Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,395
- 13,266
Huenda aliwaza vizuri lakini utekelezaji wake imekuwa ni karaha kwa wafanya biashara wadogo. Watendaji wa serikali wanatumia nguvu kubwa sana kukazimisha watu kununua vitambulisho hivyo. Sehemu nyingine watumishi wametishiwa hadi kufukuzwa kazi wasipofanikiwa kuuza vitambulisho hivyo.
Hapa ilipaswa kujuliuliza kwanini vitambulisho hivyo havinunuliwi? Jibu ni fupi tu wafanyabiashara wengi wana mitaji midogo sana hivyo kwa lugha nyingine wao ni masikini kabisa. Sasa kwenda kuchukua 20,000/= kwa masikini kwa kisingizio cha kitambulisho hiyo ni sawa uuaji. Ukiangalia baadhi ya wafanyabiashara wanaolazimishwa kununua vitambulisho hivyo mitaji yao ni chini ya 20,000/= halafu analazimishwa kununua kitambulisho cha 20,000/= ambayo hana. Hivi shoe shiner na muuza karanga kwa mfano mitaji yao ni shilingi ngapi hadi walazimishwe kununua kitambulisho?
Kwakuwa hili lilikuwa ni wazo binafsi la rais kama alivyoeleza yeye mwenyewe na kwakuwa ni yeye ndiye aliyevitengeneza na kwakuwa ni yeye ndiye aliyepanga bei namshauri avifute kabisa vitambulisho hivyo kwani vina mshushia hadhi sana miongoni mwa wafanyabiashara wadogo masikini na wananchi kwa ujumla. Vinginevyo ili kuwasaidia ni bora avitoe bure. Ikumbukwe madhara yoyoyte watakayopata wamachinga, watumishi na wananchi kwa ujumla lawama zote zitaelekezwa kwake rais kwakuwa yeye ndiye mwenye vitambulisho hivyo.
Ni vizuri rais ajue kuwa watendaji wake wanafanya kazi kwa nidhamu ya woga sana na kujipendekeza ili kumfurahisha yeye hivyo wanaoumia ni wananchi kutokana na hatua wanazochukua dhidi ya wananchi. Ni watendaji wasioweza kutoa ushauri pale wanapoona mambo magumu zaidi ya kutumia nguvu ili kila mmoja aonekane anaweza.
Sent using Jamii Forums mobile app