Paul Makonda Akutana na Rais Mwinyi Ikulu ya Zanzibar. Ampongeza kwa uchapa kazi wake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu Watanzania,

Napenda kuwataarifu ya kuwa Mh Paul Makonda Katibu wa itikadi,uenezi na mafunzo wa CCM Taifa, mwamba wa siasa za ardhini na mujukwaani, kiongozi jasiri na shupavu,imara na hodari. Kijana anayetajwa kuwa jasiri zaidi kuwahi kutokea katika eneo lote la kusini mwa jangwa la sahara ,ambaye akizungumza Dar Sauti yake inatikisa na kutetemesha Kigoma huko mwisho wa Reli.

Amefika,kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt Hussein Mwinyi Ikulu ya Zanzibar,Ambapo amempongeza kwa uchapa kazi wake uliotukuka katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Lakini pia Mheshimiwa Rais wa Zanzibar amempongeza sana Mheshimiwa Makonda kwa kuchaguliwa kwake na kwa kazi nzuri aliyoanza nayo na anayoendelea kuifanyia katika usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa ilani ya CCM.

Kwa sasa Mwamba yupo visiwani Zanzibar katika kushiriki sherehe za maazimisho ya miaka 60 ya mapinduzi matukufu ya zanzibar.endeleeni kutulia na kufuatilia kinachoendelea huko, maana macho ya Dunia na vyombo vyote vikubwa Vya Habari Duniani vipo na vimeelekeza nguvu zake na rasilimali zake zote katika matukio yanayoendelea huko zanzibar..

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Back
Top Bottom