Kimsingi Mbowe anapenda sana kulalamika, lakini akumbuke kwamba alisema wamemchukua Lowasa kwani ndo anajua wizi wa ccm, mbona tena anatapatapa?
Na wao wataangaika sana, kwani Mwl.Nyerere aliwahi kuwambia kwamba ni vema wakatafuta nafasi za kutumikia wananchi kwa maana ya serikali/mitaa, udiwani na ubunge alafu wakishaaminiwa wapewe nchi, walipuuza ushauri wa baba wa taifa, huwezi kuwa na wabunge 27 kati ya majimbo 266, alafu unataka Urais, ni aibu sana, wangetumia nguvu nyingi kwenye ubunge na udiwani maana yake tungepata hiyo tume huru na sheria nyingi zingekaa vizuri na ndo shida ya watz, wao wamekomaa na Urais wakati wagombea wao tena walio wengi hawana fedha za kufanyia kampeni, kila siku wimbo wao ni tume ya uchaguzi.
Kweli katika hali ya kawaida utawapatia nchi watu ambao kila kukicha ugombana kwenye nafasi za majimbo? hii nafasi ya Urais bado haiwafai kabisa.