Namuogopa mke wangu

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298


1)Wanasema si vibaya,nikianza kuchepuka
Rafiki wasema haya,eti wataja nicheka
nami ninaona haya,nikija kugundulika
Mi sitaki kuchepuka,namwogopa mke wangu.

2)Nyumba ndogo eti nzuri,kwangu hijazoeleka
Ndo mana natafakari,janga lisije nifika
Wanasema ni kuzuri,naogopa kuanguka
Mi sitaki kuchepuka,namwogopa mke wangu.

3)Mke ataniheshimu,kama nikiruka ruka
Naona hiyo ni sumu,ninataka kuipika
Tena jambo la haramu,lenye kuvuka mipaka
Mi sitaki kuchepuka,namwogopa mke wangu

4)Nilishampa ahadi,vipi leo kuvunjika
Ndoa ni kama zawadi,toka kwa mola rabuka
Myaka yangu kwa idadi,mbona nimeshapevuka
Mi sitaki kuchepuka,namwagopa mke wangu.

5)Kipi kipya nitapata,nikianza kuchepuka
Hiyo ni tabia tata,kwa shetani ilizuka
Sitaki huko kupita,pataweza zoeleka
Mi sitaki kuchepuka,namwogopa mke wangu.

6)Naogopa yangu ndoa,itaweza kuvunjika
Tena itapata doa,nami nitaaibika
Watu watanikosoa,jambo hilo sitotaka
Mi sitaki kuchepuka,namwogopa mke wangu.

SHAIRI -NAMWOGOPA MKE WANGU
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Unashairi zuri sana tunga lingine juu ya makinikia ili wakupime mkojo
 
we hutaki chepuka,limbwata limekukolea!
kila siku sasita,mkeo hunidumia!
tena bila kuchoka,kiuno hunikatia!

ati hutaki chepuka,uoga umekuvulia
si kwa nyavu wala kwacha,na amani wajisikia!
utumwa si kula kucha,bali meno kutokukata kucha!

siwezi kufa abadani,mkeo simuachi asilani
bora nife na chepuko tandani,kuliko na bia baani!
utamu wake si wapweza,wapita tanga na muheza!
nami kifimbo cheza,taratibu ananimeza!

wao wako themanini,sisi tu arobaini
hesabu sikuipoteza,lazima nitaicheza

chepuko li tamu,tena huliwa kwa hamu!
usijaribu kuita haramu,sifa iso nidhamu!
chepuko si mwanaharamu,bali hutia chachu kwa ndimu
usiliandike kwa karamu,ukafufisha wake utamu
ha ha ha
CHEPUKO SI MWANAHARAMU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom