Namtafakari Ndugai kama Spika na Mwanadamu

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Katika maisha, kuna mambo fulani yakitokea ndiyo humthibitisha mtu kama ubinadamu wake ulikuwa umekamilika au mtu huyo hakuufikia utimilifu wa ubinadamu halisi.

Moja ya mambo hayo ni jirani na mwenzako iwe katika kazi, ujirani au undugu anapopatwa na hatari ya kuondokewa kwa uhai wake. Mtu aliyekamilika kabisa katika ubinadamu wake, lazima atafanya kila awezalo ili kuyaokoa maisha ya huyo mwenzako. Na ukiwa kiongozi mwenye ubinadamu uliokamilika, utahangaika maradufu zaidi kuokoa maisha ya mwenzako unayemwongoza.

Ndugai alipokuwa spika, ndiyo wakati Tundu Lisu aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30, na risasi 16 zikiingia mwilini mwake. Spika Ndugai, alikuwa kiongozi wa Tundu Lisu Bungeni. Tundu Lisu alikuwa ni mbunge mwenzake na Ndugai.

Ndugai, siyo tu hakushughulika maradufu kama kiongozi kuokoa maisha ya Tundu Lisu, bali alihangaika kufa na kupona kumnyima Tundu Lisu haki ya matibabu, na haki zake stahiki za pesa ambayo zingeweza kuisaidia familia yake katika kumwuguza mpendwa wao. Ndugai akafikia kumfuta ubunge Tundu Lisu kwa hila.

Yule mwingine tunaambiwa aliwahi kuugua magonjwa ya akili. Kama ni kweli, basi asamehewa kwa sababu ya tatizo hilo la ugonjwa wa akili, lakini walaaniwe waliofahamu kuwa ndugu yetu alikuwa mgonjwa wa akili lakini wakampa nafasi ya juu kabisa, awaongoze walio wazima na wagonjwa wa akili.

Lakini huyu ambaye aliweza kuhangaika kuhakikisha Tundu Lisu hapati haki ya matibabu kwa kuacha kumlipia gharama ya matibabu kama ilivyokuwa stahiki yake, kweli tunaamini alikuwa na ubinadamu kamili au naye ama ubinadamu wake ulikuwa incomplete au naye alikuwa na tatizo la afya ya akili? Maana katika hali ya kawaida, ukiwa na nduguyo, hata kama mlipishana, lakini ikifikia mahali pa huyo mwenzako kuwa katika hatari ya kupoteza maisha, aghalabu unasahau yote, na kuhangaikia kuokoa maisha yake.

Ndugai popote ulipo, hakika kama ubinadamu wako ulikiwa kamili lakini wewe kwa kutaka kumfurahisha shetani, ukaamua kuudunisha, na au ulikuwa na akili timamu lakini kwaajili ya kumfurahisha ibilisi, ukaamua kuiondoa akili, na kuamua kuuabudu upungufu wa akili, ni vema ukiwa bado una pumzi, ufanye tona iliyo kuu na njema, na kwa sababu ulikuwa kiongozi, toba yako ni vema ikawa ya wazi. Hakika, usipofanya hivyo, mimi si mshirika wa Mungu, lakini kwa Roho ile aliyoiweka kwetu, nakuusia, utabeba laana hata ikasambae kwa wana wako, na wana wa wana wako. Neno la Bwana ndivyo lisemavyo.
 
Yule mwingine tunaambiwa aliwahi kuugua magonjwa ya akili. Kama ni kweli, basi asamehewa kwa sababu ya tatizo hilo la ugonjwa wa akili, lakini walaaniwe waliofahamu kuwa ndugu yetu alikuwa mgonjwa wa akili lakini wakampa nafasi ya juu kabisa, awaongoze walio wazima na wagonjwa wa akili.
Wengi wanaamini nikiwemo mm kuwa Ndugai alimfanyia Tundu Lisu unyama huu kwa shinikizo toka kwa huyu mgonjwa wa akili
 

Toba hii ya Ndugai ilikuwa kwa yale aliyomkosea Samia kwa kumshutumu kwa kushobokea mikopo toka nchi za nje. Tukumbuke tu kuwa Ndugai Akiwa spika enzi ya Jiwe aliwakwaza wananchi wengi kwa kutokuiheshimu na kuilinda katiba ya nchi.

Aliwaingiza wanamama 19 kuwa wabunge kinyume kabisa na taratibu za bunge na akakataa kurebisha makosa yake hata pale alipotakiwa kufanya hivyo. Hili kosa linahitaji toba ya peke yake. Asipofanya hivyo laana ya nchi nzima itamuangukia.
 
Tusimuombee mabaya,Bali tupitishe bakuli la michango ili apate matibabu stahiki.

Upendo Tanzania umepungua, hakuna mbunge hata mmoja aliyepeleka hoja binafsi kuiuliza Serekale wapi Ndugai. Alipokuwa kwenye kiti walimupigia makofi.
 
Tusimuombee mabaya,Bali tupitishe bakuli la michango ili apate matibabu stahiki.
Upendo Tz umepungua,Hakuna mbunge hata mmoja aliyepeleka hoja binafsi kuiuliza Serekale wapi Ndugai.Alipokuwa kwenye kiti walimupigia makofi.
kumchangia mtu ni kuonesha upendo na sijui "narudia" sijui kama wapo wanaompenda.
Ile ati ukipigwa shavu la kulia mgeuzie la kushoto hakuna tena

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kuna Sheria ipi Ndugai aliyoivunja kwenye hayo unayoiita malipo ya Tundu Lisu? Tundu Lisu ni millionaire in dollar terms wewe unakuja hapa kupoteza muda wako kumtetea wakati kuna watu Tanzania hawajalipwa mafao ya ustaafu kwa miaka na ni wazee walioitumikia nchi si ajabu hata kwenye familia yako unao, you must be crazy man.

Tundu Lisu analipwa kila mahali mpaka Familia yake kahamishia Ulaya wewe unakwenda kupigania vishilingi ? Kwanza hata Tundu Lisu mwenyewe akikosoma atakushangaa sana, the man is rich, very rich au unafikiri fedha ya kumlipa Jew Amsterdam alikuwa anaitoa wapi ?
 
Back
Top Bottom