Namshauri Professa Assad aende Mahakamani kwa uonevu aliofanyiwa

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Pole sana Professa Assad.

Mimi binafsi nilisikitika sana kwa uonevu uliofanyiwa kwa kustaafishwa bado ukiwa hujatimiza umri wako wa kustaafu. Ulisimamia ukweli, ulikuwa mwadilifu na mkweli kwa nchi yako lakini haya yote wakubwa hawakuona na bado wakakukejeli. Kama katiba inavyosema CAG ili kustaafu kwa CAG ni lazima atimize miaka 65 isipokuwa anaweza kustaafishwa kabla ya 65 kama haya yatamtokea. (1) Kama akili yake siyo timamu (2) Kifo (3) vitendo vya kimaadili n.k.

Hivi vyote Professa hakuwa nazo na bado umri wake ulikuwa miaka 58. Huu ni uonevu mkubwa sana kwa wakubwa wa Mamlaka na hivyo mimi ninakushauri uende Mahakamani ili utafute haki yako hata kama hawatakurudisha lakini wajifunze na jambo kama hili lisirudiwe tena.

Soma > Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu
 
Hiyo namba tatu unaipima vipi? Unajuaje kama alikuwa maadili ya mteuzi wake. Ndiyo maana tunahitaji katiba mpya inayofafanua vitu na siyo ya sasa inayoweka vitu in blankets.
 
M/Mungu alishamuhukumu kubwa la Roho mbaya,Asad Hana Tena sababu ya kwenda MAHAKAMANI, aliyemfanyia ubaya tayari kashaingia kwenye kumi na nane za Mfalme wa Falme, saizi anachezea punishment mwanzo mwisho
 
Kipengere cha kwanza (i) ndiyo kilichomtoa kazini tatizo ni kwamba haelewi yeye mwenyewe kama ana hilo tatizo
 
Pole sana Professa Assad.

Mimi binafsi nilisikitika sana kwa uonevu uliofanyiwa kwa kustaafishwa bado ukiwa hujatimiza umri wako wa kustaafu. Ulisimamia ukweli, ulikuwa mwadilifu na mkweli kwa nchi yako lakini haya yote wakubwa hawakuona na bado wakakukejeli. Kama katiba inavyosema CAG ili kustaafu kwa CAG ni lazima atimize miaka 65 isipokuwa anaweza kustaafishwa kabla ya 65 kama haya yatamtokea. (1) Kama akili yake siyo timamu (2) Kifo (3) vitendo vya kimaadili n.k.

Hivi vyote Professa hakuwa nazo na bado umri wake ulikuwa miaka 58. Huu ni uonevu mkubwa sana kwa wakubwa wa Mamlaka na hivyo mimi ninakushauri uende Mahakamani ili utafute haki yako hata kama hawatakurudisha lakini wajifunze na jambo kama hili lisirudiwe tena.

Soma > Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu
Kwa mahakama zipi hizo?
 
Nchi hii ukiwa mkweli kabisa kabisa existence yako itakuwa kwenye mashaka makubwa!! wengi wanaamua kubakia kimya tu...siku ziende. Ila ki ukweli wapo wengi sana wameumizwa na hawana option nyingine zaidi ya kubakia kimya hadi kaburini.

Unless uchimbe shimo then uongeee yote then ulifukie - kama ile hadithi ya Mfalme mwenye masikio marefu.
 
M/mungu alishamuhukumu kubwa la Roho mbaya,Asad Hana Tena sababu ya kwenda MAHAKAMANI, aliyemfanyia ubaya tayari kashaingia kwenye kumi na nane za Mfalme wa Falme, saizi anachezea punishment mwanzo mwisho

Usitangulize sana hisia zako utakufuru ndugu yangu ,kwa mfano una mzazi wako mmoja kafariki leo itakua kahukumiwa nae au kuna kitu atakua amekosea? Kitu unachotakiwa kujifunza muda huu ni kwamba hakuna mkamilifu ila tunatofautiana kiwango cha ukosefu ,leo hii hata uanguke wewe wapo watakaolia na wapo watakaoshindia k vant kwa raha mpaka asubuhi tafakari
 
Pole sana Professa Assad.

Mimi binafsi nilisikitika sana kwa uonevu uliofanyiwa kwa kustaafishwa bado ukiwa hujatimiza umri wako wa kustaafu. Ulisimamia ukweli, ulikuwa mwadilifu na mkweli kwa nchi yako lakini haya yote wakubwa hawakuona na bado wakakukejeli. Kama katiba inavyosema CAG ili kustaafu kwa CAG ni lazima atimize miaka 65 isipokuwa anaweza kustaafishwa kabla ya 65 kama haya yatamtokea. (1) Kama akili yake siyo timamu (2) Kifo (3) vitendo vya kimaadili n.k.

Hivi vyote Professa hakuwa nazo na bado umri wake ulikuwa miaka 58. Huu ni uonevu mkubwa sana kwa wakubwa wa Mamlaka na hivyo mimi ninakushauri uende Mahakamani ili utafute haki yako hata kama hawatakurudisha lakini wajifunze na jambo kama hili lisirudiwe tena.

Soma > Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu
Unamsifu weee, kumbe bure tu! Aliwezaje kuwa na maadili ktk uongozi wa mtu ambaye hakuwa na maadili? Si alikuwa ni CAG wa Kikwete na safari zake za nje kila siku hadi kupokelewa na wana mziki!

Mtu gani huyu nayelalama kila siku utadhani alisomea kozi ya CAG? Kwani hana kazi nyingine? KIla siku anakuja na jipya kwani wengine nchi hii hawakuachishwa kazi?
 
Pole sana Professa Assad.

Mimi binafsi nilisikitika sana kwa uonevu uliofanyiwa kwa kustaafishwa bado ukiwa hujatimiza umri wako wa kustaafu. Ulisimamia ukweli, ulikuwa mwadilifu na mkweli kwa nchi yako lakini haya yote wakubwa hawakuona na bado wakakukejeli. Kama katiba inavyosema CAG ili kustaafu kwa CAG ni lazima atimize miaka 65 isipokuwa anaweza kustaafishwa kabla ya 65 kama haya yatamtokea. (1) Kama akili yake siyo timamu (2) Kifo (3) vitendo vya kimaadili n.k.

Hivi vyote Professa hakuwa nazo na bado umri wake ulikuwa miaka 58. Huu ni uonevu mkubwa sana kwa wakubwa wa Mamlaka na hivyo mimi ninakushauri uende Mahakamani ili utafute haki yako hata kama hawatakurudisha lakini wajifunze na jambo kama hili lisirudiwe tena.

Soma > Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu
Atajichosha bure tu. "The courts have been compromised".
 
Back
Top Bottom