ananipenda na so far sijaona dalili zozote za kunisaliti.

Kinachonitatiza ni hali yangu kiuchumi. Sina ajira rasmi takribani miaka 6 sasa tangu nimehitimu chuo. Nahishi kwa kuungaunga tu na wala sioni dalili yoyote ya mambo yangu kutulia miaka ya hapa karibuni.

Ni binti anaevutia na anani-push sana tuishi pamoja yaani yale mahusiano rasmi. Kiukweli nampenda lakini nahisi nampotezea muda. Muda wote ambao yupo nami ambae bado nayumba kiuchumi angeweza kumpata mwanaume mwenye uwezo kiuchumi wakaishi pamoja.

Nataka nimuache ila nafsi inanisuta kwa sababu hajanikosea chochote.
Umuache ili umpotezee muda rasmi sasa sio!??
 
Nchi hii ina uhaba wa vijana! Umeshamwuliza yeye akakujibuje? Kama kuishi na wewe anaona fresh tu hama mjini urudi kijijini ukapige jembe mkuu huyo ndiye mke mwema!
 
Hela tunatafuta mkuu. Changamoto kaumbiwa binadamu zinakuja kitofauti tu hata wenye hela wana changamoto zao. Kama ramani zinasomeka upande huo tupeane connection.
Kama una mpango wa kuoa kwa mwanamume hakuna short cut lazima uwe na chanzo cha mapato (kujiajiri/kuajiriwa) kuitunza familia yako
 
Nakuelewa sana lakini unaishi maisha halisi kwa maana kwamba anajua haki yako na huja fake maisha, pima moyo wako Nje ya vyote ndo chaguo lako?

Hapa wengi tutakukejeli lkn balaa la ajira Acha tu.

Niliwahi tamani kumwacha aende lkn yeye alisema tupambane Namshukuru Mungu maisha yameleta mwanga kidogo na ni mwaka wa nane sasa katika ndoa.

Sikiliza moyo mengine mtapambana tu Mkuu.
 
Kama una mpango wa kuoa kwa mwanamume hakuna short cut lazima uwe na chanzo cha mapato (kujiajiri/kuajiriwa) kuitunza familia yako
Shida kwa jamii yetu ukiangalia muda unaotumia kusoma unajikuta umeingia mtaani tayari una mentality ya kuwa kwenye mahusiano na kimaisha ndio unaanza moja. Hapo kama hauna connection basi uwe competency sana kwenye field yako yaani uwe kipaji maalumu
 
Najua lazima nitajuta na nishajiandaa kisaikolojia lakini iyo ni kwa upande wangu vipi kuhusu yeye mkuu, huoni kama nampotezea muda
Unampotezea muda kutoka muda gani mpaka muda upi,,,,hayo kupoteza muda alitakiwa alalamike huyo mwanamke Asa wewe tena mtoto wa kiume umeanza kulalama jitafakari upya

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Nimejaribu kujiajiri mara kadhaa lakini niliishia kufeli changamoto kubwa za kujiajiri zinazonikwamisha ni mtaji, kukosa uzoefu/ujuzi wa biashara, utunzaji wa hela na tatizo la kiafya(nina shida kidogo ya kusikia vizuri ni ngumu kuwa sharp kwenye biashara mfano kuwasiliana na watu kwa haraka, kutumia simu kwa mawasiliano n.k)
Jiajiri, weka msaidizi atakayefaa kuwasiliana na wateja, wewe utakuwa msimamizi, pia kilimo na ufugaji, havihitaji sana kusikia.
 
Shida kwa jamii yetu ukiangalia muda unaotumia kusoma unajikuta umeingia mtaani tayari una mentality ya kuwa kwenye mahusiano na kimaisha ndio unaanza moja. Hapo kama hauna connection basi uwe competency sana kwenye field yako yaani uwe kipaji maalumu
Mtoa mada ulisoma fani gani?
 
Pamoja na ushauri tunaotoa, kama mtu ana connection ya ajira popote, tumsaidie mtoa mada, maana humu jamvini pengine kuna waajiri humu, tumpe ajira hata kama haiendani na fani aliyosoma.
 
Back
Top Bottom