Namuona Mchengerwa akifika mbali sana kiuongozi kutokana na uchapa kazi wake

Hivi hizi CHANGAMOTO zinazozikabili nchi huwa huzioni? Or hazipo kwenye job description yako?..maana wewe kutwa ni MAPAMBIO tu

Kama kweli u kijana MZALENDO kama unavyojiita,baadhi ya siku ungekuwa unaziongelea hizi changamoto na hata kutoa USHAURI wa nini cha kufanya

Kwa kukutajia machache
- Janga la UMEME
-Ukosefu wa Maji hata maeneo yaliyo kandokando ya Maziwa na mito
-Ongezeko la mara kwa mara la bei ya MAFUTA
-Sakata la ndugu zetu wa Ngorongoro
-Ukosefu mkubwa wa Ajira kwa vijana wetu
Hayo hayaoni wala hawezi kuongelea. Ni masifu tu hata kwenye upuuzi hadi anatia kinyaa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Tuseme ukweli tu ndugu zangu kuwa Mchengerwa ni mchapa kazi sana, Ni Jembe kwelikweli, Ni hadhina kwa Taifa ,Ni Nyota inayong'aa kwa kasi, Ni kiongozi mwenye kiu ya kutaka kuona wananchi wanapata huduma iliyo bora,wanapata haki,wanatendewa haki, wanasikilizwa,wanapokewa vizuri maofisini na kuhudumiwa vizurii sana. Ukiangalia ni kiongozi ambaye amefanya vizuri na kuacha alama katika kila wizara aliyopita .sote tunakumbuka namna watumishi wa umma walivyosikitika alipo hamishwa kutoka Utumishi.

Ni kiongozi mwenye ari ya kazi na anayejituma sana,ni kiongozi ambaye hasubiri kusukumwa au kukumbushwa majukumu na wajibu wake na Ni kiongozi jasiri na anayejiamini sana.Namuona kama hadhina kwa Taifa letu katika masuala ya uongozi na Namuona akifika mbali sana kiuongozi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Yani mtu kama wewe usiyeweza kuelezea matatizo ya wananchi na kubaki kusifiasifia na kujikomba kwa kila kiongozi utasaidia ninj kwenye uongozi sasa maana inaonekana una njaa kali sana. Disgrace to the youth of Tanzania.
 
Narudia tena kukwambia kuwa acha kumchafua mh Rais wetu. Acha kuandika vitu ambavyo huna hata ushahidi navyo zaidi ya kupotosha tu.
Kama napotosha mwambie huyo mama Abdul ajibu hoja za Bandari badala ya kuseme eti anakaa kimya, ameziba masikio. Rais asiyewaheshimu wananchi hafai kuwa madarakani! Unajua uhusianao wake na huyo mwanamke aliyemteua kuwa balizo wa nchi huko OMAN? Unawajua ndugu gani wa damu wa Samia wanaishi huko Oman? Upofu wako ndio unakushawishi kudhani kuwa haya yote sio Kweli!!!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Tuseme ukweli tu ndugu zangu kuwa Mchengerwa ni mchapa kazi sana, Ni Jembe kwelikweli, Ni hadhina kwa Taifa ,Ni Nyota inayong'aa kwa kasi, Ni kiongozi mwenye kiu ya kutaka kuona wananchi wanapata huduma iliyo bora,wanapata haki,wanatendewa haki, wanasikilizwa,wanapokewa vizuri maofisini na kuhudumiwa vizurii sana. Ukiangalia ni kiongozi ambaye amefanya vizuri na kuacha alama katika kila wizara aliyopita .sote tunakumbuka namna watumishi wa umma walivyosikitika alipo hamishwa kutoka Utumishi.

Ni kiongozi mwenye ari ya kazi na anayejituma sana,ni kiongozi ambaye hasubiri kusukumwa au kukumbushwa majukumu na wajibu wake na Ni kiongozi jasiri na anayejiamini sana.Namuona kama hadhina kwa Taifa letu katika masuala ya uongozi na Namuona akifika mbali sana kiuongozi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Kuanzia sasa uache kutumia neno ndugu zangu, hatuna ndugu kichwa maji kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu Watanzania,

Tuseme ukweli tu ndugu zangu kuwa Mchengerwa ni mchapa kazi sana, Ni Jembe kwelikweli, Ni hadhina kwa Taifa ,Ni Nyota inayong'aa kwa kasi, Ni kiongozi mwenye kiu ya kutaka kuona wananchi wanapata huduma iliyo bora,wanapata haki,wanatendewa haki, wanasikilizwa,wanapokewa vizuri maofisini na kuhudumiwa vizurii sana. Ukiangalia ni kiongozi ambaye amefanya vizuri na kuacha alama katika kila wizara aliyopita .sote tunakumbuka namna watumishi wa umma walivyosikitika alipo hamishwa kutoka Utumishi.

Ni kiongozi mwenye ari ya kazi na anayejituma sana,ni kiongozi ambaye hasubiri kusukumwa au kukumbushwa majukumu na wajibu wake na Ni kiongozi jasiri na anayejiamini sana.Namuona kama hadhina kwa Taifa letu katika masuala ya uongozi na Namuona akifika mbali sana kiuongozi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
umeacha kumsifia mama mkewe umeenda kwa mkwe
 
Limeahamia Kwa Mkwe wa Samia.

Ili lionekane linacheza nao wote.

Wewe msengee , Uongozi unaoutafuta hatabikipewa, HAUJUI UUFANYIE NYINYI

andika nyuzi zinazoonyesha Uwezo wako wa Kichwani ukoje !!.

