Nampenda sana huyu binti

Nampenda sana huyu binti

Clemford

Member
Joined
Nov 26, 2011
Posts
63
Reaction score
91
Naleta kwenu wadau,

Yupo dada mmoja ambaye nimetokea sana kumpenda. Ukaribu wetu na kufahamiana kulianza mwaka huu mwezi January. Sasa baada ya kufahamiana kama marafiki kwa muda sasa nimetokea kumpenda na kumuhitaji maishani kama mke wangu. Nina miaka ishirini na nane sasa na ningetamani kuoa mwakani mambo yakienda vyema. Nisingependa kufika 30yrs sijaoa.

Tatizo langu ni moja, huyu binti baada ya kumweleza ukweli alinitamkia waziwazi kwamba ana mtu ambaye wako kwenye mahusiano japokuwa hawapo in good terms lakini wako pamoja. Swali langu ni moja, je niendelee kukaza uzi kwa huyu binti especially at this time akiwa na mahusiano shake? Au niachane nae tuendelee kuwa marafiki tu?

Naomba ushauri wenu wadau

Nawasilisha
 
Ila kiukwel bila kukurupuka zipo njia nying za kutafuta furaha, usikaribu kuvunja ya mwenzako kisa kujenga yako, utakuwa unakosea, kiukwel ndo nyie baadae mnagongewa wake zenu, kwa kulazmisha kwenu Ushaur
 
Last edited by a moderator:
tukuulize kwanza wewe moyoni mwako unaonaje?
 
Kwanin uweke benchmark ya umri wakati wa kufanya maamuzi makubwa kama hayo?...
Kama ulikuwa unahitaji kuingia kwenye ndoa kabla ya 30 kwanin hukumtafuta mpenzi mapema na kumuandaa kabisa?....
What if huyo akikukatalia?...
 
Naleta kwenu wadau,

Yupo dada mmoja ambaye nimetokea sana kumpenda. Ukaribu wetu na kufahamiana kulianza mwaka huu mwezi January. Sasa baada ya kufahamiana kama marafiki kwa muda sasa nimetokea kumpenda na kumuhitaji maishani kama mke wangu. Nina miaka ishirini na nane sasa na ningetamani kuoa mwakani mambo yakienda vyema. Nisingependa kufika 30yrs sijaoa.

Tatizo langu ni moja, huyu binti baada Ya kumweleza ukweli alinitamkia waziwazi kwamba ana mtu ambaye wako kwenye mahusiano japokuwa hawapo in good terms lakini wako pamoja. Swali langu ni moja, Je niendelee kukaza uzi kwa huyu binti especially at this time akiwa na mahusiano Shake? Au niachane nae tuendelee kuwa marafiki tu? Naomba ushauri wenu wadau.

Nawasilisha

 
Last edited by a moderator:
kama wako pamoja hata kama hawako in good terms kama usemavyo achana nae mkuu tafta kwingine ila mwisho wa siku akili za kuambiwa changanya na zako utapata jawabu
 
Sidhani kama itakua sawa kumvujia mwenzio ili upate wewe,na vile vile unahakika gani kama akitoka huko aliko utachukua wewe? Kheir kukosea kujenga kuliko kukosea kuoa, vuta subra mtangulize mwenyezi mungu kwenye kila jambo lako
na mwenye kheir na wewe atakuja..
As long as huyo mdada ameshakwambia yuko na mtu heshimu maamuzi yake na endelea na maisha yako bila kutaja kujua kama huyo bwana wanaelewana au laa, kama rizki yako atakuja.
 
kaza uzi tu kwani hayupo utakayemkuta yupo peke yake
 
Kaza uzi, dunia hii hamna mwanamke ambae hana mtu, nguvu yako ya ushawishi na tabia ndio ngao yako
 
kaza zaidi ataelewa tu... them not being in a good terms ndo golden opportunity yako ya kum-win huyo bimdada.... ukpunguza kasi na jamaa akijenga tena furaha katika mauhusiano yake... umeshamkosa huyo hadi urafiki utapotea
 
Mkuu tumia hiyo line of weakness kumaliza mambo kakurahisishia mmbo kwa kukwambia udhaifu wa mahusiano yake, tumia mwanya huo kumaliza mambo, ingekua mimi hapo ni sawa na kunitengea penalti na kumfunga golikipa mkono mmoja,nikikosa ni utaahira wangu.

Inaonekana huyo binti anampenda huyo jamaa yake ndio maan hataki kujitoa rasmi akitegemea labda jam atabadili mawazo na kujirudi.

Sasa wewe huu ndio wakati wa kumuonyesha upande mwingine wa mahusiano,onyesha kumpenda,kumjali bila kujali wako na mshakaji,fake mapenzi, mpe muda, mpe attention ya kutosha within weeks utafanikiwa.

Jaribu kumuonyesha pale alikosea hata kama anampenda mshikaji,na kwamba wewe ni the right choice kwake,mpe care ya kutosha kipindi hiki akiwa kwenye wakati mgumu, kua faraja yake awe anakukumbuka muda wote na kumis uwepo wako hata akiwa na jamaa yake uone kama hutamtafna bila yeye mwenyewe kujua ameliwaje.

Jifanye kujionyesha wewe ndio mwanaume alietakiwa kumpenda in the first place na sip mchizi wake.

ONYO: Usijaribu kumponda mshikaji,be your own.
 
Nkaushauri usikaze uzi,kwa sababu huyo mwanamke anampenda huyo aliyenaye japokuwa wametofautiana(ambalo ni jambo la kawaida)...ukilazimisha mambo ipo siku utaumia na hapo tayari utakuwa ndani ya ndoa,tafuta aliye single wapo wengi sana...

usitafute maumivu ya ndoa kwa lazima
 
One mistake one goal,mwenzako kashawekwa dosari hapo sasa chelewa chelewa ukute mwana si wako..
 
Wewe fanya yako ndugu, EVERYBODY FOR HIMSELF AND GOD FOR US ALL. Lines of weaknesses may lead you to success of failure depending on your convincing powers. Kila la kheri.
 
tatizo lako ni moja.........

swali langu ni moja..........
 
Back
Top Bottom