Nampongeza Rais Samia kwa kukubali kuwa Mkuu wa Machifu Tanzania



Kwa hiyo ule utaratibu uliotumika kumtawaza/simika haukuhusisha ibada za matambiko na makafara ya mizimu? Unaposema ceremonial unamaanisha nini? Huyu chifu kwa utaratibu ule hakufanyiwa ibada ya mizimu, kuvishwa kaniki na ngosi ya chui? Kwenye ulimwengu wa kiroho upande wa kiza limefanyika jambo kubwa sana. Uislamu na Ukristo sijui unatuambia mambo yapi juu ya utaratibu huu.
 
Makafara ya kuzimu ni sawa na misa za kanisani na sala misikitini.

Hakuna tofauti yoyote.

Na as long as hayo makafara na hizo misa ni vitu vinavyobaki kuwa vya kufurahisha macho ya watu tu, haviingii katika kuendesha nchi kwa namna ya kupendelea upande fulani, then hakuna tatizo.

Ninachosema ni kwamba hicho cheo cha uchifu ni maigizo ya kufurahisha baraza, hakipo katika katiba wala sheria.

Nyerere alishakitoa.
 

Mizimu haina nguvu wala influence yeyote kwa muhusika si ndivyo unataka kutuaminisha?
 
Wachache sana watakuelewa!
In short kiti kimenajisika badala ya kuketishwa Mungu,imeketishwa miungu yenye jina hilo.
Na Mungu anachukia kuabudu miungu,subiri tuone Mungu hajawahi kushindwa, tunaendelea kuomba yupo Mungu.
 
Mizimu haina nguvu wala influence yeyote kwa muhusika si ndivyo unataka kutuaminisha?
Nguvu na influence maana yake nini?

Mizimu haina nguvu nje na watu watakayoipa mizimu.

Na hata kwenye dini ni hivyo hivyo, ndiyo maana namkwambia, haya yote ni kitu kile kile.

Mizimu, uchawi, sala, misa.

Majina tofauti, kitu kilekile.
 
Nchi hii inaongozwa na Mungu aliye hai,muumba was mbingu na nchi sio hiyo miungu ya kichifu!
 
Wachache sana watakuelewa!
In short kiti kimenajisika badala ya kuketishwa Mungu,imeketishwa miungu yenye jina hilo.
Na Mungu anachukia kuabudu miungu,subiri tuone Mungu hajawahi kushindwa, tunaendelea kuomba yupo Mungu.
Mungu mwenyewe hayupo, mizimu nayo haipo.

Zote ni hadithi za watu tu, kwa hivyo hata wewe unavyosema habari za Mungu, mimi nakuona bado unaongea habari za mizimu tu.
 
Nchi hii inaongozwa na Mungu aliye hai,muumba was mbingu na nchi sio hiyo miungu ya kichifu!
Ukiona mtu anamtajataja Mungu katika hoja za kawaida KABISA ujue analazimisha "USHINDI" wa kuimaliza hoja.....

Hata mtoto mdogo wa miaka 6 anajua MUNGU MWENYEZI ni alpha & Omega....ila si sababu ya kutokuwa na MACHIFU NA VIONGOZI WAKUU.....
 
Wachache sana watakuelewa!
In short kiti kimenajisika badala ya kuketishwa Mungu,imeketishwa miungu yenye jina hilo.
Na Mungu anachukia kuabudu miungu,subiri tuone Mungu hajawahi kushindwa, tunaendelea kuomba yupo Mungu.
Are you deluded?!!!!
 
Nguvu na influence maana yake nini?

Mizimu haina nguvu nje na watu watakayoipa mizimu.

Na hata kwenye dini ni hivyo hivyo, ndiyo maana namkwambia, haya yote ni kitu kile kile.

Mizimu, uchawi, sala, misa.

Majina tofauti, kitu kilekile.

Ziko programme za kumuombea Mkuu wa nchi kwenye baadhi ya makanisa na hata misikiti na fikiri hivyo. Wanapomuona Mkuu wa nchi kasimikwa uchief kwenye madhabahu ya hawa machief unafikiri unawaweka hawa kwenye position gani ya kumuombea ulinzi na hekima au kukemea mapepo?
 
