Namshauri Mh. Rais abadilishe fedha ya nchi

JT2014

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
1,863
1,367
Habari zenu wana jamvi.

Kutokana na dhamira ya rais ya kuikwamua nchi hii kiuchumi namshauri afanye haraka abadilishe fedha yetu, na atoe muda kama miezi sita hivi,fedha yote ya zamani iwe imebadilishwa vinginevyo mmiliki atakuwa ameingia hasara endapo ataendelea kuwa na fedha mkononi bila kuipeleka benki au taasisi nyingine za fedha.

Naamini hii itasaidia kufichua wabadhilifu wa mali za umma waliotumia madaraka yao vibaya na kujilimbikizia mali lakini wanaogopa kutumia taasisi za kifedha ili kuepuka mkono wa dola.

Na hivyo hizo fedha wamezichimbia majumbani na hivyo hazipo kwenye mzunguko wa kuzalisha.

Karibu tujadili,wewe binafsi unashauri nini ili uchumi wetu uinuke na kurudia hali yake.

Asanteni.
 
Hivi mtu anaweza akakaa na mabilioni ndani?
Ukirudi nyuma kwenye historia kipindi cha mwalimu Nyerere,watu walikuwa na fedha ndani na ilipokuwa inatangazwa kubadilisha fedha ilikuwa mshike mshike.

Lakini wakati wa sakata la escrow utakumbuka ilitajwa kwamba kuna waliobeba fedha kwa viroba,unadhani walikuwa wanapeleka benki gani kama siyo majumbani na kuanza kuzitakatisha taratibu.

Hivyo inawezekani kuwa na mabilioni nyumbani.Inategemea una dhamira gani na mabilioni hayo au njia uliyoitumia kuyapata.
 
JT2014

Watu watajengea majumba na kununua mashamba bila hata hiyo hela kufika benki kwa kutumia mkono wake.
 
Last edited by a moderator:
Kuna ukweli fulani. Muda uwe wiki moja. Nakumbuka wakati wa kubadilisha noti za 500,na 5,000 ilikuwa ni sarakasi tupu,maana noti za zamani unapeleka benki,lakini zilikuwa zinarudi kwenye mzunguko.
 
nataka raisi apige marufuku matumizi ya dola kwenye nchi yetu.Na atakaye kiuka haya akamatwe na kufunguliwa mashtaka kwa kuihujumu nchi.
 
nataka raisi apige marufuku matumizi ya dola kwenye nchi yetu.Na atakaye kiuka haya akamatwe na kufunguliwa mashtaka kwa kuihujumu nchi.

Mkuu dola ndio inatakiwa iwepo Zambia walipiga marufuku iyo dola kama miaka miwili iliyopita sasa imekua Hadimu kweli na rate kwa dola mia mpaka milion na laki tano kwatcha kwa sasa. Sema matumizi ya kuuza tv mlimani city au sahani eti kwa dola hao wapigwe marufuku..
 
Hiyo kitu ikitokea ndani ya wiki kubadili pesa itabidi na wachimba makaburi waongezeke.
 
JT2014

great Idea, iendane na devaluation au kuondoa sifuri moja kwenye fedha yetu.pia iambatane na BAN ya Mauzo yote ya nyumba,viwanja au mali zisizohamishika kwa cash.biashara ha kununua shamba kwa million 20 ufe.ili transfer iwe legal,lazy iambatane na bank slip. Ukijumlisha na ubadilishaji wa fedha Ndani ya wiki moja,mabazazi wanaptutia umaskini watakuwa na Wakati mgumu Sana.
 
Last edited by a moderator:
nataka raisi apige marufuku matumizi ya dola kwenye nchi yetu.Na atakaye kiuka haya akamatwe na kufunguliwa mashtaka kwa kuihujumu nchi.

Sheria za madini na utalii zinahalalisha matumizi ya dollar nchini. Zifutwe kwanza ili tubanane
 
Wazo zuri sana. Hakika kuna mabilioni mengi yapo majumbani mwa watu. Si mnamkumbuka yule waziri wa Zambia alivyobambwa kafukia mahela nyumbani kwake, same apply in tz.
 
JT2014

great Idea, iendane na devaluation au kuondoa sifuri moja kwenye fedha yetu.pia iambatane na BAN ya Mauzo yote ya nyumba,viwanja au mali zisizohamishika kwa cash.biashara ha kununua shamba kwa million 20 ufe.ili transfer iwe legal,lazy iambatane na bank slip. Ukijumlisha na ubadilishaji wa fedha Ndani ya wiki moja,mabazazi wanaptutia umaskini watakuwa na Wakati mgumu Sana.

re-valuations/
is it possible?
don't thinks!
 
