Namsaidiaje mtu anayepatwa na hii hali

Namsaidiaje mtu anayepatwa na hii hali

CPR ni nini? CPR ni kifupisho cha neno “Cardiopulmonary resuscitation” ikiwa na maana ya kufufua moyo na mapafu viweze kufanya kazi. Ni kitendo cha kubana kifua ili kuweza kurejesha mapigo ya moyo kwa mtu ambaye amepatwa na mshituko wa moyo.

CPR inakazi mbalimbali na inawezesha kutoa msaada wa hali ya juu kuliko inavyofikiriwa. CPR inafanya kazi zaidi ya “kuwezesha moyo kusukuma damu.” CPR ni huduma ya kwanza inayowezesha kupelekwa kwa hewa safi ya oxygen kwenye ubongo na viungo vingine muhimu hadi mgonjwa atakapopata matibabu rasimi. Je unajua kuwa 75% ya matukio yote ya mshtuko wa moyo hutokea nyumbani? CPR inampa mtu nafasi maradufu ya kumuokoa mara apatapo shambulio la mshtuko wa moyo au magonjwaa kama pump /asthma

CPR inaokoa maisha ndio maana ni muhimu kila mmoja kujifunza mbinu hii.

Mara kadhaa, kwa matukio yanayotokea nje ya hosipitali, wahathirika wa matukio ya
Mambo kama haya inabidi watoto mashuleni wafundishwe ...angalau hata basic tu
Ila mpaka sasa asilimia kubwa wa watu hawajui masuala haya

Ova
 
Mambo kama haya inabidi watoto mashuleni wafundishwe ...angalau hata basic tu
Ila mpaka sasa asilimia kubwa wa watu hawajui masuala haya

Ova
Serikali yetu ni sikivu nazani tunakoelekea wataanza kufundisha mashuleni
 
Vipi kama hiyo hali ya kukoroma ivo haikuwahi kumpata hapo kabla,,,imetokea tu na umauti umemfika,,nazani kulikuwa na haja ya kuwa na uhakika zaidi juu ya kifo chake kama ni pumu kweli ama kuna something else.
 
Habarini za majukumu

Niende moja moja kwenye mada. Jana asubuhi nilipata habari za msiba, kuna kijana mwenzetu amefariki .

Huyu kaka toka tunamfahamu hatukuwahi kumuona au kusikia anamatatizo yoyote kiafya, iko hivi juzi alishinda vizuri tu hadi kufika usiku , alikula vizuri, piga stori saana hadi tano usiku na wapangaji wenzie kisha kwenda kulala,

Kuna Dada mpenzi wake alikuwa anaish nae Mara moja moja anakuja na kuondoka ,sasa kipindi cha hivi karibun kabla umauti haujamkuta huyu Dada alikuwa nae kama miezi miwil mitatu hivi,( nimemtaja huyu kama mtu wake wa karibu marehem ambaye labda angeweza kumsaidia)

SAA tano waliingia kulala ,ilipofika mida ya saa nane marehemu alianza kukoroma saaana hadi nje kwa majiran kuna baadhi walimsikia, yule mpenz wake baada ya kuona hivo akawa anamuamsha lakini hakuamka, akatoka kuwaamsha majiran wamsaidie ,hali walivoona hawaelew waliwataarifu ndugu wakaja wakampeleka hospitality

Wanafika Hosp wanaambiwa mgonjwa alishafariki, sasa naona hata madaktar hawakuhangaika sana mana tulitaman kujua kilichomuua marehem hatukujua,

Badae tunakuja kusikia kwa ndugu kuwa marehem alisumbuliwa na pumu ndo ugonjwa wake toka akiwa mdogo kuna muda ilimsumbua sumbua

Sasa Mimi nilitaka kujua tu endapo utapatwa na mgonjwa kama huyo utamsaidiaje kwa haraka kama huduma ya kwanza kuokoa maisha yake?

Nawasilisha

Pumzika kwa amani Mario kijana mdogo mpambanaji ,msafi,mpole, tumeumia wenzio
Wenye pumu huwa kuna dawa zao na sindano zipo, ndugu sio wa kuwaamini sana inawezekana kuchukuliwa mtaji wa maisha 50/50 hio
 
Kuna umuhimu wa kuwaambia ukweli wenza wetu juu ya hali zety za afyaa hasa kama una changamotoo ya magonjwa kama Pumuu..Kifafa au matatizo yoyote ya moyoo yani muhimu sana na awe anajua dawa zako zinapokaa au unapoweka.
 
Back
Top Bottom