Andiko LA Mwl Shija Samweli kutoka misungwi Mwanza;

RAIS AINGIZWA KINGI USUKUMANI

Ukweli ni kwamba,USUKUMANI hatujawahi kuwa na CHIFU wa jinsia ya kike na hatutarajii Kama atakuwepo kesho au kesho kutwa.

Usukumani hajawahi kuwepo CHIFU wa MACHIFU(ntemi o batemi) tangu mwanzo wa Zama za sukuma land (igunguli lya banhu ba sukuma).

Iko hivi;
1.kwa usukumani, cheo Cha UCHIFU hupewa wanaume tu(Ngosha)ndiyo maana tuna majina Kama CHIFU MALONJA,MASANJA NK

2.Wapo wanawake(bakima) waliowahi kupewa nafasi kubwa za "ulezi" wa ukoo(clan) ambapo cheo Chao waliitwa NGOLE(malikia).tunayo mifano kadhaa ya kina NGOLE wa kike Kama vile,MINZA,NGOLO,NG`WASHI,NKAMBA,NG`WISABI,na huyu NKWIMBA aliyepewa kuulea ukoo uliozaa jina la wilaya ya KWIMBA yenye mjumuiko wa wilaya za MISUNGWI na MAGU.
Ukikaa na msukuma yeyote,sikiliza salamu yake asubuhi.Utasikia maneno E-MINZA au E-NGOLO,E-NKWIMBA nk.hii ni heshima pekee inayotolewa kwa kuwakumbuka Hawa malikia kulingango na Koo zao na kamwe hautasikia msukuma anasalimia na kusema E-shija,E-magufuli,E-malonja au E-suluhu.

3.NGOLE/malikia(kiongozi wa kike) ni mlezi tu wa ukoo.mipango yote ya ulinzi na usalama hufanywa na NTEMI/ Chief akishirikiana na maakida/maaskali wakuu wa ikulu(bashilikale ba g'wi-kulu).

4. jina la HANGAYA Ni jina la nyota(sonda) inayong'aa Sana asubuhi ambapo mtu akizaliwa asubuhi Kabla nyota hiyo haijafifia anaweza kuitwa jina Hilo, haijarishi ni mwanamke au mwanume.usukumani hatujawahi kuwa na CHIFU wala NGOLE wa jina la HANGAYA.

5.ngoma za heshima za kumtawaza CHIFU(ng'oma ja milango) hazilii hovyohovyo Bali huandaliwa siku na utaratibu maalum tofauti na hiki kilichofanywa na UMT katika viwanja vya Redcross-magu.
Je,Ni Nani alishawahi kusikia "mkuu wa mkoa" wa "wakuu wa mikoa"?,au CHIFU wa MACHIFU?? Hiiiiiiiiii elelo twa lembiwa lemi nyange!!.tukisema rais ameingizwa kingi usukumani,hii ndiyo maana yake.
Hata Kama mna FURAHA,Fanyeni utafiti wa kutosha hasa kwenye matukio makubwa Kama haya.tofauti na hapo unaweza kushushwa hadhi bila kujua.

SHIJA ss SHIBESHI.
Misungwi.
 
Hata sijaelewa unachotaka kuuliza ni nini.

Naomba urudie vizuri.

Kwani kukemea mapepo hakuwezi kuendana na kumuombea mtu hekima na ulinzi?
 
Wacha we, sasa ulifikiri ustaarabu ndio Uafrika?
Waarabu wana... yao na sie tuna machifu
Desturi za kibantu, desturi za utu. "Ubuntu"
Desturi za kiarabu? we we
 
Open up your eyes and try to re-think beyond the horizon.....umejazwa "FIKRA" NA "ZIMEJAZIKA" kwelikweli.....

#SiempreChiefHangaya
 
Hata sijaelewa unachotaka kuuliza ni nini.

Naomba urudie vizuri.

Kwani kukemea mapepo hakuwezi kuendana na kumuombea mtu hekima na ulinzi?

Kukemea mapepo ni maombi ya vita ambayo yanaweza kuangamiza mapepo na muhusika kama alikuwa anayatumia na kuendelea kuyangangania unless ametubu na kuachana na njia hizo. Machief walimfata ama aliwafuata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…