Namuona Mchengerwa akifika mbali sana kiuongozi kutokana na uchapa kazi wake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
18,081
12,238
Ndugu zangu Watanzania,

Tuseme ukweli tu ndugu zangu kuwa Mchengerwa ni mchapa kazi sana, Ni Jembe kwelikweli, Ni hadhina kwa Taifa ,Ni Nyota inayong'aa kwa kasi, Ni kiongozi mwenye kiu ya kutaka kuona wananchi wanapata huduma iliyo bora,wanapata haki,wanatendewa haki, wanasikilizwa,wanapokewa vizuri maofisini na kuhudumiwa vizurii sana. Ukiangalia ni kiongozi ambaye amefanya vizuri na kuacha alama katika kila wizara aliyopita .sote tunakumbuka namna watumishi wa umma walivyosikitika alipo hamishwa kutoka Utumishi.

Ni kiongozi mwenye ari ya kazi na anayejituma sana,ni kiongozi ambaye hasubiri kusukumwa au kukumbushwa majukumu na wajibu wake na Ni kiongozi jasiri na anayejiamini sana.Namuona kama hadhina kwa Taifa letu katika masuala ya uongozi na Namuona akifika mbali sana kiuongozi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Kanywe nae Chai.
Watanzania tujifunze kuwapa nguvu ya kusonga mbele watu wanaojitoa na kujitolea katika kututumikia watanzania.

Wenye mioyo hiyo ya uchapa kazi ni wachache na wengini wanafanya kazi mpaka wasukumwe na kusimamiwa kwa kila kitu kama watoto wadogo.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Tuseme ukweli tu ndugu zangu kuwa mh mchengerwa ni mchapa kazi sana ,Ni Jembe kwelikweli, Ni hadhina kwa Taifa ,Ni Nyota inayong'aa kwa kasi, Ni kiongozi mwenye kiu ya kutaka kuona wananchi wanapata huduma iliyo bora,wanapata haki,wanatendewa haki, wanasikilizwa,wanapokewa vizuri maofisini na kuhudumiwa vizurii sana. Ukiangalia ni kiongozi ambaye amefanya vizuri na kuacha alama katika kila wizara aliyopita .sote tunakumbuka namna watumishi wa umma walivyosikitika alipo hamishwa kutoka Utumishi.

Ni kiongozi mwenye ari ya kazi na anayejituma sana,ni kiongozi ambaye hasubiri kusukumwa au kukumbushwa majukumu na wajibu wake na Ni kiongozi jasiri na anayejiamini sana.Namuona kama hadhina kwa Taifa letu katika masuala ya uongozi na Namuona akifika mbali sana kiuongozi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Hivi hizi CHANGAMOTO zinazozikabili nchi huwa huzioni? Or hazipo kwenye job description yako?..maana wewe kutwa ni MAPAMBIO tu

Kama kweli u kijana MZALENDO kama unavyojiita,baadhi ya siku ungekuwa unaziongelea hizi changamoto na hata kutoa USHAURI wa nini cha kufanya

Kwa kukutajia machache
- Janga la UMEME
-Ukosefu wa Maji hata maeneo yaliyo kandokando ya Maziwa na mito
-Ongezeko la mara kwa mara la bei ya MAFUTA
-Sakata la ndugu zetu wa Ngorongoro
-Ukosefu mkubwa wa Ajira kwa vijana wetu
 
Masuala ya ajira kwa vijana serikali imetoa maelfu kwa maelfu na itaendelea kutoa kila mwaka kwa kadri hali ya uchumi itakavyokuwa inaruhusu, lakini pia kupitia miradi mbalimbali iliyojengwa imetoa fursa za ajira kwa vijana wengi sana.

Suala la mafuta nafikiri umekurupuka kuandika tu na huna Takwimu sahihi,maana bei ya mafuta iliyopo nchini ni ya wastani ukilinganisha na majirani zetu,hii ndio sababu wakenya wengi sana wanakimbilia Tanzania kununua mafuta kutokana na kuwa Tanzania mafuta bei ni chini sana ukilinganisha na kwao.

Masuala ya maji hapo pia serikali imefanya kazi kubwa ya kuwekeza mabillioni vya pesa katika kuchimba visima virefu kwa mitambo ya kisasa kabisa,lakini pia imesambaza maji mpaka maeneo ya vijijini.nafikiri uliona hata majuzi mh Rais akiwa mkoani Mtwara akizindua miradi mikubwa ya maji. kazi hiyo inaendelea ili kumaliza kabisa maeneo baadhi yaliyobakia bila kufikiwa na huduma hii muhimu kwa wananchi.

Suala la umeme nalo pia linaendelea kushughulikiwa ili kuhakikisha watanzania wanapata umeme muda mwingi ili waendelee na shughuli zao za uzalishaji,ikumbukwe kuwa kutokana na kasi ya ukuaji wa uchumi wetu imepelekea mahitaji ya umeme kuongezeka kila siku na kukua.Hata hivyo serikali inaendelea kufanya jitihada za kuongeza kiwango cha umeme nchini ikiwepo kutumia vyanzo vingine kama vile gas na umeme wa jua katika kuzalisha umeme badala ya kutegemea chanzo kimoja tu cha umeme wa maji.
 
Back
Top Bottom