JT2014
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 1,863
- 1,367
Habari zenu wana jamvi.
Kutokana na dhamira ya rais ya kuikwamua nchi hii kiuchumi namshauri afanye haraka abadilishe fedha yetu, na atoe muda kama miezi sita hivi,fedha yote ya zamani iwe imebadilishwa vinginevyo mmiliki atakuwa ameingia hasara endapo ataendelea kuwa na fedha mkononi bila kuipeleka benki au taasisi nyingine za fedha.
Naamini hii itasaidia kufichua wabadhilifu wa mali za umma waliotumia madaraka yao vibaya na kujilimbikizia mali lakini wanaogopa kutumia taasisi za kifedha ili kuepuka mkono wa dola.
Na hivyo hizo fedha wamezichimbia majumbani na hivyo hazipo kwenye mzunguko wa kuzalisha.
Karibu tujadili,wewe binafsi unashauri nini ili uchumi wetu uinuke na kurudia hali yake.
Asanteni.