Namuona PM Kassim Majaliwa mbali sana

alumn

JF-Expert Member
Jul 15, 2018
2,366
3,109
Wasaalam ndugu wana Jamhuri ya JF.

Nawapenda sana ndugu zangu pamoja na Mara kadhaa kupishana kimisimamo na kiitikadi lakini ni Imani yangu Tungali na Umoja na Mshikamo Mkubwa Baina yetu tena Mkubwa sana, ni wachache wanaotaka kuturudisha Nyuma lakini abadani Tutasonga Mbele.

Leo na Mimi naomba niwajuze ndugu zangu juu ya ndugu Waziri Mkuu wetu Bwana KASSIM MAJALIWA KASSIM. Huyu Bwana kwa jicho la pili namuona mbali sana kwenye duru za kisiasa hasa Uongozi wa juu kabisa wa Nchi yetu kwa badae.

Kwa nini nasema hivyo ni kwa sababu hizi:

Ni kiongozi mwenye misimamo thabiti na isiyoyumbishwa kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Sijawahi kuwa nae kwa ukaribu wala hanijui ila ni imani yangu walio karibu nae ni mashahidi wa hili.

Ni Kiongozi mwenye uono wa kiutendaji zaidi na kiuwajibikaji zaidi kuliko maneno maneno yasiyo na vitendo kama ilivyo kwa baadhi ya watendaji ndani ya Uongozi wa Kiserikari.

Na mwisho ila sio Tamati ni Kiongozi Jasiri, shupavu na thabiti katika kutekeleza Adhima ya Serikari katika kuboresha mifumo ya kiuongozi na Thabiti katika kusimamia rasilimali za Taifa Hili kwa ufanisi usio na shaka.

Natambua kwa wapigaji, wenye maono ya kibinafsi na wasiopenda kua katika mstari ulionyooka hawatakubaliana nami na itakua sio maono mazuri Kwao ila ukweli usio na shaka ni kweli kama Taifa ili Tuendelee tunahitaji kiongozi Msimamizi, Mfatiliaji, na Mwajibishaji huku akizingatia mahitaji ya wananchi kwa Usawa na Haki.

Mama yetu Samia Suluhu Hassan Binafsi ninakupenda natambua wewe unajua zaidi ila kua Karibu na Mtendaji Wako Mkuu wa Shughuli za Kiserikari ni Imani yangu Atakusaidia Pakubwa kutekeleza maono uliyonayo.

Mawazo ya Mungu si sawa na ya Mwanadamu. Ila ni Imani yangu Ana kitu cha kipekee sana. Niwatakie usiku Mwema Wapambanaji.
 
alumn uzi wako nakutumia kupima upepo, subiri wale wanaoamini kuwa "neema kutoka Msoga part Ii" itamwagika watakavyotema you hapa, stay tuned!
 
Taarifa iliyopo tu.

CAG Ndugai HK n.k matamko yao yakikuwa yanaleta kizunguzungu masikioni mda watu.

Ila alipotamka KMK leo kila mtu amemuelewa na wamemwamini kuliko hata huyo CAG na makaratasi yake.

So KMK anasikika vizuri sana.
 
Waziri Mkuu gani Mwongo danganya Wazee wa watu tena Msikitini siku ya Ijumaa bila hata kuwarudia na kuwaomba radhi

Mkuu ni sehem ya maisha ya Binadamu kukosea, huwezi hukumu Mtu kila wakati kwa Jambo moja lililopita. Samehe songa mbele.

Sote tunamapungufu
 
Kama Hayati Magufuli alimuamini katika vipindi vyote viwili vya utawala wake basi nasisitiza aongezewe ulinzi atatufaa huko mbeleni.
 
Wasaalam ndugu wana Jamhuri ya JF.

Nawapenda sana ndugu zangu pamoja na Mara kadhaa kupishana kimisimamo na kiitikadi lakini ni Imani yangu Tungali na Umoja na Mshikamo Mkubwa Baina yetu tena Mkubwa sana, ni wachache wanaotaka kuturudisha Nyuma lakini abadani Tutasonga Mbele.

Leo na Mimi naomba niwajuze ndugu zangu juu ya ndugu Waziri Mkuu wetu Bwana KASSIM MAJALIWA KASSIM. Huyu Bwana kwa jicho la pili namuona mbali sana kwenye duru za kisiasa hasa Uongozi wa juu kabisa wa Nchi yetu kwa badae.

Kwa nini nasema hivyo ni kwa sababu hizi:

Ni kiongozi mwenye misimamo thabiti na isiyoyumbishwa kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Sijawahi kuwa nae kwa ukaribu wala hanijui ila ni imani yangu walio karibu nae ni mashahidi wa hili.

Ni Kiongozi mwenye uono wa kiutendaji zaidi na kiuwajibikaji zaidi kuliko maneno maneno yasiyo na vitendo kama ilivyo kwa baadhi ya watendaji ndani ya Uongozi wa Kiserikari.

Na mwisho ila sio Tamati ni Kiongozi Jasiri, shupavu na thabiti katika kutekeleza Adhima ya Serikari katika kuboresha mifumo ya kiuongozi na Thabiti katika kusimamia rasilimali za Taifa Hili kwa ufanisi usio na shaka.

Natambua kwa wapigaji, wenye maono ya kibinafsi na wasiopenda kua katika mstari ulionyooka hawatakubaliana nami na itakua sio maono mazuri Kwao ila ukweli usio na shaka ni kweli kama Taifa ili Tuendelee tunahitaji kiongozi Msimamizi, Mfatiliaji, na Mwajibishaji huku akizingatia mahitaji ya wananchi kwa Usawa na Haki.

Mama yetu Samia Suluhu Hassan Binafsi ninakupenda natambua wewe unajua zaidi ila kua Karibu na Mtendaji Wako Mkuu wa Shughuli za Kiserikari ni Imani yangu Atakusaidia Pakubwa kutekeleza maono uliyonayo.

Mawazo ya Mungu si sawa na ya Mwanadamu. Ila ni Imani yangu Ana kitu cha kipekee sana. Niwatakie usiku Mwema Wapambanaji.
Wale wanaopita pita kwa ajili ya 2025 si walishaambiwa waache?
 
Back
Top Bottom