Nampongeza Sana Huyu Mwalimu

Nampongeza Sana Huyu Mwalimu

Yupo hai.. hadi hivi miaka ya karibuni alikuwa anafundisha msasani.. sina uhakika kama ameshastaafu... jamaa ni kichwa mno.. back in the days mbuyuni kulikuwa na omary. msasani hyera.. wakali wa namba hao
Msasani pale mvua ikinyesha mwalimu mkuu anakimbilia darini. Maana pale kunabonde la kutuamisha maji. Sisi walimu tunafanya kazi katika mazingira magumu sana.
 
Walimu mnatafuta kiki hatujasahau mlichomfanya yule dogo
Unachanganya hadithi mbili tofauti,hapa tunazungumzia mafanikio na pongezi kwa mwalimu wetu kumjenga mtoto kulipenda somo la hesabu hadi mwanafunzi wake kapata ufaulu wa juu zaidi,wewe unazungumzia makosa ya watu wengine tena kwa wakati na sehemu isiyokuwa sahihi.Acha kuwajengea chuki waalimu hata kwa mazuri wanayoyafanya,Watu kama nyinyi nahisi hata watoto wenu mnawapotosha.Ningekua mwalimu ningekua nafuatilia tabia za wazazi alafu nalinganisha na tabia za mtoto wake ili mtoto anapokosea nijue tabia kajifunza kwa mzazi au jamii na hatua gani nichukue kumsaidia mtoto maana watu wengi sasa wanazaa bila kutoa malezi mazuri kwa familia zao kwakua huenda mlezi mwenyewe tabia zake si njema hivyo watoto huweza kuiga tabia za wazazi au la.! kwa kua maji hufuata mkondo
 
Ni mwalimu wa Hisabati Shule ya Msingi Kimara B wilayani Kinondoni.
Mwanafunzi aliyepata alama 50 juu ya 50 katika somo la Hisabati alifundishwa na mwalimu huyu
aitwaye Aron Athanas

Kwa mujib wa mahojiano mwalimu huyu aliyoyafanya na televishen ya East Africa, mwalimu huyu
alieleza kwamba kwenye mitihani ya taifa anaandaa wanafunzi wake kuanzia darasa la tatu.Msichana Rachel Kiunsi ni mmoja wa
wanafunzi walioandaliwa na mwalimu huyu kwenye somo la hisabati tangu wakiwa darasa la tatu.
Mwalimu huyu anaeleza kwamba anatumia mbinu alizobuni za kuwavuta wanafunzi kulipenda somo la hisabati
na mbiu hii inatokana na motisha binafsi alio nao na si motisha kutoka serikalini.

Bila shaka wapo waalimu wengi wa aina hii ya mwalimu aron ambao wamejaa ubunifu katika ufundishaji wa masomo lakini serikali haiwaongezei motisha kwenye ufundishaji kwa kuboresha maslahi na vifaa vya ufundishaji.

Yanayotokea wizara ya afya ndio polepole yananyemelea wizara ya elimu na itafika siku akina aron watagoma, na hapatakuwepo tena wanafunzi kama Rachel na wengineo kupata alama A au B kwenye masomo yao.
View attachment 201796
Mwanafunzi Rachel Kiunsi
HONGERA SANA MWALIMU ARON
Chama cha wanahisabati muifanyie kazi hiyo na muiendeleza kwenye shule nyingi iwezekanavyo na kama michango ya kuongezea sisi wadau wa elimu [wazazi tupo]
 
Umenikumbusha mwalimu wangu wa Airwing primary mana alinifanya nipate 48/50 kisha nikatumbukia zangu Azania na huko nikakutana na Lindugan Mlilile nikapiga zangu banda then mzumbe nikakutana na wakali kibao advance ila nikapiga A ila sijawah kuongoza advance math kule
 
Unachanganya hadithi mbili tofauti,hapa tunazungumzia mafanikio na pongezi kwa mwalimu wetu kumjenga mtoto kulipenda somo la hesabu hadi mwanafunzi wake kapata ufaulu wa juu zaidi,wewe unazungumzia makosa ya watu wengine tena kwa wakati na sehemu isiyokuwa sahihi.Acha kuwajengea chuki waalimu hata kwa mazuri wanayoyafanya,Watu kama nyinyi nahisi hata watoto wenu mnawapotosha.Ningekua mwalimu ningekua nafuatilia tabia za wazazi alafu nalinganisha na tabia za mtoto wake ili mtoto anapokosea nijue tabia kajifunza kwa mzazi au jamii na hatua gani nichukue kumsaidia mtoto maana watu wengi sasa wanazaa bila kutoa malezi mazuri kwa familia zao kwakua huenda mlezi mwenyewe tabia zake si njema hivyo watoto huweza kuiga tabia za wazazi au la.! kwa kua maji hufuata mkondo
Umeongea kama watu 1000 ndugu yangu. Mtu kama huyo labda tunaweza kusema haelewi anachomaanisha japo anataka kutuelewesha anachoongea ingawa hakina maana kwa watu ambao akili zao zinaendelea kusonga mbele. Watu kama hawa wanajaribu kuwakatisha tamaa watu wengine ambao wameshafikia mafanikio tena kwa juhudi zao wenyewe.
 
HONGERA SANA MWALIMU ARON
Chama cha wanahisabati muifanyie kazi hiyo na muiendeleza kwenye shule nyingi iwezekanavyo na kama michango ya kuongezea sisi wadau wa elimu [wazazi tupo]
Asante ndugu yangu. Nafarijika sana kwa pongezi zenu. Japo motisha ni changamoto lakini najua pongezi zenu ni motisha tosha kwa jasho jingi lililovuja bila malipo.
 
Umenikumbusha mwalimu wangu wa Airwing primary mana alinifanya nipate 48/50 kisha nikatumbukia zangu Azania na huko nikakutana na Lindugan Mlilile nikapiga zangu banda then mzumbe nikakutana na wakali kibao advance ila nikapiga A ila sijawah kuongoza advance math kule
Umeandika historia ndugu yangu. Wapo ambao hata c hawajawahi kuipata.
 
Asante ndugu yangu. Nafarijika sana kwa pongezi zenu. Japo motisha ni changamoto lakini najua pongezi zenu ni motisha tosha kwa jasho jingi lililovuja bila malipo.
Habari ya malipo usihofu !katika akiba bora kabisa za wema ni kumpa mtu elimu,omba uhai utakula sana matunda ya wanafunzi wako !
Mimi hivi sasa walimu wangu amabo wako hai wanafaidika na alichonijaalia mungu kupitia kwao walimu !nikiwaona huwanajisikia vingine kabisa kila hisani ninayowafanyia nahisi haitoshi mpaka kuna mmoja amekywa rafiki mkybwa wa mzee wangu kupitia mimi maana na muona kama baba yangu na najisikia faraja kuwasaidia wanawe amabao sasa wananiona kama kaka yao!
Wanafunzi waliofanikiwa hawasahau walimu wao au shule walizopitia.
Kwangu kisutu primary,tambaza secondary na forest hill high silikuwa karakana muhimu za kutengeneza elimu na maisha yangu!
 
Asante sana ndugu yangu. Umeongea vema kabisa.
 
Back
Top Bottom