Mjinga Mmoja wewe
 
Nashukuru kwa majibu yako,lakini kuna point unamiss,kwanza sio kweli kwamba hakuna MAZURI yanayofanywa na Serikali,nina amini serikali inayoongozwa na mwanadamu obvious kuna mazuri na makosa itafanya,na huo ndio UBINAMU wenyewe..sasa shida yako wewe huoni hizi changamoto,na unadhani wote wanaozisema sio WAZALENDO..ndio maana nimekushauri uwe unasema na CHANGAMOTO (hizi nilizojitaja ilikuwa mfano tu) na toa SULUHU kama Kijana MSOMI,sio KUSIFUU tu kila siku

Nianze na la UMEME,kwa hili JANGA la UMEME sio dogo kama wewe unavyoliaddress,watu wanataabika..kuna watu bila UMEME hawali na ndio wengi..
Sasa tujiulize wote, KWANINI SASA shida imekuwa KUBWA hivi?..Mbona kipindi cha Magufuli hali ilikuwa nzuri..kama shida ni ongezeka kubwa la watumiaji wa UMEME ndani ya muda mfupi,serikali kupitia Wasomi wetu wa UCHUMI na NISHATI walishindwa kuliona hili(anticipate) na kuja na mikakati ya muda mfupi ,kati na muda mrefu?..ninachoona kwa sasa kila mtu anaongelea bwawa bwawa la Stiglier,lakini hii SULUHU ya muda mrefu..kwa hali ilivyo,kwa sasa UMEME ni JANGA KUBWA,serikali ije na Hatua za muda mfupi kama kununua or kukodisha Majenereta ya kupunguza hili Janga,dunia now ni Kijiji,shirikisha wenzio,shirikisha SEKTA binafsi

Tuje kwenye MAFUTA,hapa napo naona kama UMEPUYANGA..kwa uelewe kuna shida zaidi ya bei ya SOKO..Kuna hili la ufichwaji wa makusudi wa mafuta kila wiki kabla ya tangazo la bei kutoka..hii kukosekana/kufichwa kwa mafuta kwako wewe huoni kwamba ni TATIZO?..na kwa nini stock ya zamani ifichwe na iuzwe kwa bei mpya?.. vyomba ya Udhibiti vipo wapi?

Tuje kwenye bei, hivi unadhani ni sawa Tz kuwa na bei sawa ya MAFUTA na nchi kama Zambia,Malawi (landlocked countries) nini sasa FAIDA ya sisi kuwa na BANDARI?..

Tuje kwenye Bei na mfano wako wa Kenya..ni kweli Kenya Bei ipo juu kidogo,hapa kuna issue ya Value ya hela ya nchi na purcharsing power ya wananchi..ndio maana ukiangalia na huko nchi za Magharibi,bei ni kubwa kwa kuwa purchasing power yao ni kubwa zaidi..kwa hiyo kusema tu bei yetu ni himilivu pasipo kuangalia factors zingine,nadhani sio sawa

Kuhusu Maji,hatusemi kwamba hakuna JITIHADA,ninachosema UWEKEZAJI huo wa muda mrefu,unatoa MAJIBU chanya?..tumekuwa tunaona wakandarasi wakilipwa Mabilion ya hela kwa ajili ya miradi ya Maji,lakini ukipita kwa wananchi hakuna Maji,nenda Mwanza,Musoma ..hata Dar hapo kuna wakati kulikuwa na mradi wa mabomba ya Mchina,je ule mradi ulileta tija?..wale waliosanifu mradi waliwajibika?..miradi hii kwa ujumla imepunguza shida ya maji kama ilitarajiwa? Kwanini?..waliokwamisha wamefanywa nini?..hao wakandarasi feki wamechukuliwa hatua?
Niishie hapa kwanza..
Aisee 👏🏽👏🏽 Natamani ungekuwa kwenye timu ya wanaomshauri Rais. Umeongea vitu vya maana sana.
 
Bro samahani kwa usumbufu lakini. Ulishawahi kupata ajali ya kichwa? Wako katika kuliendeleza Taifa ,mtiifu msomaji.
 
Limeahamia Kwa Mkwe wa Samia.

Ili lionekane linacheza nao wote.

Wewe msengee , Uongozi unaoutafuta hatabikipewa, HAUJUI UUFANYIE NYINYI

andika nyuzi zinazoonyesha Uwezo wako wa Kichwani ukoje !!.

Mjinga Mmoja wewe
Hapana ndugu yangu.mimi nampongeza yeyote yule anayeonekana kufanya kazi nzuri kwa Taifa letu bila kuangalia ni nani .simpongezi mtu kwa misingi ya upendeleo au kutafuta fadhila ya aina yeyote yule.msingi wangu katika kumpongeza mtu umejikita katika uchapa kazi wa mtu.
 
Bro samahani kwa usumbufu lakini. Ulishawahi kupata ajali ya kichwa? Wako katika kuliendeleza Taifa ,mtiifu msomaji.
Mimi siyo mgonjwa wa kichwa wala sijawahi kupata ajali ya kichwa .Hata hivyo mimi ni kama jalala nayepokea kila aina ya kejeli na matusi pasipo kupaniki au kumtusi mtu.maana nikifanya hivyo nitakuwa najidhalilisha tu.Hivyo lazima niwe kiongozi katika kuwaongoza watu humu kutumia lugha za heshima,staha na adabu katika uchangiaji wa mijadala ya humu jukwaani.
 
Back
Top Bottom