Namtafuta sana anayewadanganya Mashabiki wa Simba SC kuwa Kaizer Chiefs FC ni 'wepesi' na 'utopolo' mno kama walivyo Yanga SC

Wana 'Hitman' wao Mmoja huyu Yeye katika mipira ya Krosi Mitano Mitatu lazima akuumize na ana uwezo kwa Kukunjuka kwa Kupiga Miwa ( Mashuti ) ya maana kokote pale na ikawa imo.
Hapa ulimaliza.. maana jamaa kapata nafasi 3 na mbili kaweka.
Tshabalala alitoa assist jamaa akakunjuka MUWA wa Hatari sana.
 
Daa nilichelewa kuona hili bandiko, lakini mkuu kile ulichokua umeandika ndio kilichotekea. Basi tena inabidi turudi kujipanga upya kwa michuano ijayo sababu safari ndio imeishia kule bondeni.
 
Kwa kuwafuatilia Kwangu kwa Jicho la Kiufundi naliomba Benchi la Ufundi la Simba SC lifanye Maandalizi makubwa ikiwezekana hata kuliko yale waliyoyafanya ilipocheza na Al Ahly hapa Dar es Salaam.

Wana Winga zao ( Viberenge ) Wawili ambao nina uhakika Siku hiyo akina Kapombe na Tshabalala wajipange kweli kweli kwani 'Jamaa' wanateleza na Chaki hadi hatari.

Wana 'Mido' yao moja hiyo ni 'Fundi' hasa hata huyu Chama wetu anasubiri na anajua kusambaza mipira huku akiichezesha vyema Timu yake vile atakavyo.

Wana 'Hitman' wao Mmoja huyu Yeye katika mipira ya Krosi Mitano Mitatu lazima akuumize na ana uwezo kwa Kukunjuka kwa Kupiga Miwa ( Mashuti ) ya maana kokote pale na ikawa imo.

Hata hivyo Udhaifu wao mkubwa upo sana katika Beki zao za Kati na Beki wao wa Kushoto ambao kama Simba SC itayatumia vyema haya Mapungufu tunaweza Kufanikiwa.

Simba SC tunajisifu kwa Kucheza Pira Biriani ( Mpira Burudani ) ila kwa hawa Kaizer Chiefs FC huu sasa ndiyo Mchezo wao na wakati huku Tanzania tukimsifia Bernard Morrison kwa kuwa na 'Udambwidambwi' huko Kaizer Chiefs FC karibia Wachezaji wao wote ndiyo Mabingwa wa hii tena hasa pale wakiwa wanaongoza.

Ni kweli kwa miaka ya karibuni Kaizer Chiefs FC haijafanya vyema kivile ila tusijisahau kuwa Ligi ya Afrika Kusini ( PSL ) ni Kubwa na inaizidi yetu ya VPL tena kwa mbali mno hivyo hata Kiviwango wapo juu na hili tusilibishie kwani ndiyo Ukweli wenyewe.

Wakati huku Simba SC yetu tunaambiwa Mchezaji anayeoongoza kwa Kuchukua Mshahara mkubwa ni Bernard Morrison 11,000 USD ila katika Klabu ya Kaizer Chiefs Mshahara wa chini ( mwisho ) wa Mchezaji wao nimedokezwa ni 39,000 USD.

Na tukumbuke kuwa Ligi Kuu ya Afrika Kusini ( PSL ) ni miongoni mwa Ligi 'ghali' sana Duniani ndiyo maana hata Wachezaji wao wengi wakitakiwa na Vilabu vikubwa vya Nje huwa hawataki kwenda na wengi Wao husema kama ni Pesa nyingi hata Kwao Afrika Kusini katika Ligi Kuu yao huwa wanalipwa vile vile.

GENTAMYCINE sijaanzisha huu Uzi ili Kuwatisha Simba SC ( ambayo Mimi pia ni Shabiki wake ) ila nimeona nitahadharishe hili mapema tusije kuendelea 'Kudanganyana' halafu tukipata 'Vipigo' mfululizo Johannesburg ( Jozy au Gauteng ) na Dar es Salaam ( Bongo ) tukaanza kutafuta 'Mchawi' wakati ukweli ni kwamba Kudharau, Kubweteka na Kujiamini Kwetu kupitiliza ndizo zitakuwa sababu Kuu.

Yangu ni haya tu kwa hii leo akhsanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Matokeo gani tena unayasubiria?
Yale ya kwa Mkapa...tutampiga mtu 5-0 na kupindua meza...tuliwahi kufanya hivyo miaka kadhaa ya nyuma ...Tulifungwa pale shamba la Bibi 4-0 na timu moja ya Zambia ...tukaenda kwao Zambia tukapindua meza na kuwachapa 5-0 mbele ya Kaunda...tukasonga mbele..
 