Last edited by a moderator:
Ukirudi nyuma kwenye historia kipindi cha mwalimu Nyerere,watu walikuwa na fedha ndani na ilipokuwa inatangazwa kubadilisha fedha ilikuwa mshike mshike.

Lakini wakati wa sakata la escrow utakumbuka ilitajwa kwamba kuna waliobeba fedha kwa viroba,unadhani walikuwa wanapeleka benki gani kama siyo majumbani na kuanza kuzitakatisha taratibu.

Hivyo inawezekani kuwa na mabilioni nyumbani.Inategemea una dhamira gani na mabilioni hayo au njia uliyoitumia kuyapata.
Benard Membe ana handaki kubwa nyumbani kwake amehifadhi Mabilion ya dola za marehemu Gadafi huku zingine akiwa kazificha kwa Jack Gotham rafiki yake mkubwa mmiliki wa Tenda ya vitambulisho vya Taifa, hata Nape, mwigulu na January Makamba , kinana, mangula, Rajab luhavi na wajanja wa CCM waliopiga pesa za kampeni toka China wamezificha ndani Aridhini, wengine wajanja zaidi wamenunua majumba Ulaya, Dubai, South Africa na kufungua biashara kwa majina ya watu mbalimbali, .
 
Wazo zuri sana. Hakika kuna mabilioni mengi yapo majumbani mwa watu. Si mnamkumbuka yule waziri wa Zambia alivyobambwa kafukia mahela nyumbani kwake, same apply in tz.

January Makamba wakati kampeni ikiendelea alipiga billion 1.7 hadi Magufuli akapagawa lakini bahati akina Membe na Jack Gotham wakaenda china kuwatisha kuwa endapo Ukawa watachukua Nchi mikataba yao yote ikiwemo ya bandari ya Bagamoyo itafutwa, ndipo Serikali ya China ikatoa tena Mabilioni ya dola kampeni ikaendelea zikatumika kununua magoli ya mikono, zile Mabilioni zilizosalia zote kinana peke yake alichukua billion 3 kisha zingine wakagawana mzee mangula, Nape, Luhavi, mama zakia na wajanja wengine wa ccm wakiwemo hao hao akina Membe na Jack Gotham ambao pia wana Bank majumbani mwao wamehifadhi Mabilioni ya marehemu Gadafi,
.
 
Pesa aliyoficha Membe na Jack Gotham licha ya kuitumia sana kwenye kampeni kuwadhoofisha ukawa Bado ni nyingi sana, Mabilioni ya dola la marehemu Gadafi, 10% za ununuzi nyumba za balozi huko nje,
 
Kuna ukweli fulani. Muda uwe wiki moja. Nakumbuka wakati wa kubadilisha noti za 500,na 5,000 ilikuwa ni sarakasi tupu,maana noti za zamani unapeleka benki,lakini zilikuwa zinarudi kwenye mzunguko.

Ndiyo maana kipindi kile uchumi uliporomoka sana hawakuwa makini.
 
No, hii haina maana.... kwa uhakika kabisa, kwa Tz ya sasa, hakuna mtu anaweza weka tshs 500,000,000 nyumbani... Hata kama yupo say 1 au 2, huwezi badili FEDHA ya nchi sbb ya watu 2 au 3 hata kama wapo... !!

Kuna njia nyingi za kudhibiti hizo fedha zisizagae mikononi mwa watu... Moja wapo ni FEDHA HARAMU ya Drugs... pili UKWEPAJI KODI MKUBWA... na tatu KUDHIBITI MFUMUKO wa bei, meaning fedha kuwa na VALUE... Grand CORRUPTION etc..

So, No, No... kubadili fedha, umefikiria kwa kifupi sana pua na mdomo..
 
Mkuu watu wenye mapesa majumbani mimi naamini ni wengi sana Tanzania. Hii ni kwa kuwa Watanzania wengi hawana utamaduni wa kutumia benki kutunza pesa zao na pia wezi na wapiga deal wengi hawaweki pesa bank. Pia watu hawaweki pesa bank ilikuficha utajiri walionao!!

Imagine ile story ya watu kubeba pesa kwenye magunia na viroba STANIBC kama ni kweki unafikiri wamezipeleka wapi!!?
 
Back
Top Bottom