Nampenda lakini naelekea kuchoka.....

pepekale

Member
Nov 25, 2010
60
50
Nina mpenzi wangu nampenda sana , ila tatizo kubwa lililopo ni kwamba huko nyuma niliwahi kumsaliti na alinisamee tukaendelea na maisha, lakini toka amenisamee amekua ni mtu mwenye hasira na kuwahi kupaniki hata kwa sababu zisizo na msingi. Inafikia wakati ananiambia kama vipi tuachane coz mapenzi yameisha, ila akikaa siku mbili anakuja kwangu ananiomba msamaha huku akilia na kuniambia ananipenda sana. Kiukweli hali hii imekua ikijirudia mara kwa mara mpaka imekua kero kwangu hadi nahisi mapenzi yameanzakupungua na siku zinavyokwenda naweza kumwacha kabisa,ila sitaki tufike huko. Msaada tafadhari nini nifanye ili niweze kuweka mambo sawa .
 
Mwambie hashike zake na wewe zako kwa muda wa mwezi kama kila mmoja anajisikia kuendelea na mwenzake baada ya mwezi poa, ila kama manunguniko yapo ipo siku atakukata uume kisa uvivu.Mapenzi sio kulazimishana kama unatakiwa kulipa deni flani
 
pole, kwa sababu hayo ndo matunda ya kumcheat umpendaye unapoteza uaminifu hata kama utasamehewa mambo hayatakua kama zamani, ndo maana kuna msemo wa NIMEKUSAMEHE LAKINI SITASAHAU.
 
Well said Navoyne, mtengane kwa muda pasi mawasiliano yoyote then after say a month mkutane mfanye tathmin ya uhusiano wenu and mtadecide whether to continue au kuseparate.
 
Last edited by a moderator:
Hapo uaminifu juu yako umepungua.. Mtengenezee mazingira yatayomfanya akuamin, Mazingira yatayomdhihirishia kuwa yuko peke yake..
 
Huo ni mshahara wa dhambi uliyoitenda. Ni lazma ulipe gharama yake. Atachukua muda mrefu kukuamini tena. Kiukweli wakati unamsaliti mwenza anakuwa anajua na kuhisi kwa sababu lazma kuna dalili huwezi ficha. Na mwingine anaweza kukuinya na kuuliza mbona husomeki. Inapodhihirika anajumlisha dots zote na.kujua hatua mlizopitia. Akiziona dalili zinajirudia hatosita kuhamaki na kusema tuachane.
Msitengane manake atakuacha kiukweli, ama atakusaliti kipindi cha uhamishoni. Acha tabia zinazomtia mashaka. Angalia vitu unavyotenda na kumpelekea kusema tuachane. Mtu alieugua kifua kikuu anazijua dalili zake. Akianza kukohoa huwezi mzuia kuogopa. Ukuacha gap hapo unalizwa, kama umechoka achana nae for sure!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Nina mpenzi wangu nampenda sana , ila tatizo kubwa lililopo ni kwamba huko nyuma niliwahi kumsaliti na alinisamee tukaendelea na maisha, lakini toka amenisamee amekua ni mtu mwenye hasira na kuwahi kupaniki hata kwa sababu zisizo na msingi. Inafikia wakati ananiambia kama vipi tuachane coz mapenzi yameisha, ila akikaa siku mbili anakuja kwangu ananiomba msamaha huku akilia na kuniambia ananipenda sana. Kiukweli hali hii imekua ikijirudia mara kwa mara mpaka imekua kero kwangu hadi nahisi mapenzi yameanzakupungua na siku zinavyokwenda naweza kumwacha kabisa,ila sitaki tufike huko. Msaada tafadhari nini nifanye ili niweze kuweka mambo sawa .

sababu za wewe kucheat ilikuwa ni nini kama unampenda sana? Kama yeye alikuwa amekosa vitu fulani vilivyokulazimu kucheat then huna haja ya kuendelea naye maana kama utendelea kuvikosa waweza kuja kurudia tena na matatizo kuendelea.

Lakini kama ulipitiwa tu na shetani, naungana na the HEART kuwa ni vyema umjengee mazingira kwamba sasa yuko pekee yake na hivyo akuamini na makosa uliyoyafanya umeyajutia na hautarudia tena.

Ila ukweli ni kuwa mtu akikukamata umecheat ni ngumu sana kukuamini kwa asilimia mia ...
 
Last edited by a moderator:
Kama hamna ndoa mnaweza kuachana ila tatizo sio kulikimbia ni kulitatua,nendeni kwa watu wa pschology watawapa ushaur mzur na mtafurahia maisha
 
Well said Navoyne, mtengane kwa muda pasi mawasiliano yoyote then after say a month mkutane mfanye tathmin ya uhusiano wenu and mtadecide whether to continue au kuseparate.

Kwanza kabisa ningeshangaa kama hii thread ingewapita CIELLO na HEART bila kuichangia, big up wadada wangu yaelekea mengi ya conflict za kimapenzi zinazoletwa humu zimewagusa au zimewapata kwa kiasi chake. Hebu tupeni na nyie ya kwenu. Karibu weekend.
 
Mkuu Miwatamu binafsi nina experienc ndogo ktk mapenzi mie kwa sehemu kubwa ni mtazamaji japo nimewah kuwa kwenye uhusiano,smtms naobserve kwa watu wa karibu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Miwatamu binafsi nina experienc ndogo ktk mapenzi mie kwa sehemu kubwa ni mtazamaji japo nimewah kuwa kwenye uhusiano,smtms naobserve kwa watu wa karibu
Siku zote si kila anayeogopa unyasi unapotikisika ameshawahi kuumwa na nyoka.
 
