nikupe kanuni yenye mafanikio,ukiona mwenzi wako hakuamini rudi kwenye kioo na ujiangalie wewe!amani ya moyo ya mwenzako haijengwi kwa mtutu,kulazimisha au kwa kulalama kwanini hauaminiwi!matendo yako,maneno yako,mtizamo wako na tabia zako ndizo zenye kuleta au kuondoa imani ya mwenzako juu yako!ukienenda ktk namna hatarishi kamwe usitarajie kupata imani ya mwenza wako.
uaminifu ili ukamilike unaendana na matendo ya kutia amani!kama hauna hiyari ya kuachana na mienendo yote ya kutia mashaka hivyo sahau kupata imani ya mwenza wako!jitizame mwenyewe urekebishe mambo na upate kilicho bora ktk mapenzi