Namsaidiaje mtu anayepatwa na hii hali

Namsaidiaje mtu anayepatwa na hii hali

Poleni sana...

Hapo kuna walakini kwa kusema kwamba alilala na demu wake,maana vijana wa sasa akisikia demu wake anakuja huwa wanajiandaa na mikongo/viagra etc huenda labda alijichangana na hayo makitu yakamletea shida.

Pia kuna cardiac arrest inaondoa sana watu fasta.
 
Habarini za majukumu

Niende moja moja kwenye mada. Jana asubuhi nilipata habari za msiba, kuna kijana mwenzetu amefariki .

Huyu kaka toka tunamfahamu hatukuwahi kumuona au kusikia anamatatizo yoyote kiafya, iko hivi juzi alishinda vizuri tu hadi kufika usiku , alikula vizuri, piga stori saana hadi tano usiku na wapangaji wenzie kisha kwenda kulala,

Kuna Dada mpenzi wake alikuwa anaish nae Mara moja moja anakuja na kuondoka ,sasa kipindi cha hivi karibun kabla umauti haujamkuta huyu Dada alikuwa nae kama miezi miwil mitatu hivi,( nimemtaja huyu kama mtu wake wa karibu marehem ambaye labda angeweza kumsaidia)

SAA tano waliingia kulala ,ilipofika mida ya saa nane marehemu alianza kukoroma saaana hadi nje kwa majiran kuna baadhi walimsikia, yule mpenz wake baada ya kuona hivo akawa anamuamsha lakini hakuamka, akatoka kuwaamsha majiran wamsaidie ,hali walivoona hawaelew waliwataarifu ndugu wakaja wakampeleka hospitality

Wanafika Hosp wanaambiwa mgonjwa alishafariki, sasa naona hata madaktar hawakuhangaika sana mana tulitaman kujua kilichomuua marehem hatukujua,

Badae tunakuja kusikia kwa ndugu kuwa marehem alisumbuliwa na pumu ndo ugonjwa wake toka akiwa mdogo kuna muda ilimsumbua sumbua

Sasa Mimi nilitaka kujua tu endapo utapatwa na mgonjwa kama huyo utamsaidiaje kwa haraka kama huduma ya kwanza kuokoa maisha yake?

Nawasilisha

Pumzika kwa amani Mario kijana mdogo mpambanaji ,msafi,mpole, tumeumia wenzio
Poleni sana wakuu.
Hope watu watakua wameeleza huko chini, kama sitaona usaidizi nitaeleza pia. [emoji120]
 
Unampaje mtu kalala
Inapuliziwa mdomoni. Iko kama spray inaitwa inhaler.
Mtu mwenye tatizo la pumu ni vema akawa na hii dawa kila aendako pia ajiepushe na vumbi ama moshi,upepo ama marashi makali.
Ikiwa anaendesha gari basi asipende kutembea umbali mrefu peke yake ama bila kuwajuza wa karibu yake wapi anakwenda.
 
Wewe songa mbele tu na maisha yako na uzidi kutafuta hela ukisubiria na wewe siku yako ifike. Usiumize kichwa sana. Mwenzako aliyetangulia ana bahati kwani atapumzika milele na kuepukana na mikimiki, kero, uonevu, madharau na maudhi ya wenye kiburi cha maisha na uzima.
Nafahamu coz siwez kumfufua, ila yote ni kujifunza jaman bado tupo hai huwez jua ya kesho, unapata mgonjwa wa hivyo utamuacha afe huku unamuona?
 
Dawa ya kutuliza kabla ya Ile miruzi ya firimbi, ni gongo.
 
Habarini za majukumu

Niende moja moja kwenye mada. Jana asubuhi nilipata habari za msiba, kuna kijana mwenzetu amefariki .

Huyu kaka toka tunamfahamu hatukuwahi kumuona au kusikia anamatatizo yoyote kiafya, iko hivi juzi alishinda vizuri tu hadi kufika usiku , alikula vizuri, piga stori saana hadi tano usiku na wapangaji wenzie kisha kwenda kulala,

Kuna Dada mpenzi wake alikuwa anaish nae Mara moja moja anakuja na kuondoka ,sasa kipindi cha hivi karibun kabla umauti haujamkuta huyu Dada alikuwa nae kama miezi miwil mitatu hivi,( nimemtaja huyu kama mtu wake wa karibu marehem ambaye labda angeweza kumsaidia)

SAA tano waliingia kulala ,ilipofika mida ya saa nane marehemu alianza kukoroma saaana hadi nje kwa majiran kuna baadhi walimsikia, yule mpenz wake baada ya kuona hivo akawa anamuamsha lakini hakuamka, akatoka kuwaamsha majiran wamsaidie ,hali walivoona hawaelew waliwataarifu ndugu wakaja wakampeleka hospitality

Wanafika Hosp wanaambiwa mgonjwa alishafariki, sasa naona hata madaktar hawakuhangaika sana mana tulitaman kujua kilichomuua marehem hatukujua,

Badae tunakuja kusikia kwa ndugu kuwa marehem alisumbuliwa na pumu ndo ugonjwa wake toka akiwa mdogo kuna muda ilimsumbua sumbua

Sasa Mimi nilitaka kujua tu endapo utapatwa na mgonjwa kama huyo utamsaidiaje kwa haraka kama huduma ya kwanza kuokoa maisha yake?

Nawasilisha

Pumzika kwa amani Mario kijana mdogo mpambanaji ,msafi,mpole, tumeumia wenzio
Jinsi yabkumsaidia ni kuhakikisha anakuwa na dawa zake za kuvuta kwa kitaalamu inaitwa inhalor na pia kama ni mtoto au mpenzi unampumulia maana anakuwa anashindwa kuvuta hewa pia unaweza kumfanyia CPR au kumkanda kwa nguvu kwenye kifua mwisho unamuwaisha hospital
 
Unadhani ukisema CPR sie laymen tunaelewa? tumia lugha nyepesi tuelewe ndugu yangu. CPR ndo mnyama gani?
 
Kuna dada mmoja nilipata kusoma nae na ana tatizo hilo alikuwa anatembea na kile kidude kinaitwa inhaler,sasa walimwengu bwana tulikuwa tukimwona nacho tulikuwa tunahisi anafanya show off;kwasababu kama tunavyojua kipindi cha miaka ya nyuma kidogo kulikuwa na magonjwa ya wenye hela ikiwemo pumu, kwahyo tulikuwa tunahisi nae anatembea nacho ili tujue kwamba familia yao wana hela sana kumbe yalikuwa ni maelekezo ya daktari. Mungu anisamehe nilimhukumu yule dada bila kujua.
 
Unadhani ukisema CPR sie laymen tunaelewa? tumia lugha nyepesi tuelewe ndugu yangu. CPR ndo mnyama gani?
CPR ni nini? CPR ni kifupisho cha neno “Cardiopulmonary resuscitation” ikiwa na maana ya kufufua moyo na mapafu viweze kufanya kazi. Ni kitendo cha kubana kifua ili kuweza kurejesha mapigo ya moyo kwa mtu ambaye amepatwa na mshituko wa moyo.

CPR inakazi mbalimbali na inawezesha kutoa msaada wa hali ya juu kuliko inavyofikiriwa. CPR inafanya kazi zaidi ya “kuwezesha moyo kusukuma damu.” CPR ni huduma ya kwanza inayowezesha kupelekwa kwa hewa safi ya oxygen kwenye ubongo na viungo vingine muhimu hadi mgonjwa atakapopata matibabu rasimi. Je unajua kuwa 75% ya matukio yote ya mshtuko wa moyo hutokea nyumbani? CPR inampa mtu nafasi maradufu ya kumuokoa mara apatapo shambulio la mshtuko wa moyo au magonjwaa kama pump /asthma

CPR inaokoa maisha ndio maana ni muhimu kila mmoja kujifunza mbinu hii.

Mara kadhaa, kwa matukio yanayotokea nje ya hosipitali, wahathirika wa matukio ya
 
Mmmmhhh.... Inashauriwa kwa mtu mwenye pumu, ndani asikose Inhaler.. Yan kifupi popote pale awe nayoooo
 
Sasa Mimi nilitaka kujua tu endapo utapatwa na mgonjwa kama huyo utamsaidiaje kwa haraka kama huduma ya kwanza kuokoa maisha yake?

Nawasilisha

Pumzika kwa amani Mario kijana mdogo mpambanaji ,msafi,mpole, tumeumia wenzio
Kama tatizo ni pumu mpatie dawa zake za kuvuta haraka.

Kama amepaliwa mgeuze umgonge mgongoni kwa nguvu.

Kama hujui sababu ni nini ,compress kifua chake kama vile unapump moyo wake na kumuingizia hewa ya mouth to mouth breathing mpaka utakapofika hospitali.

Siku nikipata nafasi nitatoa somo la huduma ya kwanza humu kwa wagonjwa wa cardiac arrest na airway obstruction
 
Back
Top Bottom