Nampongeza Sana Huyu Mwalimu

Nampongeza Sana Huyu Mwalimu

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,270
Ni mwalimu wa Hisabati Shule ya Msingi Kimara B wilayani Kinondoni.
Mwanafunzi aliyepata alama 50 juu ya 50 katika somo la Hisabati alifundishwa na mwalimu huyu
aitwaye Aron Athanas

Kwa mujib wa mahojiano mwalimu huyu aliyoyafanya na televishen ya East Africa, mwalimu huyu
alieleza kwamba kwenye mitihani ya taifa anaandaa wanafunzi wake kuanzia darasa la tatu.Msichana Rachel Kiunsi ni mmoja wa
wanafunzi walioandaliwa na mwalimu huyu kwenye somo la hisabati tangu wakiwa darasa la tatu.
Mwalimu huyu anaeleza kwamba anatumia mbinu alizobuni za kuwavuta wanafunzi kulipenda somo la hisabati
na mbiu hii inatokana na motisha binafsi alio nao na si motisha kutoka serikalini.

Bila shaka wapo waalimu wengi wa aina hii ya mwalimu aron ambao wamejaa ubunifu katika ufundishaji wa masomo lakini serikali haiwaongezei motisha kwenye ufundishaji kwa kuboresha maslahi na vifaa vya ufundishaji.

Yanayotokea wizara ya afya ndio polepole yananyemelea wizara ya elimu na itafika siku akina aron watagoma, na hapatakuwepo tena wanafunzi kama Rachel na wengineo kupata alama A au B kwenye masomo yao.
KIUNSI.jpg
Mwanafunzi Rachel Kiunsi
 
Asanteni sana nyote. Nimefarijika sana kwa pengezi zenu watu wangu. Najua mnatambua kuwa juhudi za walimu ni kubwa hasa katika kuliendeleza taifa hili. Mwisho nasema wapendeni sana watoto na muwape Moyo kabla ya kukata tamaa.
 
Ni mwalimu wa Hisabati Shule ya Msingi Kimara B wilayani Kinondoni.
Mwanafunzi aliyepata alama 50 juu ya 50 katika somo la Hisabati alifundishwa na mwalimu huyu
aitwaye Aron Athanas

Kwa mujib wa mahojiano mwalimu huyu aliyoyafanya na televishen ya East Africa, mwalimu huyu
alieleza kwamba kwenye mitihani ya taifa anaandaa wanafunzi wake kuanzia darasa la tatu.Msichana Rachel Kiunsi ni mmoja wa
wanafunzi walioandaliwa na mwalimu huyu kwenye somo la hisabati tangu wakiwa darasa la tatu.
Mwalimu huyu anaeleza kwamba anatumia mbinu alizobuni za kuwavuta wanafunzi kulipenda somo la hisabati
na mbiu hii inatokana na motisha binafsi alio nao na si motisha kutoka serikalini.

Bila shaka wapo waalimu wengi wa aina hii ya mwalimu aron ambao wamejaa ubunifu katika ufundishaji wa masomo lakini serikali haiwaongezei motisha kwenye ufundishaji kwa kuboresha maslahi na vifaa vya ufundishaji.

Yanayotokea wizara ya afya ndio polepole yananyemelea wizara ya elimu na itafika siku akina aron watagoma, na hapatakuwepo tena wanafunzi kama Rachel na wengineo kupata alama A au B kwenye masomo yao.
View attachment 201796
Mwanafunzi Rachel Kiunsi
Asante sana Mkuu. Nafarijika kwa kunipa Moyo. Karibu Kimara B s/m uone watoto wanavyofurahia hisabati.
 
Walimu mnatafuta kiki hatujasahau mlichomfanya yule dogo

Walimu hatuwezi kutafuta kick kupitia mitandao ya kijamii. Kama ni kick IPO tu. Kitendo cha wewe tu kujua ku-log in hapa JF tayari kick kwa mwalimu.
Tatizo sio hata la kwako, wewe kudharau walimu ni matokeo ya kitu kingine kabisa ambacho kwa uelewa wako (maana tayari nimeshakupima) wala hautanielewa. Nikusamehe bure tu.
 
Big up. Namkumbuka teacher wangu alikuwa ananipa zawadi kila nikipiga 47/50 pepa chini ya hapo viboko. Lakini mtihani wa mwisho nikapata 45/50 mwaka 2003 na ifunda tech ikanihusu.
 
hongera sana mwl.nami amenikumbusha mwl wang w primary alikuwa anatufundisha kiswahil ase alikuwa anatuandaa kwel tuliiva.
[HASHTAG]#asante[/HASHTAG] mwl
 
Back
Top Bottom