Last edited by a moderator:
let matters take their natural ways, if this love was meant for you it will work and if not it will never work out. think all the possibilities and choose the right way for you two.
inawezekana kabisa ukawa umebadilika ila jamii (yeye) bado hakupi nafasi ya kuamin kwamba umebadilka so you can't tolerate that shit for the rest of your life, just quit so as to have peace of mind and while thinking what to be the next step.

angekuwa mke/mume i would have suggested otherwise but just a girlfriend/boyfriend no ways ondoka tena kwa amani tu then you shall see the goodness of God.
 
Nina mpenzi wangu nampenda sana , ila tatizo kubwa lililopo ni kwamba huko nyuma niliwahi kumsaliti na alinisamee tukaendelea na maisha, lakini toka amenisamee amekua ni mtu mwenye hasira na kuwahi kupaniki hata kwa sababu zisizo na msingi. Inafikia wakati ananiambia kama vipi tuachane coz mapenzi yameisha, ila akikaa siku mbili anakuja kwangu ananiomba msamaha huku akilia na kuniambia ananipenda sana. Kiukweli hali hii imekua ikijirudia mara kwa mara mpaka imekua kero kwangu hadi nahisi mapenzi yameanzakupungua na siku zinavyokwenda naweza kumwacha kabisa,ila sitaki tufike huko. Msaada tafadhari nini nifanye ili niweze kuweka mambo sawa .

hiyo n hali ya kawaida kabisa hasa pale inapotokea mwenzako kakusaliti,anahitaji mda na ww pia play your party kumuonyesha kwamba hali ile haitajirudia..sasa kama unampenda na yeye anakupenda why ufikie kufikria kumuacha wakati ushajua tatizo liko wapi,ama unazani kumpata anaekupenda kwa dhat na mwaminifu ni simple sana,
 
Kusalitiana kuna laana kubwa mno haswa kwa watu walioaminiana na kupenda sana.Hata ukimuambia i love you anahisi unamjambisha,ukienda mbali kidogo lazima fikra ziame atahisi unafanya ule upuuzi.Raha ya kuaminiana inapoteza fikra chafu kwa mpz wako.
 
hamna chakuweka sawa hapo. wee mbwage tuu mapenzi gani full vitisho kila baada ya siku kadhaa?
 
Nina mpenzi wangu nampenda sana , ila tatizo kubwa lililopo ni kwamba huko nyuma niliwahi kumsaliti na alinisamee tukaendelea na maisha, lakini toka amenisamee amekua ni mtu mwenye hasira na kuwahi kupaniki hata kwa sababu zisizo na msingi. Inafikia wakati ananiambia kama vipi tuachane coz mapenzi yameisha, ila akikaa siku mbili anakuja kwangu ananiomba msamaha huku akilia na kuniambia ananipenda sana. Kiukweli hali hii imekua ikijirudia mara kwa mara mpaka imekua kero kwangu hadi nahisi mapenzi yameanzakupungua na siku zinavyokwenda naweza kumwacha kabisa,ila sitaki tufike huko. Msaada tafadhari nini nifanye ili niweze kuweka mambo sawa .

Marry your best friend you won't get tired .imagine that
 
"How Will I Know"

There's a boy I know, he's the one I dream of
Looks into my eyes, takes me to the clouds above
Ooh I lose control, can't seem to get enough
When I wake from dreaming, tell me is it really love

[Chorus:]
How will I know (Don't trust your feelings)
How will I know
How will I know (Love can be deceiving)
How will I know
How will I know if he really loves me
I say a prayer with every heart beat
I fall in love whenever we meet
I'm asking you what you know about these things
How will I know if he's thinking of me
I try to phone but I'm too shy (can't speak)
Falling in love is all bitter sweet
This love is strong why do I feel weak

Oh, wake me, I'm shaking, wish I had you near me now
Said there's no mistaking, what I feel is really love

[chorus]

If he loves me, if he loves me not [X3]

[chorus]
 
Last edited by a moderator:
Nina mpenzi wangu nampenda sana , ila tatizo kubwa lililopo ni kwamba huko nyuma niliwahi kumsaliti na alinisamee tukaendelea na maisha, lakini toka amenisamee amekua ni mtu mwenye hasira na kuwahi kupaniki hata kwa sababu zisizo na msingi. Inafikia wakati ananiambia kama vipi tuachane coz mapenzi yameisha, ila akikaa siku mbili anakuja kwangu ananiomba msamaha huku akilia na kuniambia ananipenda sana. Kiukweli hali hii imekua ikijirudia mara kwa mara mpaka imekua kero kwangu hadi nahisi mapenzi yameanzakupungua na siku zinavyokwenda naweza kumwacha kabisa,ila sitaki tufike huko. Msaada tafadhari nini nifanye ili niweze kuweka mambo sawa .

....hakuna "amani" na imani tena hapo. Trust imechezewa, na kwakuwa ni 'fragile,' kama ni glass hiyo imekwisha vunjika... Hata uviokoteze vigae na kuviunga unga, huwezi rudisha tena Trust iliyopotezwa

You dont deserve her, and she dont deserve you. Kwakuwa 'mnapendana' lakini HAMUAMINIANI, nakushauri muachane "kwa wema" kabla ya shari kamili.

Pole. :cool:
 
Back
Top Bottom