Enzi za mkoloni...mpira unachezwa bila kadi nyekundu.. rafu ruksa
 
Upo vizuri kwa uchambuzi Mkuu GENTAMYCINE sio wale wengine washabiki uchwara wasiojua Mpira wao ni kushabikia tu na kutukana hawataki kuanalyse Mpira katika ukweli wake na uhalisia.
 
Yale ya kwa Mkapa...tutampiga mtu 5-0 na kupindua meza...tuliwahi kufanya hivyo miaka kadhaa ya nyuma ...Tulifungwa pale shamba la Bibi 4-0 na timu moja ya Zambia ...tukaenda kwao Zambia tukapindua meza na kuwachapa 5-0 mbele ya Kaunda...tukasonga mbele..
Endelea ( Endeleeni ) tu Kujidanganya.
 
Kwa kuwafuatilia Kwangu kwa Jicho la Kiufundi naliomba Benchi la Ufundi la Simba SC lifanye Maandalizi makubwa ikiwezekana hata kuliko yale waliyoyafanya ilipocheza na Al Ahly hapa Dar es Salaam.

Wana Winga zao ( Viberenge ) Wawili ambao nina uhakika Siku hiyo akina Kapombe na Tshabalala wajipange kweli kweli kwani 'Jamaa' wanateleza na Chaki hadi hatari.

Wana 'Mido' yao moja hiyo ni 'Fundi' hasa hata huyu Chama wetu anasubiri na anajua kusambaza mipira huku akiichezesha vyema Timu yake vile atakavyo.

Wana 'Hitman' wao Mmoja huyu Yeye katika mipira ya Krosi Mitano Mitatu lazima akuumize na ana uwezo kwa Kukunjuka kwa Kupiga Miwa ( Mashuti ) ya maana kokote pale na ikawa imo.

Hata hivyo Udhaifu wao mkubwa upo sana katika Beki zao za Kati na Beki wao wa Kushoto ambao kama Simba SC itayatumia vyema haya Mapungufu tunaweza Kufanikiwa.

Simba SC tunajisifu kwa Kucheza Pira Biriani ( Mpira Burudani ) ila kwa hawa Kaizer Chiefs FC huu sasa ndiyo Mchezo wao na wakati huku Tanzania tukimsifia Bernard Morrison kwa kuwa na 'Udambwidambwi' huko Kaizer Chiefs FC karibia Wachezaji wao wote ndiyo Mabingwa wa hii tena hasa pale wakiwa wanaongoza.

Ni kweli kwa miaka ya karibuni Kaizer Chiefs FC haijafanya vyema kivile ila tusijisahau kuwa Ligi ya Afrika Kusini ( PSL ) ni Kubwa na inaizidi yetu ya VPL tena kwa mbali mno hivyo hata Kiviwango wapo juu na hili tusilibishie kwani ndiyo Ukweli wenyewe.

Wakati huku Simba SC yetu tunaambiwa Mchezaji anayeoongoza kwa Kuchukua Mshahara mkubwa ni Bernard Morrison 11,000 USD ila katika Klabu ya Kaizer Chiefs Mshahara wa chini ( mwisho ) wa Mchezaji wao nimedokezwa ni 39,000 USD.

Na tukumbuke kuwa Ligi Kuu ya Afrika Kusini ( PSL ) ni miongoni mwa Ligi 'ghali' sana Duniani ndiyo maana hata Wachezaji wao wengi wakitakiwa na Vilabu vikubwa vya Nje huwa hawataki kwenda na wengi Wao husema kama ni Pesa nyingi hata Kwao Afrika Kusini katika Ligi Kuu yao huwa wanalipwa vile vile.

GENTAMYCINE sijaanzisha huu Uzi ili Kuwatisha Simba SC ( ambayo Mimi pia ni Shabiki wake ) ila nimeona nitahadharishe hili mapema tusije kuendelea 'Kudanganyana' halafu tukipata 'Vipigo' mfululizo Johannesburg ( Jozy au Gauteng ) na Dar es Salaam ( Bongo ) tukaanza kutafuta 'Mchawi' wakati ukweli ni kwamba Kudharau, Kubweteka na Kujiamini Kwetu kupitiliza ndizo zitakuwa sababu Kuu.

Yangu ni haya tu kwa hii leo akhsanteni.
Hongera uliona mbali
 
We jamaa uandishi wako ni kama 'mjinga mjinga hivi' ila hapana shaka una akili kubwa na fikra pevu sana. Kile alichokisema kimetokea kwa zaidi ya asilimia 85. Anyway simba atashinda kwa mkapa ila sijui kama atafikisha goli 3.

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom