mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,573
- 9,809
Prof. Assad ni mtu mcha Mungu kwa imani ya dini yake, muadilifu na msomi mbobevu. Watu kama hawa kwa nchi nyingine zenye taasisi imara huchukuliwa kama sehemu muhimu ya "think tank" ya kuiongoza nchi. Lakini siyo kwa nchi yenye kuendeshwa kwa akili za ki CCM.Pole sana Professa Assad.
Mimi binafsi nilisikitika sana kwa uonevu uliofanyiwa kwa kustaafishwa bado ukiwa hujatimiza umri wako wa kustaafu. Ulisimamia ukweli, ulikuwa mwadilifu na mkweli kwa nchi yako lakini haya yote wakubwa hawakuona na bado wakakukejeli. Kama katiba inavyosema CAG ili kustaafu kwa CAG ni lazima atimize miaka 65 isipokuwa anaweza kustaafishwa kabla ya 65 kama haya yatamtokea. (1) Kama akili yake siyo timamu (2) Kifo (3) vitendo vya kimaadili n.k.
Hivi vyote Professa hakuwa nazo na bado umri wake ulikuwa miaka 58. Huu ni uonevu mkubwa sana kwa wakubwa wa Mamlaka na hivyo mimi ninakushauri uende Mahakamani ili utafute haki yako hata kama hawatakurudisha lakini wajifunze na jambo kama hili lisirudiwe tena.
Soma > Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu
Mtu kama huyu huwezi kutegemea akapate "due respect" kutoka kwa mafisadi na wezi wa mali za umma ambao wamejazana ndani ya CCM. Kila mzalendo mwenye uthubutu wa kutetea rasilimali za nchi hii ni lazima atawekewa zengwe na hata njama za kutaka kummaliza.
Nchi yetu imekuwa ni ya ajabu kabisa, badala ya vyombo vya dola, bunge na mahakama kuwa upande wa wananchi wenye kudhulumiwa na kuonewa, vyote hujitoa ufahamu na kusimamia dhuluma inayofanywa na mahafidhina yaliyojazana ndani ya chama tawala.